If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, September 5, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AFANYA MKUTANO NA WANANCHI WA KATA YA MOLLO


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea kwa ukali wakati akionyeshwa ramani na Mpima wa Manispaa Selice Nzyungu ya eneo alilouziwa muwekezaji Ephatta Ministry na lile walilopewa wananchi wa kata ya Mollo katika Manispaa ya Sumbawanga.

Mkuu huyo wa Mkoa amelazimika kutembelea eneo hilo baada ya kupewa taarifa za awali na Kamati aliyoiunda katika kufuatilia mgogoro unaoendelea kati ya muwekezaji na wananchi wanaolizunguka shamba hilo.

Lengo kuu la ziara yake hiyo ya tarehe 02, Septemba 2012 ilikuwa ni kutembelea mashamba yakiwemo ya muwekezaji na wananchi pamoja na kuzungumza na wananchi na muwekezaji kwa kuchukua kero zao kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo.


Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa akizungumza kwenye Mkutano na wananchi wa kata ya Molo ambapo pia wawakilishi wa muwekezaji walialikwa kuskiliza na kutoa kero zao mbele ya wananchi wa kata hiyo.

Hata hivyo baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kusikiliza kero hizo aliwaahidi wananchi pamoja na muwekezaji kuendelea kuushughulikia Mgogoro huo kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa, Wizara na Taifani kwa ujumla kwa ustawi wa wote na maendeleo ya Mkoa na Nchi kwa ujumla. Alisema kuwa lengo lake sio kuegemea upande mmoja bali ni kutafuta haki kwa kila pande.

Aliwataka wananchi na muwekezaji kufungua upya milango ya mahusiano mazuri baina yao ili kumuunga mkono katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao umekuwa ukiibua sura mpya kwa vipindi tofauti.

  Wananchi wakitoa kero zao mbalimbali zikiwepo unyanyaswaji kwa kuchapwa viboko na kukatwa maskio kwa pindi wakutwapo na muwekezaji huyo wakipita shambani kwake au wakikata nyasi kwa ajili ya kulishia mifugo yao. 

Kero nyingine waliyoitoa ni kukosa maeneo ya kulima na kupata kipato kutokana na eneo kubwa kupewa muwekezaji ambalo eneo alilopewa ni hekta alfu kumi (10,000) kwa ajili ya ufugaji kwa mujibu wa Mkataba.

Uharibifu wa barabara pamoja Muwekezaji huyo kwenda kinyume na Mkataba wake wa kufuga na badala kulima zaidi ni kero pia ambayo waliitoa wananchi hao wa kata ya Molo.

Kwa picha zaidi bofya hapa 

No comments:

Post a Comment

Maoni yako