Tsunami ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM mkoani Morogoro imeiacha CHADEMA taaban wilayani Gairo baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Mkalama wilayani Gairo Zefania Magiga na wenzake 68 kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 17, 2013, kwenye Uwanja wa shule ya Msingi, Umoja mjini Kilosa mkoani Morogoro.(Picha na Bashir Nkoromo).
Tsunami ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM mkoani Morogoro imeiacha CHADEMA taaban wilayani Gairo baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Mkalama wilayani Gairo Zefania Magiga na wenzake 68 kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara.
Magiga na wenzake wamekabidhi kadi zao za Chadema kwa Kinana, na kupewa kadi za CCM, baada ya kutangaza kukihama chama chao na kujiunga na CCM kwenye mkutano huo ambao ulifurika mamia ya wananchi, kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Gairo B, katika wilaya mpya ya Gairo.
Mbali na kupokea wanachama hao kutoka Chadema, kwenye mkutano huo, Kinana alipokea wanachama wapya 120, waliojunga na CCM na kufanya jumla ya wanachama wapya waliojinga na CCM kwenye mkutano huo kuwa 188.
“Ndugu wana Gairo wenzangu na Watanzania wote, mimi kwa nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Kata, nilikuwa naongoza wanachama wengi wa Chadema na nilikuwa si mtu mdogo, lakini kwa muda ambao nimekuwa ndani ya chama hicho nimebaini kuwa viongozi wake wa kitaifa ni matapeli wa hali ya juu, ndiyo maana mimi na wenzangu tumeamua kuhamia CCM”, amesema Magiga.
Amesema, akiwa Chadema alikuwa akishangaa kuona kwamba kila agizo alilokuwa akipokea kutoka viongozi hao wa chama hicho lilikuwa la kumwagiza kushawishi wananchi shari na kukataa kutii sheria za nchi, jambo ambalo amesema kwa muda mrefu alikuwa hakubaliano nalo kwa kuwa ni tofauti na lengo lililokuwa limemwingiza Chadema tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 15 iliyopita.
Akizungumza kwenye mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM, amesema, uamuzi wa wananchi wanaojiunga na CCM sasa na hata baadaye ni wa busara sana kwa sababu CCM ndicho chama ambacho bado cha kuaminika kwa malengo na matarajio yote ya maendeleo, amani na usalama wa Watanzania.
Chanzo: bashir-nkoromo.blog



No comments:
Post a Comment