Viongozi wa kidini wa Kikiristo na Kiislamu wamesema kuwa wanataka kufanya mkutano wa dini za imani mbalimbali mwishoni mwa mwaka kuhamasisha uelewa na kusaidia kuondoa mtindo hasi usiobadilika na usio sahihi.
Viongozi wa Kikiristo na Kiislamu wanafanya kazi kuhamasisha mazungumzo ya imani mbalimbali baada ya shambulio katika kanisa huko Jijini Nairobi lililomuua mtoto mmoja. [Simon Maina/AFP]
Viongozi kumi na watano kutoka makanisa mbalimbali ya kikiristo walikusanyika huko Wajir tarehe 26 Septemba kujadili kwa ufasaha na wananchi kuhusu Uislamu na kuhimiza mazungumzo ya heshima na ya amani na Waislamu katika wilaya hiyo.
Viongozi hao, ambao ni sehemu ya Ushirika wa Wakiristo wa Wajir, waliitisha mkutano huo kujibu filamu ya utata inayopinga Uislamu, "Innocence of Muslims", ambayo ilichochea upingaji wenye vurugu katika nchi kadhaa zenye idadi kubwa ya Waislamu.
Kutokana na mkutano huo, Wakiristo na Waislamu wamepanga kufanya mkutano wa dini za imani mbalimbali, kwa mujibu wa Mchungaji Eustus Nyagah wa Kanisa la Pentekoste la Afrika Mashariki huko Wajir. Mkutano huo unadhamiria kuwaleta watu pamoja kubadilishana mawazo kwa namna ya heshima na kusaidia kuondoa chuki, aliiambia Sabahi.
Alisema wenye siasa kali za kidini kwa pande zote mbili wanapaswa kuhukumiwa binafsi na siyo kuonekana kama taswira ya dini ya imani hiyo yote. "Kwa nini jamii kubwa inasumbuliwa kwa sababu ya vitendo au chuki za mtu binafsi mmoja? Huo ni utovu wa hali ya juu wa ustahimilivu na hatupaswi kuukubali," alisema.
Nyagah alilalamikia shambulio la guruneti la terehe 30 Septemba ambalo lilimuua mtoto mmoja na kujeruhi watu wengine tisa katika kanisa la Anglikani la Mtakatifu Polycarp katika wilaya ya Pangani jijini Nairobi, pamoja na vitendo vya vurugu vinavyowalenga wenye asili ya Kisomali baada ya mlipuko huo.
Mkutano huo haumaanishi kubadilisha imani lakini kuondoa picha za ukatili zinazotolewa na Wakiristo wenye msimamo mkali, alisema Mheshimiwa Rueben Njue, Mkuu wa Kanisa la Anglikani katika jimbo la Kaskazini Mashariki nchini Kenya.
"Waislamu na Wakristo kwa hakika wana vitu visivyobadilika kila upande dhidi ya upande mwingine," Njue aliiambia Sabahi. "Wanatia madoa ambayo tunatakiwa kuyakomesha kwa kutumia kinga ya dini."
Njue alilaumu tukio hilo na kusema hotuba na vitendo vya chuki dhidi ya maadili ya wakristo havitasaidia jamii kuendeleza uhusiano mzuri. " Tunapenda jamii kubwa ya Kiislamu kufikiria kwamba watu wachache wenye mawazo ya ukereketwa kupita kiasi wanawakilisha au wanazungumza badala ya jamii kubwa." aliiambia Sabahi. "Ukristo unasisitiza misingi ya upendo."
Tarehe 27 Septemba, Njue aliwakusanya pamoja viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu na mamlaka za ndani kujadili jinsi ya kusonga mbele kama jamii yenye umoja. Alisema viongozi wana matumaini ya kujenga historia ya muda mrefu ya Kenya ya kuaminiana kwa pamoja miongoni mwa watu wa dini zote, ambayo iliendeleza kuwepo kwa amani kwa miaka mingi.
Njue alisema Wakenya wanapaswa kujilinda dhidi ya wenye msimo mkali ambao wanajaribu kuanzisha mgawanyiko. "Mashambulio ya magaidi na matukio ya wanaopinga Uislamu yanakusudia kuleta vita kati ya Waislamu na Wakristo na Wakenya wanapaswa wasiwaunge mkono," alisema.
Mazungumzo ya imani tofauti yazuia ukereketwa
Baraza la maimamu na Wahubiri wa Kenya (CIPK) Tawi la Wajir wameonyesha kuunga mkono kwa jitihada za mkutano wa imani tofauti, wakisema utaendelea kuzuia wakereketwa wa pande zote.
Katibu wa Tawi la CIPK Wajir Shehe Abduwahab Mursal alisema CIPK itaendelea kujihusisha na jamii ya Kikristo. "Kama tutaalikwa na ndugu zetu Wakristo katika mazungumzo ya kidini, tutahudhuria kwa umoja," aliiambia Sabahi.
Viongozi wa Kiislamu na Kikristo pia wanapanga kuunda ujumbe wa uwakilishi wa pamoja kwa ajili ya kutembelea maeneo mengine ya nchi kama vile Garissa na Mandera kuhimiza mazungumzo ya amani, alisema.
Ofisa Wilaya wa Wajir Mashariki Kepher Kageni aliiambia Sabahi kwamba serikali inapanga kufanya kila linalowezekana ili kusaidia uwezeshaji wa jitihada za imani tofauti ili kuimarisha hisia za umoja miongoni mwa Wakenya.
Alisifu mbinu ya viongozi wa dini kupambana na ukereketwa. "Viongozi wa dini wanaheshimika [katika jamii zao] na miongozo yao, hususani wakati ambao kuna watu wanataka kuanzisha mgawanyiko wa kiimani, ni muhimu sana," alisema.
Chanzo: http://sabahionline.com/



No comments:
Post a Comment