If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, September 26, 2012

Jinsi CCM inavyowachukia watetezi wa Umma na kuwabeba wabadhirifu wa mali za Uma

Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imebariki kuondolewa kwa majina ya baadhi ya vigogo wakiwamo wabunge kuwania nafasi ndani ya chama hicho, maamuzi yanayotoa picha ya kung’oa watu wenye tuhuma mbalimbali.

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya kikao hicho, kazi kubwa ambayo imefanywa na Kamati ya Usalama na Maadili ya chama hicho iliungwa mkono na CC, huku wajumbe wa vikao hivyo viwili wakimpongeza Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, kwa kuridhia maamuzi magumu.

Kikao cha CC ambacho kilifanyika juzi kuanzia mchana na kumalizika saa 6:30 usiku, kilielekeza shoka lake kwa majina yote ya wabunge waliowania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambao walihusika katika utiaji saini azimio la kumung’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mapema mwaka huu.

Wabunge hao walisaini katika fomu maalum iliyoandaliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, kwa ajili ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Wabunge hao walichukuliwa uamuzi huo ili kuishinikiza serikali kuwafukuza mawaziri ambao wizara zao zilitajwa katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Kamati kwa kashfa mbalimbali na kuisababishia serikali hasara.

Wabunge wa CCM waliotia saini ni Nimrod Mkono ambaye ni Mbunge wa Musoma Vijijini, anayewania nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na; Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe ambaye anagombea ujumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Ludewa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina. Wote wamekatwa.

Mwingine ambaye jina lake limekatwa ni Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu ambaye ameomba kupendekezwa kugombea uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa.


Chanzo chetu kinasema kuwa CC pia imewaengua Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ambao wote walikuwa wakiwania uenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga. Wawili hao wamekuwa na mvutano mkali baina yao.

Wengine walioshukiwa na shoka hilo ni Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangalah na Mjumbe wa Baraza Kuu la Utekelezaji wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM), Hussein Bashe. Wote walikuwa wakiwania nafasi ya ujumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Nzega.

Pia wamo Mbunge wa Viti Maalum, Sara Msafiri ambaye alikuwa akiwania ujumbe wa NEC na Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe ambaye alikuwa akiwania uenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), mkoani Tabora.

Habari hizo zilisema sababu ya kuondolewa kwa Munde na Sara ni kutokana na kudaiwa kuwa na maslahi katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wakati huo wakiwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini. Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini chini ya Mwenyekiti wake, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, chini ya wajumbe watano ilipewa kazi ya kuchunguza kashfa hiyo na suala la wabunge kudai rushwa kutoka kwa Wizara ya Nishati na Madini.

Wengine ambao majina yao yameenguliwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Swai aliyekuwa akitetea nafasi hiyo.

Waliopendekezwa na CCM ni pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ambaye anawania ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Simanjiro; Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa anayegombea ujumbe wa Nec kupitia wilaya ya Monduli na Andrew Chenge ambaye anagombea ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Bariadi na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa ambaye anawania uenyekiti wa CCM mkoani Dodoma.

Wengine waliopeta katika CC ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba na kada maarufu Mayrose Magige na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, ambao wanagombea uenyekiti wa UWT Taifa.

Chanzo hicho kilisema Rais Kikwete kwa dhamira ya dhati aliamua kuungana na wajumbe wa kamati hizo kuhakikisha kuwa mtandao wa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya chama hicho unakosa nafasi ya kugombea.

“Wengi walioondolewa wameondolewa kwa kuwa wao ni mizizi ya ufisadi na kwa kawaida ukishang’oa mizizi ya mti lazima ukauke, tuliona hakuna haja kabisa ya kuleta kishindo kikubwa kwa kuwaondoa wale ambao mlikuwa mnawataja taja kuwa ni watuhumiwa wa ufisadi,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, asilimia 70 ya mtandao huo umeangukiwa na shoka hilo na sasa wanasubiri huruma ya Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo ilianza vikao vyake jana jioni.

