If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, September 26, 2012

Na Gazeti la Mzalendo: Mke wa Bill Gates kutua Arusha leo

Magreth Munisi

MKE wa Tajiri Mkubwa Duniani Bill Gates, na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan, wanatarajiwa kuwa miongoni mwa watu maarufu watakaohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Kilimo utakaofanyika jijini Arusha kuanzia leo.

Melinda Gates
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, ilisema mkutano huo utakaohudhuriwa na Melinda Gates ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates, utafunguliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mkutano huo ambao ni Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRF), utahudhuriwa pia na mawaziri wa kilimo na wakuu wa nchi nyingine za bara hili.

Ofisa Uhusiano wa AGRA Sylvia Mwichuli, alisema maandalizi yote ya mkutano huo yameshakamilika.

Watu wengine maarufu wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano pamoja na Tanzania ni Rais wa IFAD Dk Kanayo Nwanze na Waziri wa Kilimo wa Nigeria Dk Akinwumi Adesina.

Mkutano huo ambao lengo lake ni kujadili usalama wa chakula katika bara la Afrika, utaongozwa na Rais Kikwete akishirikiana na Koffi Annan.

“Lengo ni kujadili jinsi ya kuwa na usalama wa chakula katika bara hili, katika mijadala itakayofanyika suluhisho la kuwa na usalama wa chakula litafikiwa,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako