If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, May 21, 2013

Rais Kikwete kuzindua miradi ya ujenzi wa barabara ya Dodoma-Iringa.

Dr-Jakaya-Mrisho-Kikwete
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUZINDUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA YA DODOMA – IRINGA YENYE UREFU WA KM 260 (SEHEMU ZA DODOMA – FUFU ESCARPMENT, FUFU ESCARPMENT – MIGORI NA MIGORI – IRINGA) KWA KIWANGO CHA LAMI TAREHE 22 MEI, 2013

Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba, tarehe 22 Mei, 2013 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara kama ifuatavyo:-

1) Tarehe 22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu Escarpment (km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini.

2) Tarehe 22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu Escarpment – Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji cha Migori Wilayani Iringa Vijijini.

Barabara ya Iringa – Dodoma ni sehemu ya barabara muhimu ijulikanayo kama “Great North Road” inayoanzia Capetown Afrika ya Kusini hadi Cairo, Misri kupitia Tanzania. Nchini Tanzania inaunganisha Miji ya Tunduma (mpakani na Zambia), Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha na Namanga (mpakani na Kenya).


Mradi huu ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara na unalenga kupanua fursa za kiuchumi na kibiashara kwa wananchi, na kati ya Tanzania na nchi jirani za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kwa njia hii, barabara itakuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Taarifa hii imetolewa na

Balozi Herbert E. Mrango

KATIBU MKUU

WIZARA YA UJENZI
Chanzo: Moblog

No comments:

Post a Comment

Maoni yako