If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, May 18, 2013

Diwani wa CHADEMA kata ya Mungaa jimbo la Singida Mashariki, afikishwa mahakamani.

DSC01237
Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Minyinga kata ya Mungaa jimbo la Singida mashariki, John Theodore Ghumpi (wa kwaza kushoto) akimhoji mbunge Tundu Lissu, ni kwa nini anatetea wahalifu ambao amedai wamejichukulia sheria mkononi kwa kukata kata ng’ombe zake sita.Ghumpi ni mume wa Mary John.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu

Mbunge wa jimbo la Singida mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, amepata wakati mgumu baada mmoja wa wapiga kura wake kumtaka amweleze ni kwa nini amekuwa akijikita kutetea wahalifu wa wazi wazi.

DSC01222
Diwani wa CHADEMA kata ya Mungaa jimbo la Singida Mashariki, Matheo Alex (wa pili kushoto aliyenyanyua mkono juu) akiwa katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida akisubiri kusomewa shitaka lake la kukata kata ng’ombe sita mali ya Mary John mkazi wa kijiji cha Minyinga kata ya Mungaa.Wa pili kulia ni mtoto wa diwani Alex, Faraja na wa pili kushoto Bahati Sumbe (mwenye jacketi la njano) wameunganishwa kwenye kesi moja na diwani Alex.

Mkazi wa jimbo la Singida mashariki, John Theodore Ghumpi alimbana vilivyo Tundu ambaye ni mwanasheria maarufu, muda mfupi baada ya kusimamia kesi ya diwani wa CHADEMA kata ya Mungaa Matheo Alex na wenzake wawili wanaotuhumiwa kukata kata ng’ombe sita kwa shoka mali ya Ghumpi.

“Kwa kifupi mimi sina ugomvi wo wote na CHADEMA wala na wewe Tundu, wewe licha ya kuwa ni ndugu wa ukoo, wewe ni mbunge wangu pia. Sasa unapojikita kubariki uhalifu kama huu wa kukata kata ng’ombe wangu,kwangu mimi unanipa wakati mgumu mno kukuelewa”,amesema Ghumpi.

Hata hivyo,Tundu alisema kuwa washitakiwa na walalamikaji katika kesi ya kukata kata ng’ombe sita,wote ni wapiga kuwara wake na wananchi wake wa jimbo la Singida mashariki,na hivyo ana wajibu wa kuwatumikia kwa usawa.

Kutokana na kibano hicho,wakili anayewatetea washitakiwa hao watatu, Tundu Lissu,alilazimika kufuatana na Ghumpi kwenda kijiji cha Minyinga kuangalia ng’ombe wanaodaiwa kukatwa katwa na wateja wake akina Matheo.

Awali diwani wa Kata ya Mungaa (CHADEMA) jimbo la Singida Mashariki, Matheo Alex pamoja na washitakiwa wenzake wawili wameburuzwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa, akikabiliwa na tuhuma ya kukata kata ng’ombe sita mali ya Mary John wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.5.

Katika kesi hiyo iliyovuta hisia za wakazi wengi wa jimbo la Singida mashariki na baadhi ya wakazi wa mkoa huu, washitakiwa wengine ni Faraja Matheo (mtoto wa diwani Alex) na mjomba wa diwani huyo wa CHADEMA, Bahati Sumbe.

Mwendesha mashitaka Mussa Chemu alidai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi, Ruth Massawu, kuwa mnamo mei 13 mwaka huu saa 5:00 asubuhi, huko katika kijiji cha Minjinga Kata ya Muunga, kwa makusudi diwani Matheo akishirikiana na washitakiwa wenzake, alikata kata ng’ombe sita mali ya Mary John kuzisababishia majeraha makubwa.

Washitakiwa kila mmoja kwa wakati wake, walikana kutenda kosa hilo.

Kabla ya kuahirishwa kwa Kesi hiyo, wakili wa washitakiwa hao, Tundu, alitoa hoja mbele ya mahakama hiyo kwamba katika kutoa dhamana, izingatie kifungu148 kidogo cha pili cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ibara ya 20.

Amesema kifungu hicho kinatoa maelezo kwamba kiwango cha dhamana kitapangwa kutokana na uzito wa kesi ambapo hakitakiwi kiwe kikubwa kupita kiasi.

Hakimu Massamu aliingilia kati na kumweleza Wakili Tundu kwamba, ameanza kazi ya kuilekeza mahakama nini cha kufanya.

“Subiri kwanza usikie mahakama inatoa masharti gani ya dhamana, kisha ndio uwasilishe maombi yako. Hata hivyo, kwa vile tuhuma ya uharibifu uliofanywa na washitakiwa ni wa zaidi ya shilingi 3.5 milioni, mahakama haina njia nyingine, ni lazima kila mshitakiwa adhaminiwe na watu wawili kwa ahadi ya dhamana ya shilingi milioni tano kila mmoja”,alisema hakimu Massamu.

Washitakiwa wote walidhaminiwa na wapo nje hadi mei 30 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako