If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, January 2, 2013

Wabunge wapitisha sheria huku Rais Obama akiwahakikishia wananchi watatekeleza yote yaliyoafikiwa


Kizungumkuti juu ya kupita au la kwa sheria ya kuzui kupanda kwa kodi na mpango wa kubana matumizi ya fedha nchini Marekani kimepata ufumbuzi baada ya wabunge wengi kupiga kura ya kupitisha sheria hizo na kumaliza hali hiyo ya sintofahamu.

Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na Makamu wa Rais Joe Biden punde baada ya Baraza la Seneti kupitisha sheria zilizonusuru bajeti ya nchi hiyo

Wabunge nchini Marekani wamekuwa kwenye mvutano mkali punde tu baada ya kumalizika kwa sherehe za Noeli na kuwalazimu kurejea haraka kuendelea na mchakato wa kupitishwa kwa sheria hizo ili kunusuru bajeti ya serikali.

Wasiwasi mkubwa ulikuwa umetanda kutokana na pande mbili zenye wabunge wengi Republican na Democrats kutunishiana misuli kutokana na kila upande kushikilia msimamo wake hatua ambayo imeliingiza taifa hilo kwenye hofu ya kutetereka kiuchumi.

Makamu wa Rais Joe Biden ndiye ambaye ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuhakikisha ananusuru upitishwaji wa sheria hizo baada ya kukutana na Wabunge wa Republican ambao walikubali kuweka tofauti zao na Democrats kando na kuangalia maslahi ya Umma.

Congress imepitisha sheria hizo baada ya hapo awali Bunge la Seneti kuridhia hatua kama hiyo kwa kupiga kura za ndiyo 257 dhidi ya kura za hapana 167 na hivyo kuonesha mwelekeo mwema.

Licha ya kupitishwa kwa sheria hizo lakini kumekuwa na mfarakano wa kisiasa huku wabunge wa Chama Cha Republican wakitaka marekebisho kadhaa yafanyike ili sheria hizo ziwe na manufaa kwa wananchi.

Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kufurahishwa na hatua ambayo imefanywa na wabunge wa nchi hizi na kuahidi atasaini sheria hiyo ambayo itaongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa asilimia mbili kwa matajiri.


Obama anasema sheria hiyo itasaidia wananchi wenye uwezo wa kati na mdogo kuweza kuishi vizuri kutokana na kutobanwa sana na mzigo mkubwa wa kodi kama ambavyo ilivyo kwa sasa hali inayowafanya wazidi kuwa tegemezi.

1 comment:

Maoni yako