“Kama tumewabakisha sana sana watakuwa ni asilimia tano tu, ambao hatukuwafahamu wakati tunafanya kazi ya kuchuja majina ya wanachama waliomba kugombea,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa Kanuni za uchaguzi wa chama hicho, kikao cha mwisho cha kutoa maamuzi ya wanachama wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi ni Nec ambacho kilianza jana mjini hapa chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete.

Akifungua kikao hicho Rais Kikwete, alisema katika kuhakikisha CCM inazidi kuwa na uhai na kupata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, CC imeamua kuondoa majina ya wagombea wakongwe na kutoa nafasi kubwa kwa vijana wasomi.

“Jana (juzi) CC tumemaliza saa sita na nusu usiku, kazi tuliyofanya ni kubwa na tumefurahi kwamba safari hii pamoja na kupata wagombea wengi wakiwamo wasomi wengi ni vijana, kwenye kamati hii tumeamua kuwapa nafasi zaidi vijana na wenzetu wakongwe wakapumzike,” alisema.

Alisema kati ya vijana wasomi waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho wamo waliopo vyuoni jambo linalotia moyo kuwa bado CCM iko hai, huku akibainisha wazi kuwa chama chochote cha siasa kikikosa mwamko wa vijana lazima kitakuwa na matatizo.

“Napenda nieleweke kuwa hatuwezi kuwa na chama cha watu wazima pekee, chama chenye mfumo huo hakitakuwa na mfumo mzuri wa uongozi, tumefanya hivi ikiwa ni fursa ya kukipa chama chetu uhai na taswira mpya, lakini kubwa zaidi ushindi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015,” alisema.

Alisema katika uchaguzi huo wa ndani wa chama hicho, wanachokitarajia ni kupata timu ya viongozi wenye uadilifu, shupavu, hodari na wenye kukitetea chama.

“Na nasisitiza hatutaki kiongozi mwenye ndimi mbili maana nasikia kuna watu wanatishia eti wakikatwa huku kwenye ugombea wanaenda vyama vingine, nasema hivi wenye nia hiyo waende kwa sababu hadi kufikia kutishia hivyo ina maana tayari wanazo nafasi huko, tunawatakia kila heri,” alisema.

Aliwataka wagombea watakaoshindwa kwenye uchaguzi huo kutokata tamaa kwa kuwa kushindwa kwao leo hakumaanishi hawawezi bali ni kutokana na nafasi finyu, lakini pia umuhimu wa mabadiliko na kutumia usemi kuwa kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi. “Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alisema chama kwanza mtu baadaye.”

Aidha, mwenyekiti huyo, alizungumzia suala la baadhi ya wagombea wa chama hicho kudaiwa kutoa rushwa, hali ambayo alisema inageuza uchaguzi kama biashara na kufafanua kuwa wagombea wa namna hiyo hawafai kwa kuwa hawajiamini wala kuthamini chama bali uongozi na kuwahakikishia kuwa safari hii Takukuru haitokuwa mbali nao na wakikamatwa wasimlaumu.

“Sheria ya rushwa inaanzia kwenye chama, najua wapo watu ambao wanakifanya chama chetu kinasemwa sana, nawaomba sana tutumie fursa hii kubadilika na kukipa chama chetu heshima,” alisema Rais Kikwete.

Pia Rais Kikwete aliwaonya wagombea ambao wamesababisha uchaguzi huo wa CCM kugeuka kuwa wa vurugu za silaha na kuwaeleza kuwa wamekifedhehesha chama hicho. “Watu mnafikia hatua ya kutumia mishale, bastola na mikuki, kugombea Nec tu mnashikiana silaha kweli, jamani uchaguzi si vita,” alisema.

Wakati NEC ikianza Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, alisema idadi halisi ya wajumbe wa NEC ni 216, lakini waliohudhuria ni 196 tu.

CHANZO NIPASHE

No comments:

Post a Comment

Maoni yako