If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, February 26, 2013

Al-Shabaab hawawezi 'kukimbia ukweli' wakati hadithi za al-Amriki zinaendelea

Boniface Bosire alichangia katika habari hii kutoka Nairobi

Waraka uliotolewa tarehe 18 Februari na Wandishi asiyejulikana akidai ana mahusiano na al-Shabaab ni ushahidi zaidi kwamba saga linaloendelea kumhusu mwanamgambo mzaliwa wa Marekani Omar Hammami ni tishio baya -- kama sio hatari -- kwa uongozi wa al-Shabaab.

Waraka mpya wenye ukurasa 17 ndio jaribio pana zaidi la al-Shabaab kumkataa na kumtenga mwanajihadi mzaliwa wa Marekani Omar Hammami. [Jalada]

Waraka huo wa ukurasa 17 wenye kicha cha habari "Kukimbia ukweli hakuwezi kulifanya litoweke: Kufisha hadithi ya Abu Mansour", ni jaribio pana la kuwaaibisha na kuwatenga wafuasi wa Hammami, anayejulikana pia kama Abu Mansour al-Amriki, kwa kushambulia utu wake, inia na dhamira yake katika jihadi.

"Wakati na fedha vinatumiwa kupunguza hasara ambayo tayari imeshafanyika na mpasuko uliopo [miongoni mwa al-Shabaab]," alisema Samson Omusula, mshauri wa masuala ya usalama aliyeko Nairobi, na kuongeza kuwa kikundi cha wanamgambo hakipotezi juhudi yoyote katika kufikia umma wa wasomaji ulioenea.

"[Waraka huu] ni jaribio [la la-Shabaab] kujionyesha wenyewe kama kikundi chenye wasiwasi na matatizo ya kifedha na wafuasi ambao hawakuungana," aliiambia Sabahi.

Masuala madogo yanayojulikana kuhusu mtu anayedaiwa kuandika huu waraka, Abu Hamza al-Muhajir, kuliko kile kilichomo ndani yake.

Waraka huu, ambao umeandikwa kwa Kiingereza cha mitaani na kutolewa na picha za kuvutia, nukuu za kuvuta, mfumo rahisi wa kidijitali, unamwonyesha mwandishi kama mtu wa Magharibi katika juhudi za kuwashawishi wasomaji kwamba yeye na wapiganaji wengine wa kigeni hawako pamoja na kutoridhika kwa al-Amriki kwa Uongozi wa al-Shabaab.

Hata hivyo, ushahidi unaonyesha uwezekano mkubwa kwamba kwa kweli al-Muhajir ni mwanachama wa Somalia wa al-Shabaab.


Namna na hisia ambazo waraka unamfafanua al-Amriki -- "mtu mweupe, kijana na mkarimu" aliyesafiri kwenda Afrika "kuiwezesha jamii iliyoko nyuma katika kuanzisha utawala wa taifa la Kiislamu" kwa "kulazimisha matakwa yake kwa....washenzi" -- kunazua hisia za wenyeji na mitizamo ya kikoloni ya miaka iliyopita.

Kwa kweli, Omusula alisema mwandishi au waandishi wanaweza kuwa watu hao hao wanaoshughulikia akaunti ya Twitter ya al-Shabaab. "Watu walewale wanaweza kujionyesha kama wapiganaji tofauti ambao wanamuunga mkono Abu al-Zubayr ili kujenga mwelekeo kwamba anafurahia kuungwa mkono sana," alisema, wakikusudia Mukhtar Abu al-Zubayr, kiongozi wa al-Shabaab anayejulikana pia kama Ahmed Godane.

"Wamefahamu kuwa sauti ile ile dhidi ya Hammami haijawashawishi wapiganaji wa kigeni, kwa hivyo wanajenga nyuso tofauti ili kuonyesha uungwaji mkono usiokuwepo," Omusula alisema. "Sitoshangazwa [kuona] makala nyingine ikifuatia karibuni ya mwandishi yule yule anayejificha chini ya jina jingine kama jaribio la kuonesha utofauti."

Hadithi ya Al-Amriki yapenyeza kwenye vyeo vya ndani vya al-Shabaab
Kuongezeka kwa ushahidi wa sehemu kubwa kunashiria kuwa hadithi ya al-Amriki imepenyeza maaskari ya al-Shabaab, na kwamba uongozi wa vikundi vya wanamgambo hawa umeendelea kukata tamaa zaidi ya kuondoa uoga na wasiwasi kutoenea.

Katika jaribio la hivi karibuni la kuaibisha al-Amriki, waraka ulianza na kisa kuhusu "Mwarabu muhajir mwandamizi" akitoa mahubiri kwa kundi kubwa la mujahidina na wakazi wa eneo hilo kwenye msikiti huko Barawe katika mkoa wa Shabelle ya chini ya Somalia.

Kutoka "suala la Abu Mansour [lilikuwa] bado linazungumziwa kuhusu mzunguko wa mujahidina", mwanamgambo wa kiwango cha uandamizi alielekeza mahubiri yake kwenye uhusiano kati ya ansar (wapiganaji wa ndani) na muhajireen (wapiganaji wa nje) -- suala ambalo hivi karibuni liliwakera al-Shabaab kwa miezi kadhaa.

Baada ya kulaumu al-Amriki na wafuasi wake kwa kuwa "ahlul kalaam [watu wa mazungumzo ya kubweteka]" kuliko ukamilifu wa kijihadi "ahlul qital [watu wa kupambana]", wanamgambo hao waliendelea mbele zaidi kuifanya ionekane kana kwamba hakuna mgawanyo uliopo kati ya viongozi wa Kisomali wa ndani na wapiganaji wageni.

"Kwa jina la Allah, nimetoa ahadi yangu [ahadi ya utii] kwa shekhe Abu Zubayr mimi binafsi na kuanzia sasa kutoka kwenye mimbari hii ninatamani kuwahakikishia umma ahadi yangu kwake na kutamka wazi, siyo mimi mwenyewe, lakini kwa niaba ya muhajireen, kwamba bado tuko imara kwenye ahadi zetu, na kwamba bado hatujaziacha," Arab muhajir mwandamizi aliiambia hadhira.

Mshauri mwelekezi wa usalama ambaye makao yake yako Nairobi na Meja mstaafu wa jeshi Wilberforce Onchiri aliiambia Sabahi kwamba al-Shabaab imekata tamaa kuwa na wapiganaji wote wanaoapa kuwa watii kwa al-Zubayr katika hatua ya kuongezeka kwa waasi na wasiwasi.

"Al-Shabaab ina wasiwasi wa kuongezeka kwa maasi na kutoaminiana," Onchiri alisema. "Haitashangaza kuwa al-Zubayr mwenyewe ameidhinisha kutolewa kwa nyaraka za kupunguza uoga unaongezeka kwenye akili za wapiganaji wa nje ndani na nje ya Somalia."

Onchiri aliongezea kwamba majaribio ya al-Shabaab yanaonyesha kawaida katika vyeo vyake, mgogoro kati ya wapiganaji wa ndani na nje ni wa kweli.

Zaidi ya hayo, mwandishi amekiri kuwa uhalali wa utolewaji wa waraka huu ni jaribio la kuondoa mgawanyo unaoendelea ndani ya kikundi chenye mfungamano cha al-Qaeda.

Al-Mujahir anasema sababu yake kufanya hivyo ni "kufichua hadithi za Abu Mansur kwa wafuasi wote wa mujahidina ili kutuliza hofu zao na kufafanua wasiwasi wao."

"Bila ya dharura ya taarifa zozote zaidi kuhusu hadithi zinazokua," aliendelea, "Simulizi za Abu Mansur, kwa hakika zinaonekana kukubalika kiasi cha kutosha kupata nafasi katika mioyo ya wenye nia njema na mashabiki wa jihadi duniani kote."

David Ochami, mwandishi wa habari kutoka Mombasa anayefuatilia shughuli za vikundi vya wanamgambo Mashariki ya Kati na Pembe ya Afrika, alisema waraka huo ni ishara kwamba wapiganaji wa al-Shabaab wanalifuatilia kwa makini suala la al-Amriki , na sio malengo yaliyoelezwa na viongozi wao.

"Baada ya kutupilia mbali suala hilo na kutarajia kuwa litaisha, al-Shabaab sasa inashurutisha kutoa tamko kwa sababu ya kuongezeka kwa hadhi ya Hammami," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba suala hilo linaonekana kukwepa uzingativu wa kazi ya kikundi ya kusambaza hofu.

"Ni wazi kwamba genge la waasi liko karibu na al-Shabaab hawatatoa kauli hizo kama hawafikirii uongozi wao unatishiwa," alisema.

Habari mpya katika mlolongo wa majaribio ya kumuaibisha al-Amriki
Ujumbe ndani ya waraka wa ukurasa 17 hauna lolote jipya. Kwa miezi kadhaa, al-Shabaab na washirika wake wamekuwa wakijaribu kumtweza al-Amriki na wafuasi wake.

Tarehe 17 Disemba, katika taarifa ya nadra kwa vyombo vya habari, al-Shabaab ilimkana al-Amriki na wafuasi wake mbele ya maswali yaliyoibuka kutoka kwa askari.

Katika taarifa yake al-Shabaab ilitamka kwamba "Abu Mansour al-Amriki, kwa namna yoyote, hawakilishi mawazo ya muhajireen nchini Somalia … Maoni yaliyotolewa na Abu Mansour, tuhuma za mgongano na utoaji wa video ni matokeo tu ya malalamiko binafsi ambayo yanatokana na kujipendelea kupata umaarufu na hayafikii hali halisi iliyopo."

Kauli ya kikundi cha wanamgambo ilikuja baada ya video mbili zenye maelezo ya hali ya juu zikimuonyesha al-Amriki ziliwekwa kwenye intaneti.

Katika video iliyotolewa Machi, alisema maisha yake yako hatarini kwa wanachama wenzake wa al-Shabaab "kutokana na kutofautiana kulikotokea kati yetu kuhusiana na masuala ya sharia na masuala ya mkakati". Katika video ya Oktoba, aliwaomba viongozi wa jihad duniani kuingilia kati "hali ya sasa ya kutisha ambayo inaimaliza" al-Shabaab na harakati za wapiganaji wa kigeni.

Wiki chache baadaye, al-Amriki walituhumiwa kutoa video nyingine na baadhi ya nyaraka zilizoambatana zayo, safari hii utetezi wa shekhe asiyejulikana, anayeaminika kuwa ni kiongozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri, aliingilia kati na kuwaokoa wapiganaji wa kigeni mikononi mwa al-Shabaab.

"Pamoja na propaganda kutoka kwa baadhi ya Wasomali kwamba wapo katika mapambano na jihadi ya kidunia, vitendo vyao vya zamani na vya sasa vinaashiria kwamba wanachokitaka ni kazi za nje kwa matumizi ya wenyeji," mojawapo wa waraka ulioelezwa. "Japokuwa kuna uvumi kwamba wanafuata mawazo ya al-Qaeda, wakati wao ndiyo waliowafukuza al-Qaeda nchini Somalia."

Isipotosha, Kituo cha Vijana wa Kiislamu (MYC), kikundi kinachohusishwa na al-Shabaab nchini Kenya, kilishurutishwa kujiunga na tatizo hilo kwa sababu asasi "imepokea maswali mengi kuhusu hali ya Abu Mansour al-Amriki", kwa mujibu wa taarifa yake ya tarehe 12 Januari katika vyombo vya habari.

Kwa kukusudia la kupotosha wapiganaji wengine ambao "wanatafuta kushindana na" al-Amriki, waraka ulieleza "jihadi kamwe haitahusu sura ya mtu mmoja lakini ni sura ya pamoja ya mujahideen".

MYC yatuma ujumbe wa kuonyesha kuongezeka kwa wasiwasi
Wiki za hivi karibuni, ujumbe kutoka katika akaunti ya Twitter ya MYC ulionyesha hadharani kiwango cha kukua kwa mvutano kati ya wanajihadi mkoani.

Tarehe 20 Februari, MYC walionekana wakitambua jinsi uharibifu wa hadithi ya al-Amriki kwa umma ulivyotokea. "Tunajisikia kwamba kuweka matatizo yetu ndani ni njia nzuri zaidi. Kwa nini tunataka makafiri watucheke?"

Siku tatu baadaye, hisia za ujumbe wa MYC ulianza kupata upinzani zaidi.

"Mwishowe kama mtu yeyote hawafurahii Al Shabaab & AQ ni uamuzi wako: "endelea na makafiri" au "NYAMAZA KIMYA"!!!!!" kikundi hicho kilituma tarehe 23 Februari, kufuatia mfululizo wa ujumbe kutoka kwa idadi kubwa ya watuhumiwa wa wasiokuwa na maudhui ya jihadi katika eneo, inawezekana wakawa Abu M (@abumamerican), akaunti ya Twitter ilikubalika kwa upana kama ile ya al-Amriki.

Siku hiyohiyo, MYC ilizungumza na kiongozi wa al-Shabaab al-Zubayr. "Baadhi wanajisikia shauku kuhusu al-Zubayr wakati wengine hawamuheshimu...," katika urejeleaji wa kawaida kwa al-Amriki na wapiganaji wengine wa kigeni wakiwa na pinga uongozi wa al-Shabaab.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako