If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, December 12, 2012

RAIS WA ZAMANI WA MADAGASKA MARC RAVALOMANANA AMEKUBARI KURUDI NCHINI KWAKE.

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amefanikiwa kufanya mazungumzo na Rais wa zamani wa Madagaska Marc Ravalomanana ambaye amekubari kurudi nchini kwake baada ya kuwa uhamishoni nchini Afrika Kusini tangu mwaka 2009.

Rais wa zamani wa Madagascar Marc Ravalomanana akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo December 11, 2012,kulia ni Mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Raisi Kikwete amesema Ravalomanana amekubali pia kutokugombea katika uchanguzi utakaofanyika nchini humo mwezi Mei 2013 ili kuleta amani na utulivu.

“Nimezungumza na Rais Ravalomanana na amekubali kurudi nchini kwake madagaska na kukubali kutokukugombea uchaguzi ujao kama maamuzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yalivyofikiwa katika vikao vyake vya hivi karibuni”, amesisitiza Rais Kikwete.

Raisi kikwete amefafanua kuwa Ravalomanana anarudi nchini Madagaska bila masharti yoyote na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo ikisaidiana na Jumuiya ya SADC. Kwa upande wake Rais Ravalomanana amemshukuru Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo na amesema anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na SADC kwa lengo la kuisaidia Madagaska kuwa katika hali ya amani.

“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha mazungumzo haya na niko tayari kurudi nchini kwangu kujenga, kuimarisha na kushirikiana na wananachi ili kuleta amani na utulivu,” amesema Ravalomanana.

Rais kikwete alipewa jukumu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika la kufanya mazungumzo na Marais wote wa wawili, Rais wa sasa wa Madagaska Andry Rajoelina na Rais wa zamani Marc Ravalomanana ambapo mazungumzo bado yanaendelea kwa upande wa Rais Rajoelina.ezi Mei 2013 ili kuleta amani na utulivu.

“Nimezungumza na Rais Ravalomanana na amekubali kurudi nchini kwake madagaska na kukubali kutokukugombea uchaguzi ujao kama maamuzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yalivyofikiwa katika vikao vyake vya hivi karibuni”, amesisitiza Rais Kikwete.

Raisi kikwete amefafanua kuwa Ravalomanana anarudi nchini Madagaska bila masharti yoyote na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo ikisaidiana na Jumuiya ya SADC. Kwa upande wake Rais Ravalomanana amemshukuru Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo na amesema anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na SADC kwa lengo la kuisaidia Madagaska kuwa katika hali ya amani.

“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha mazungumzo haya na niko tayari kurudi nchini kwangu kujenga, kuimarisha na kushirikiana na wananachi ili kuleta amani na utulivu,” amesema Ravalomanana.

Rais kikwete alipewa jukumu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika la kufanya mazungumzo na Marais wote wa wawili, Rais wa sasa wa Madagaska Andry Rajoelina na Rais wa zamani Marc Ravalomanana ambapo mazungumzo bado yanaendelea kwa upande wa Rais Rajoelina.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako