If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, March 2, 2013

Viongozi wa dini Tanzania wataka uvumilivu baada ya ghasia ya kidini

Na Deodatus Balile, Dar es Salaam

Viongozi wa dini nchini Tanzania wamelaani wimbi lililoibuka hivi karibuni la machafuko yanayotokana na tofauti za kiimani kati ya Wakristo na Waislamu ambayo tayari yameshasababisha vifo vya viongozi watatu katika kipindi cha mwezi Februari, na kuapa kuzirejesha jamii hizi mbili katika hali ya kawaida.

Baadhi za viongozi hao wanasema kuwa mahubiri yanayotelewa bila kuwa na kibali husika kwenye makanisa na misikiti ndio kiini cha hali ya mtafaruku inayoendelea sasa. Juu, wanaume wakifanya ibada msikitini jijini Dar es Salaam. [Na Mwanzo Millinga/AFP]

Tarehe 11 Februari, mzozo kati ya wafuasi wa dini hizo mbili juu ya nani anafaa kuchinja nyama ulisababisha kifo cha mchungaji Mathayo Machila aliyekuwa na umri wa miaka 45 na kusababisha wananchi wengine kujeruhiwa. Tangu wakati huo serikali imeanzisha kamati ya viongozi wa dini kwa lengo la kurejerea sheria za kiimani kuhusu kuchinja mifugo mbalimbali kwa ajili ya nyama.

Visiwani Zanzibar, Mchungaji Evarist Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya kanisa lake tarehe 17 Februari, wakati pia tarehe 23 Februari Sheikh Ali Khamis Ali, 65, aliuawa na watu wasiojulikana kwenye shamba lake la minazi.

Mauwaji hayo ya mwezi Februari ni mwendelezo wa matukio yaliyoanza mwaka uliopita. Katika sherehe za Krismasi, watu waliokuwa na silaha walimshambulia kwa risasi Mchungaji Ambrose Mkenda wakati alipokuwa njiani akirejea nyumbani, na mwezi Novemba watu wasiojulikana walimshambulia kwa kumwagia tindikali Sheikh Fadhil Soraga.

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Bin Shaaban Simba, amesema kuwa nchi inatakiwa kuhamasisha uvumilivu wa kidini.

"Tumekuwa tukivumiliana kwa muda mrefu lakini sasa uvumilivu huo umekwenda wapi?" aliiambia Sabahi. "Serikali, viongozi wa dini na wanasiasa wanapaswa kuhubiri amani, upendo na utulivu."


Alisema kuwa Tanzania inapaswa kuzuia hali hiyo kuendelea kwa sababu inaweza kuipeleka nchi katika machafuko makubwa, na kuongeza kuwa polisi wanapaswa kuchunguza matukio ya uhalifu na wahusika ni lazima wafikishwe mbele ya mahakama.

Mchungaji msaidizi wa Dayosisi ya Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa amesema kuwa baadhi ya watu serikalini wameshindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo, na kusababisha machafuko hayo.

Alisema kuwa baadhi ya viongozi wana udhaifu katika kuzisimamia sheria, kanuni na taratibu jambo ambalo limetoa mwanya kwa baadhi ya watu kuzua machafuko. "Suluhu iliyobakia ni kusimamia utekelezwaji wa sheria," aliiambia Sabahi.

Simba alisema viongozi wa dini zote mbili wameshirikiana kuunda Jukwaa la Amani la wajumbe 10 iliyopewa jukumu la kupunguza tafauti baina ya jamii hizo mbili. Taasisi hiyo iliyoundwa na dini hizo mbili itashughulikia masuala yanayozikabili dini hizo nchini na inadhamiria kusaidia hatua za serikali kuhusiana na ghasia za hivi karibuni.

Raia watetea umoja
Yusufu Halimoja, 79, ambaye ni mwalimu mstaafu wa sekondari, aliiambia Sabahi kwamba siasa na uongozi mbaya ndio sababu kuu za ghasia nchini.

" Taifa letu liko kwenye mtihani mkubwa," aliiambia Sabahi. "Nadhani baadhi ya viongozi wanahusika na ghasia hizi kushinikiza ajenda yao ya kuitoa Zanzibar kwenye muungano. Hizi ni siasa mbovu."

Halimoja alisema viongozi wakuu wa serikali hawafanyi ya kutosha kulaani ghasia hizo hadharani, na lazima wafanye mikutano ya hadhara.

Salum Said Hamad, 46, mkaazi wa Mchambawima Zanzibar, alisema mahubiri yasiyo na mwongozo kutoka makanisani na misikitini ndio chanzo cha migogoro ya sasa.

"Dhamira yao ni michango (ya kifedha)," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba viongozi wengi wa kidini wako tayari kuiacha nchi kuingia kwenye machafuko ili kuvutia wafuasi zaidi na kuomba michango.

"Wakati mwengine mimi husikiliza wanachohubiri na kuishia kusikitika. Tunapaswa kurudi kwenye ukweli halisi na ikibidi hata kuwachunguza viongozi wetu wa kidini wanaotoa mahubiri," alisema.

Alisema viongozi wa Kiislamu na Kikristo lazima wahubiri "umoja, amani, upendo, uvumilivu na utulivu," lakini kwa kawaida mambo huwa sivyo.

Honest Ngowi, mhadhiri wa uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Mzumbe, aliiambia Sabahi kwamba pengo kati ya matajiri na masikini nchini Tanzania linazidi kuongezeka na linaweza kuwa chanzo cha migogoro.

"Hebu serikali ijenge mifumo inayofanya kazi kwa maana ya elimu na uchumi, na haya yote (ghasia) yataondoka," aliiambia Sabahi.

Ngowi alisema pale tu watu wanapojishughulisha na kupata kipato chao, hawatakuwa tena na muda wa kujihusisha na ghasia.

Serikali yachukuwa hadhari
Kamishna wa Polisi wa Zanzibar Mussa Ali Mussa alisema polisi wanafanya uchunguzi wa kina dhidi ya ghasia hizo.

"Hatuna hakika kuhusu sababu za ghasia na mauaji," aliiambia Sabahi. "Tumejipanga vyema, tumewaomba marafiki zetu, wa ndani ya nchi na wa kimataifa, kutusadia kwenye hili."

Mussa alisema polisi hawatovunja haki za binadamu, lakini pia hawataacha kuchukua hatua yoyote ile kuwakamata wachochezi wa ghasia.

Waziri wa Mahusiano ya Kijamii na Uratibu Stephen Wassira aliiambia Sabahi kwamba serikali inafuatilia kwa karibu ghasia hizo na itawashughulikia wahalifu wanaoficha matendo yao kwa hisia za kidini.

Wassira alisema kuibuka kwa mauaji ya viongozi wa kidini kumeilazimisha serikali kujihusisha na msako wa kina wa sababu na uwezekano wa suluhisho la ghasia hizo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako