If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, April 19, 2013

Kitengo cha kukabili ugaidi kuwasili mitaa ya Mogadishu

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Serikali ya shirikisho ya Somalia imeunda na kukipa mafunzo kikosi maalumu cha askari kufanya operesheni dhidi ya ugaidi huko Mogadishu na kuzuia mipango ya al-Shabaab ya kulipua mabomu ya kujitoa muhanga kwa siku zijazo.

Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia wakitembea wakati wa gwaride la jeshi tarehe 14 Aprili huko Mogadishu. Serikali ya shirikisho inaandaa kikosi maalum imara 1,000 waliopewa mafunzo kwa ajili ya operesheni dhidi ya ugaidi kusambazwa katika mji mkuu huo. [Na Stuart Price/AU-UN IST PHOTO/AFP]

Serikali inapanga kusambaza kikosi imara 1,000 ifikapo mwishoni mwa Aprili, kitakachojumuisha vikosi kutoka matawi kadhaa ya vikosi vya jeshi na vikosi vya usalama kwa mujibu wa Mohamud Ahmed Hirsi, meneja katika idara ya ugavi na usafirishaji wa watu na vitu wa Jeshi la Ulinzi la Somalia.

Kikosi hiki kitabomoa na kuharibu ngome za ugaidi na maficho, kuondoa kabisa operesheni zao na kutegua mabomu, katika jitihada za kurejesha amani na kanuni katika mji mkuu.

"Vikosi hivi vinawajibika kutafuta magaidi na wale wanaotuhumiwa kujihusisha katika operesheni za uuaji kwa sababu za kisiasa dhidi ya wahamasishaji amani, waandishi wa habari, polisi na maofisa wa jeshi," Hirsi aliiambia Sabahi. "Miongoni mwa malengo yake ni kushambulia vikundi vya kigaidi ambavyo vinafanya mauaji, wizi na kuiba mapato, pamoja na kuingilia mali binafsi, taasisi za serikali na migahawa."

Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia wakishiriki katika mazoezi ya mafunzo tarehe 28 Machi katika kambi ya mafunzo ya Jazeera huko Mogadishu, mahali ambapo wakufunzi wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia wanaendesha vikosi vya Somalia kwa njia ya upangaji mpana wa ufundishaji askari na mbinu za kijeshi. [Na Tobin Jones/AU-UN IST PHOTO/AFP]

Baadhi ya vikosi kutoka katika kikosi kipya vitafanya doria kwenye maeneo ya mji ambako waasi wamejulikana kujificha, vikitekeleza hatua kali za ulinzi, Hirsi alisema. 

Vikosi vingine vitalinda usalama wa vituo vya ukaguzi vya kando ya barabara mahali pengine popote katika mji mkuu wakiwataka waendesha magari na pikipiki kuonyesha vitambulisho na kukabidhi magari yao kwa ukaguzi wa usalama.


Al-Shabaab walikiri kuhusika na kuongezeka kwa utupaji mabomu ya mauaji makubwa na shambulio la bomu katika gari huko Mogadishu wiki za hivi karibuni. Kikundi cha wanamgambo pia kimekuwa kikihusika katika majaribio kadhaa ya mauaji, ikiwa ni pamoja na moja la tarehe 8 Aprili ambapo Sheikh Bashir Ahmed Salad, mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu la Somalia, alinusurika baada ya bomu kulipuka kwenye gari lake.

namo tarehe 18 Aprili, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitembelea kwenye Kambi ya Mafunzo ya Jazeera karibu na Mogadishu, ambako wanachama wa kikosi kipya wanapata mafunzo.

Kuwepo kwa kikosi huko Mogadishu kutaimarisha serikali ya shirikisho ya Somalia katika kupambana na vitisho vya al-Qaeda na vikundi washirika wake, pamoja na kuleta amani na ustawi kwa Somalia, Mohamud alisema.

"Inanipa fahari kubwa kuona nyuso zenu," aliwaambia wanachama wa kikosi maalumu. "Nyie ni mustakabali wa Somalia kwa sababu mmehudhuria mafunzo haya kutokana na maadili yenu ya hali ya juu, kwa kuwa hamkujihusisha na kutafuna mirungi, kuvuta sigara, kutumia madawa ya kulevya au kunywa pombe."

"Jeshi letu la maadili, tupo pamoja nanyi. Mmebeba silaha zenu, mkiitetea nchi yenu dhidi ya adui magaidi," Mohamud alisema. "Ninawaomba muwe na umoja ili tuweze kurejesha amani na utulivu katika mji mkuu."

Wizara ya Ulinzi bado haijatenga bajeti kwa kikosi hiki maalumu, Hirsi alisema. Ili serikali ianzishe mashambulizi ya mjini dhidi ya al-Shabaab huko Mogadishu, fedha zinahitajika kununua sare, helikopta, vifaa vya majini, boti ziendazo kasi, magari ya jeshi na silaha za kisasa, alisema.

"Somalia inatarajia kuwajibika zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa ili kujenga vikosi vyake na kuvifanya kuwa na ufanisi zaidi katika kulinda ardhi yake na fukwe pamoja na kuendesha operesheni za ugaidi na kuuondoa uharamia na uvamizi mwingine wote wa ghafla katika eneo," Hirsi alisema.

Wakati ndio kiiini
Serikali haipaswi kusubiri kwa muda mrefu kuandaa kitengo chake kipya cha kuzuia ugaidi kwa sababu vitendo vya kigaidi vinawatishia wawekezaji na kuzuia maendeleo ya kiuchumi, kwa mujibu wa mchumi Mustafa Hassan Afrah.

Baada ya kupoteza chanzo chake kikuu cha fedha, al-Shabaab imejikita katika malipo na kuwaweka waporaji wenye silaha katika maduka ya mapambo ya vito kwa ajili ya kugharamia vitendo vyake vya kigaidi, Afrah aliiambia Sabahi.

Ndiyo sababu ni muhimu kupeleka vikosi vya wanajeshi huko Mogadishu kwa haraka na kuweka kizuizini wanamgambo kabla hawafanyi mashambulizi ya mauaji katika mabenki na majengo ya serikali, alisema.

Waziri wa Habari na Mawasiliano ya simu Abdullahi Ilmoge Hirsi alisema serikali haipaswi kujisahau na kuruhusu magaidi kuua watu wasiokuwa na hatia, kuharibu majengo ya biashara au kuiba fedha za watu.

Ulipuaji wa mabomu katika maeneo yenye watu wengi unakusudia kuleta kero na kutisha wageni na Wasomali ambao wamerejea nyumbani kutoka nchi za nje, alisema.

"Siwezi kutoa tarehe rasmi ambayo vitisho hivi kutoka kwa al-Shabaab vitamalizika lakini ninatarajia vitaisha hivi karibuni," Hirsi aliiambia Sabahi.

"Tutakuwa tukijadili masuala kadhaa kuimarisha usalama na mazungumzo ya kitaifa ili tuweze kuzuia mashambulio ya kulipua magari," alisema, akiongeza kwamba moja kati ya malengo yake yatakuwa ni kutenga na kuvunja nyumba zenye usalama ambazo al-Shabaab wanazitumia kupanga na kufanya mashambulio. "Tutafuatilia hali kabla milipuko haijaanza na kuandaliwa, na itakuwa katika uangalizi kwa ajili ya njama na mashambulio kutoka kwa kikundi hiki."

"Kuwepo kwa [al-Shabaab] kumefifishwa, jua lake limekuchwa na nyota yake imekufa," alisema Hirsi. "Tutajihakikishia usalama katika uwanja wa vita kwa kuwa vikosi vyetu vinafanikiwa hata kushinda zaidi."

No comments:

Post a Comment

Maoni yako