If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Sunday, February 10, 2013

Makundi ya haki za kibinadamu yaonya kuhusu hatari ya vurugu za hali ya juu katika uchaguzi wa Kenya

Hatari ya vurugu za kisiasa nchini Kenya ni "kubwa sana" kuelekea uchaguzi wa mwezi ujao, Human Rights Watch (HRW) ilionya katika ripoti iliyotolewa siku ya Alhamisi (tarehe 7 Februari).

Jeshi la Kenya likifanya doria mitaani mjini Nairobi tarehe 29 Mei 2012, siku moja baada ya dazeni ya watu kujeruhiwa katika shambulio la bomu. [Picha ya Simon Maina/AFP]

Ripoti ya kurasa 58 kikundi hicho, "Hatari Kubwa: Vurugu za Kisiasa na Uchaguzi wa Kenya 2013", inasema uhaba wa maendeleo ya serikali ya Kenya juu ya mageuzi iliyoahidi na kushindwa kushughulikia ukiukwaji wa haki za kibinadamu zinaoendelea na uliopita vimechangia kuzua mivutano Kenya yote kabla ya uchaguzi mkuu wa tarehe 4 Machi.

Ripoti ya HRW imetokana na kuwasaili watu 225 Kenya nzima, kukiwa na wengi zaidi katika mikoa ya Kati, Pwani, Mashariki, Kaskazini Mashariki, Nyanza na Bonde la Ufa.

Ripoti hiyo inapendekeza kwamba viongozi wa Kenya wachukue hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwashtaki kwa haki wale wanaohusika moja kwa moja katika kuchochea au kuandaa vurugu, ili kuhakikisha ufanyikaji wa uchaguzi wa amani na haki.

"Vurugu haziepukiki, lakini ishara za tahadhari ziko wazi sana kiasi cha kutostahiki kupuuzwa," alisema Mkurugenzi wa HRW Afrika Daniel Bekele. "Serikali imeshindwa kushughulikia sababu za vurugu ambazo zimezikumba chaguzi za vyama vingi tangu mwaka 1992, na hasa mauaji ya 2007-2008, kwa hivyo hatua za haraka zinahitajika ili kuwalinda Wakenya."

Kiasi cha watu 1,200 waliuawa na kiasi cha 300,000 kukimbia makazi yao wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.


Ripoti inataja mambo ya kawaida Kenya yote kuwa ni: serikali kutokuwa na ari, mfumo wa sheria, na mamlaka mengine kufanya mageuzi ya vikosi vya usalama, kushughulikia ufisadi, kuvunja vigenge vya wahalifu, na kuwawajibisha wale wanaohusika na vurugu. Inasema kuwa, "hali inayokaribia kutojali kabisa sheria" kwa vurugu ambazo zilitokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 imewaacha huru watu waliofanya uhalifu ule kufanya uhalifu mwengine.

"Wahanga wa vurugu wanahisi kuwa haki imewapitia upande, na watu waliosababisha vurugu zile wanahisi wanalindwa dhidi ya sheria," Bekele alisema. "Huu ni mchanganyiko wa hatari sana kwa uchaguzi unaokaribia."

Ripoti nyengine iliyotolewa tarehe 30 Januari na shirika la kimataifa la haki za kibinadamu Amnesty International ilitoa madai kama hayo.

Ripoti hiyo,"Mageuzi ya Polisi Kenya: Tone moja katika Bahari Kuu"; inataja matukio kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi wakizilenga jamii maalumu, na inadai kwamba serikali ya Kenya imefanya machache ili kuwawajibisha maafisa wa polisi wanaohusika.

"Moja ya mfano unaoonekana kwa wingi ni kuwa ongezeko la ubaguzi wa kipolisi na unyanyasaji wa watu wenye asili ya Somalia nchini kote, nchi ikiwa inakumbwa na kukua kwa ubaguzi wa wageni nchini," ripoti ilisema.

Polisi pia wameshindwa kuzuia mashambulizi mfululizo ya Tana River Delta, jambo linalozua "wasiwasi mkubwa kuhusu utekelezaji wa vikosi vya usalama katika hali kama hizo na uwezo wao wa kulinda haki za binadamu za watu wa Tana," kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Kikundi hicho kilionya kwamba kushindwa kwa mageuzi ya polisi kutamaanisha kuwa mfumo ule ule wa polisi uliotumika tangu uchaguzi wa mwaka 2007 ndio pia utakaokuwa na dhamana ya usalama katika uchaguzi ujao.

Mivutano inaizunguka kesi ya ICC
Ripoti ya HRW ilisema kuwa mivutano imekuwa ikiongezwa na kesi inayokuja ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inayowahusu mgombea wa urais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza mwenzake William Ruto kwa madai ya nafasi yao katika kuandaa vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Kesi hiyo, iliyopangwa kuanza tarehe 11 Aprili, inaweza kugongana na duru ya pili ya uchaguzi wa urais, utakaofanywa ndani ya mwezi ikiwa mgombea atashindwa kupata jumla ya asilimia 51 ya kura zote katika duru ya kwanza.

Msaidizi wa Wizara ya Nchi kwa Masuala ya Afrika Johnnie Carson siku ya Alhamisi aliwaonya Wakenya kuwa "uteuzi una matatizo yake", kama tahadhari ya wazi juu ya uwezekano wa ushindi wa Kenyatta na Ruto, kwa mujibu wa gazeti la The Standard la Kenya.

"Wakenya wanapaswa kujua kwamba watu binafsi wana heshima na pichwa zilizomo katika historia yao na lazima wawe na tahadhari dhidi ya kufanya maamuzi yanayoweza kuathiri kwa njia hasi kwa uchumi wa taifa na mikoa," alisema.

Mwezi wa Disemba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwaonya Wakenya kutochagua viongozi wanaokabiliwa na mashtaka huko ICC, na kusema hatua hiyo inaweza kuathiri mahusiano ya Kenya na nchi za nje.


No comments:

Post a Comment

Maoni yako