If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, April 16, 2013

Salva Kirr apunguza mamlaka ya makamu wake

Na Victor Melkizedeck Abuso

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametoa agizo la kupunguza mamlaka ya naibu wake Riek Machar hatua ambayo huenda ikasababisha machafuko ya kikabila nchini humo.

Salva Kiir rais wa Sudan Kusini

Hatua hiyo ya rais Kiir inaamanisha kuwa Machar ambaye ni mpiganaji wa zamani wa msituni na anayefahamika kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya kabila la Nuer sasa atahusika tu na kazi aliyopangiwa kikatiba nchini humo, lakini haikufahamika wazi ni mamlaka yepi hayo yaliondolewa.

Kuanzia siku ya Jumanne, jukumu kubwa la Machar litakuwa ni kumwakilisha rais Kirr wakati anapokuwa nje ya nchi hiyo kuwa mwanachama wa baraza la Mawaziri na baraza la Kitaifa la Usalama.

Uamuzi wa rais Kiir pia una maana kuwa hatua za Machar za kujaribu kuweka mipango ya kuliunganisha taifa hilo ambalo limekumbwa na ukabila huenda zikadidimia.

Kamati ya uwiano wa kitaifa nchini humo imevunjwa na rais Kiir suala ambalo raia nchini humo wamesema wameshangazwa na hatua hiyo ya rais.


Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa Machar ni mwanasiasa ambaye msimamo wake mara nyingi huwa haueleweki kutokana na wakati mmoja kuunga na kutounga mkono kujitenga kwa Sudan Kusini wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1983 hadi 2005.

Wakati mmoja, wapiganaji wake wa SPLM kutoka kabila la Nuer walijitenga na kuunga mkono serikali ya Khartoum wakati wa mapambano ya kujitenga kwa Sudan Kusini huku vikosi vyake vikituhumiwa kuwaua watu wa kabila la Dinka katika mji wa Bor mwaka 1991.

Chanzo: kiswahili.rfi

No comments:

Post a Comment

Maoni yako