If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, March 13, 2013

Somalia yakabiliwa na changamoto mpya, fursa za kurahisishwa kikwazo cha silaha

Na Majid Ahmed, Mogadishu

Mwaka mmoja wa kulegezwa kwa kikwazo cha silaha kwa Somalia na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaiwezesha serikali kununua silaha nyepesi nyepesi kwa ajili ya vita vyake dhidi ya al-Shabaab, lakini baadhi ya wachambuzi wanaonya kuwa kwa kufunguliwa kwa njia ya silaha kunaweza kuruhusu silaha kuishia katika mikono isiyotakiwa.

Chini ya Azimio 2093 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) itaendelea kubakia huko hadi mwezi Februari 2014. [Na Stuart Price/AU-UN IST/AFP]

Azimio nambari 2093 linairuhusu Somalia kununua silaha zenye ukubwa wa mwisho wa kipenyo cha milimita 12.7. Azimio pia linarefusha mamlaka ya jeshi la askari 17,000 la Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) hadi tarehe 28 Februari, 2014.

Katika azimio hilo, serikali ya Somalia lazima itoe siku tano za taarifa kwa kamati inayoshughulikia na usimamizi wa vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa kuhusu uingiaji wa shehena wa silaha nyepesi. Somali pia lazima itoe ripoti kila baada ya miezi sita juu ya mpango wake wa kuhakikisha utunzaji salama wa silaha hizo.

Ulinzi

Mwanachama wa Brigedi ya Ras Kamboni ambayo inaiunga mkono serikali akinyanyua bunduki nzito aina ya mashine akiwa amepanda nyuma ya gari ya mzigo huko Kismayo mwezi Oktoba 2012. [Na Stuart Price/AU-UN IST/AFP]

"Hatua hii ya kulegeza kikwazo cha silaha kilichowekewa Somalia ni mafanikio makubwa kwa watu na serikali ya Somalia, na inaonyesha hatua chanya katika kipengele cha imani ya jumuiya ya kimataifa kwa serikali mpya ya Somalia," alisema Waziri wa Ulinzi wa Somalia Abdihakim Haji Mohamud Fiqi.

Fiqi alisisitiza kuwa kulegezwa kwa kikwazo kutaisaidia serikali ya Somalia kutimiza lengo lake kuu la kuwavunjavunja al-Shabaab. "Kwa vile sasa kikwazo kimelegezwa, serikali ya Somalia inayo nafasi ya kununua silaha nyepesi kwa dhamiri ya kuimarisha usalama wa vikosi vyake na kuviwezesha kufanya kazi zao za ulinzi kwa ufanisi zaidi," aliiambia Sabahi.



"Napenda kuthibitisha kuwa serikali ya Somalia ina nia ya kutekeleza masharti yaliyowekwa na azimio la Baraza la Usalama katika hali ya uwazi, na pia ninataka kuwaambia watu wa Somalia kuwa fursa hii iliyopatikana kwa serikali yao haitakuwa tishio kwa maisha ya raia, na silaha hazitatumiwa vibaya," Fiqi alisema.

"Somalia ni sawa na nchi nyingine duniani ambayo inahitaji silaha kwa jeshi lake la taifa na kutumia jeshi halali kwa kulinda uhuru wake kutetea ardhi yake," alisema.

Matokeo yasiyotarajiwa
Mapema mwaka huu, Shirika la Amnesty International lilitahadharisha kwamba kuondoshwa kwa kikwazo cha silaha kwa Somalia kunaweza kuziingiza silaha katika mikono ya al-Shabaab, na bila ya ulinzi unaofaa, uhamishaji wa silaha unaweza kuharibu zaidi hali ya kibinadamu.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na usalama pia wanaonya kwamba bila ya ulinzi kama huo, kulegezwa kwa kikwazo kutaongeza hali ya kutokuwepo kwa usalama katika kanda hii.

"Ikiwa hatua za kufaa za kuhakikisha matumizi mazuri ya silaha hazikuzingatiwa na manunuzi ya silaha hayakufanywa pamoja na mataifa katika kanda, uondoshwaji huu wa kikwazo cha silaha unaweza kuifanya hali kuwa tete zaidi," alisema Mohamed Hassan Abdi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa aliyeko Galkayo.

Tawala za kanda kama vile Puntland na Somaliland zinaweza kugeukia soko haramu ili kupata aina ya silaha kama hizo zitakazonululiwa na serikali ya shirikisho chini ya suluhisho la Umoja wa Mataifa, aliiambia Sabahi. Kwa upande mwingine, "inaweza kupelekea mashindano mapya ya silaha nchini Somalia ambayo yanaweza kuchochea mizozo mipya baina ya Mogadishu na tawala za kanda zilizotajwa kabla," alisema.

"Wasiwasi uliotajwa na viongozi wa Puntland na Somaliland ni halali kwa sababu wana woga wa kwamba serikali ya shirikisho inaweza kuzitumia silaha hizo kwa kuiunganisha nchi kwa nguvu, na pia kuna woga mwingine wa silaha kuweza kuangukia katika mikono isiyotakiwa -- hasa kwa vikundi vyenye siasa kali vyenye mafungamano na al-Qaeda na wanamgambo wa kikabila," alisema.

Kusambaa kwa silaha kwatia wasiwasi
Mwanajeshi mstaafu Kanali Abdishakur Ahmed alisema Somalia haihitaji silaha zaidi. Badala yake, alisema, serikali inapaswa kuzingatia unyanyang'anyaji wa silaha kwa wanamgambo wa makabila na vikundi vingine vinavyotumia silaha.

"Katika nchi kama vile Somalia ambayo imevurugwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, migogoro ya kikabila na wingi wa silaha, hakuhitajiki silaha zaidi kwa sasa," Ahmed aliiambia Sabahi. "Nchini, kusambaa kwa silaha katika mikono ya wananchi kunatia wasiwasi sana."

Alisema vikosi vya serikali bado haviwakilishi Somalia kikamilifu, kwani vikosi vyao vinajumuisha watu wenye uaminifu wa kikabila ambao bado unahitaji kuhusishwa katika jeshi la taifa.

"Kuna wanamgambo wa kikabila ambao wanatawala baadhi ya maeneo ya nchi, kama vile Brigedi ya Ras Kamboni huko Kismayu na Ahlu Sunna wal Jamaa huko Galgaduud. Hao hao wanakwenda katika mikoa ya Hiran na Bay ambako vikosi vya wanajeshi vinatawaliwa na baadhi ya sheria za makabila," alisema Ahmed.

"Pamoja na jitihada zilizofanywa na serikali ya Somali kuijenga upya vikosi vya jeshi lake la taifa, ukweli ni kwamba vikosi vya taifa bado haviwakilishi maeneo tofauti na mikoa ya Somalia ili waweze kutambuliwa kwa urahisi kama vikosi vya taifa," alisema.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako