If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, October 9, 2012

Gazeti la Mwananchi: Pigo tena CCM

RUFAA YA UBUNGE WA SUMBAWANGA ULIOTENGULIWA YATUPWA

Na James Magai
Aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini 
Aeshi Hilaly


CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimepata pigo jingine kisiasa baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly ambaye alivuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.

Pigo hilo limekuja miezi miwili baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kutengua matokeo ya ubunge Jimbo la Igunga yaliyompa ushindi mgombea wake, Dk Dalaly Peter Kafumu, Agosti 21, mwaka huu.
Rufaa ya Hilaly ilitupiliwa mbali katika uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu, Januari Msoffe, Edward Rutakangwa na Engela Kileo, baada ya kubaini kasoro za kisheria.

Dosari hiyo ni kutokuwapo kwa mwenendo wa maombi ya mlalamikaji katika kesi ya msingi ya kuomba Mahakama impangie kiwango cha fedha ambacho alipaswa kulipa ikiwa ni amana ya kufungua kesi hiyo, kwa mujibu wa Kifungu cha 111 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

Katika uamuzi uliosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma, mahakama hiyo ilirejea kifungu na kusema mtu anayefungua kesi ya uchaguzi, ni lazima awasilishe maombi ili Mahakama impangie kiwango cha amana anachopaswa kulipa ndani ya siku 14 tangu kufungua kesi na kwamba ndani ya siku 14 nyingine tangu siku ya maombi hayo, Mahakama hiyo iwe imeshapanga kiwango hicho.

Jopo hilo la majaji likielezea umuhimu wa mwenendo huo, lilisema ni muhimu kwa sababu kuu mbili, moja ni kuipa nafasi Mahakama kuona kama maombi yaliwasilishwa ndani ya muda baada ya kesi kufunguliwa na pili ni kuona kama maombi hayo yaliamuliwa ndani ya muda tangu kuwasilishwa.


Mahakama hiyo ilisema kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 96 (1) na (3) za Kanuni za Mahakama ya Rufani, si jukumu la upande katika kesi kuamua kuwa nyaraka fulani ni muhimu au si muhimu katika rufaa, kama Wakili wa Hilaly, Richard Rweyongeza alivyodai, bali na kanuni hiyo, mahakama hiyo pia ilirejea uamuzi wake katika rufaa namba 8 ya mwaka 2008, Fedha Fund Limited na wenzake wawili, dhidi ya George T.Varghese pamoja na tafsiri ya Kanuni ya 85 (3) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani ya Kenya za mwaka 1979.

“...Tunarudia kusema kwamba kumbukumbu zinazohusiana na mwenendo wa maombi ya kupangiwa kiwango cha kulipa kama amana, ni nyaraka muhimu katika rufaa. Kutokuwapo kwa nyaraka hizo, rufaa haina nguvu chini ya Kanuni ya 96 (1) (k) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani, hivyo rufaa inatupiliwa mbali.”
Hata hivyo, Mahakama hiyo ilisema haiwezi kuamua upande wa warufani ulipe gharama za rufaa hiyo kwa kuwa kasoro zilizosababisha kutupiliwa mbali kwa rufaa hiyo ziliibuliwa na Mahakama yenyewe.

Hilaly hajaridhika
Akizungumzia hatua hiyo ya Mahakama jana, Hilaly alisema anafikiria kukata rufaa ili kuiomba irejee tena uamuzi wake kuwezesha rufaa hiyo kusikilizwa.

“Ninafikiria kuona jinsi ninavyoweza kukata rufaa, maana kutupwa kwa rufaa yangu kumetokana na makosa ya kiufundi katika mchakato wa kuiwasilisha,” alisema Hilaly na kuongeza:

“Kama unavyojua nilitiwa hatiani kwa makosa ya rushwa, kwa hiyo kutokata rufaa ni kama nakubaliana kwamba kweli nilitoa rushwa jambo ambalo siyo kweli, lazima niendelee kutafuta haki yangu.”
Alisema haogopi kurudi kwenye uchaguzi kwa sababu ana uhakika wa kushinda, lakini akasema ikiwa uchaguzi mdogo utafanyika sasa, hataweza kugombea kwani kifungu cha makosa ya rushwa kilichomtia hatiani, kinamzuia kugombea nafasi hiyo kwa miaka mitano.

Hilaly alivuliwa wadhifa huo Aprili 30, mwaka huu na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila kutokana na kesi iliyofunguliwa na Nobert Yamsebo aliyekuwa mgombea wa ubunge katika jimbo hilo kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, kupitia Chadema.

Hata hivyo, Mei 28, mwaka huu Hilaly alikata rufaa namba 55 ya mwaka 2012, dhidi ya Yamsebo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, na mtu aliyetajwa kwa jina la Vitus Kapufi, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu.

Julai 3, 2012, AG na Kalama nao walikata rufaa namba 65 ya mwaka 2012 dhidi ya Yamsebo wakipinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.

Malumbano ya Mawakili

Kutokana na rufaa hizo dhidi yake, Yamsebo kupitia kwa Wakili wake Victor Mkumbe, aliweka pingamizi la awali pamoja na mambo mengine, akidai kuwa Hilaly hakuwa amelipia ada ya kufungua rufaa hiyo ya Sh2,000.

Mahakama ya Rufani iliamua kuziunganisha rufaa hizo na Hilaly aliunganishwa na AG pamoja na Kalama wakawa waomba rufaa dhidi ya Yamsebo.

Kabla ya kuanza kusikiliza pingamizi la Yamsebo dhidi ya rufaa ya Hilaly, Mahakama hiyo ilibaini kutokuwapo kwa mwenendo huo wa maombi ya Yamsebo kupangiwa gharama za kufungulia kesi hiyo ya msingi.

Kutokana na kasoro hiyo, mahakama ilihoji na kutaka maoni ya mawakili wa pande zote kuhusiana na kasoro hizo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwema Punzi alijibu kuwa walimwandikia barua Msajili wa Mahakama ya Rufani Kanda ya Sumbawanga kumwomba mwenendo wa kesi hiyo pamoja na vielelezo vingine na kwamba walipopewa, mwenendo wa maombi ya gharama za kesi haukuwamo.

Wakili Mkumbe alisema kutokuwapo kwa mwenendo huo kunaifanya rufaa hiyo iwe batili na akaiomba Mahakama hiyo iitupilie mbali.

Hata hivyo, Wakili Rweyongeza alidai kuwa kukosekana kwa mwenendo huo hakuwezi kuifanya iwe batili, badala yake aliiomba Mahakamahiyo itumie mamlaka yake chini ya Kanuni ya 2 ya Kanuni za Mahakama ya Rufani, ili iweze kuendelea.

Alisema hata ikibainika kuwa gharama za kufungulia kesi hazikulipwa, anayeathirika ni mjibu rufaa, hoja ambayo iliungwa mkono na Wakili Punzi.

Katika uamuzi wake kwenye kesi ya msingi Namba 1 ya mwaka 2010, Mahakama Kuu ilikubaliana na baadhi ya hoja zilizotolewa na mlalamikaji na hatimaye kutengua ushindi wa Hilaly.
Katika uchaguzi huo, Hilaly alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 17,328, huku Yamsebo akipata kura 17,132.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako