Na Majid Ahmed, Mogadishu
Wakaazi, wazee wa kimila na maofisa wa serikali nchini Somalia kote wanatoa wito kwa wanamgambo wenye uadui wa kurithi juu ya udhibiti wa Kismayo kuweka silaha chini na kuja katika meza ya mazunguzmo kutatua masuala yaliyobakia na kuhakikisha maisha ya amani yanarejea.

Wanachama wa Jeshi la Taifa la Somalia na wanamgambo wa Ras Kamboni walioshirika na serikali wakipeperusha bendera ya Somalia kutoka kwenye uliokuwa mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa Kismayo katika kushereheka kukamatwa kwake tarehe 2 Oktoba, 2012. [AFP Photo/AU-UN IST Photo/Stuart Price]
Vurugu zilizokuwa zimesimama zilianza tena Ijumaa (tarehe 7 Juni) baada ya wanamgambo wa Ras Kamboni wanaomtii Shekhe Ahmed Mohamed Islam Madobe kuripotiwa kuweka wazi kuwa kiongozi wa wanamgambo hao Iftin Hassan Basto kutoka kwenye mkutano na Waziri wa Ulinzi wa Somalia Abdihakim Haji Mohamud Fiqi. Madobe, Basto na Barre Adam Shire Hirale wote kwa sasa wamelaumiwa kwa kuwa watiifu kwa raisi aliyeteuliwa wa serikali changa ya shirikisho ya Jubbaland.
Mapigano makali yaliibuka, yaliua watu wapatao 18, yakijeruhi wengine zaidi ya 20 na kulazimisha mamia ya wakaazi kukimbia na kutafuta hifadhi katika vijiji vya jirani, kwa mujibu wa Nur Abdirahman, mkaazi mwenye umri wa miaka 38.
Familia ya watu watano mtaani wake walikuwa miongoni mwa waathirika, Abdirahman alisema, wakati magamba ya mota yalipodondoka katika nyumba yao ya wastani .
"Tunachotaka tu ni hali kuimarika," aliiambia Sabahi. "Tunamwomba Mungu kwamba mapigano haya yamalizike kabisa na kamwe tusikie tena milio ya mota au risasi huko Kismayo."
Jumapili, wazee wa kimila waliweza kunyamazisha mapigano baina ya vikundi vilivyo katika mapigano, kumaliza vita na kurudisha jiji katika hali ya utulivu, mtandao wa Shabelle Media Network uliripoti. Pande zote mbili ziliamua kurudi kwenye ngome zao baada ya wazee wa eneo hilo kukutana nao tofauti tofauti kuwashawishi kushiriki katika mazungumzo.
Hata hivyo AFP iliripoti Jumatatu kwamba wapiganaji wanaomtii Madobe wamejizatiti katika udhibiti wao wa mji.
"Hali sasa ni shwari na sehemu nyingi za mji zinadhibitiwa na watu wa Madobe," alisema mkaazi wa Abdulahi Mire, akiongeza kwamba vikosi vya upinzani vilikuwa nje ya mji lakini "haviko mbali".
Kwa sasa, viongozi wa wanamgambo wa pande zote mbili wanaendelea kushutumiana kwa kuanzisha vurugu na kuhusika na kuendeleza hali hiyo.
Basto aliiambia Sabahi vikosi vyake vilikuwa vinajihami mara mbili wakati wanamgambo wapinzani walipojaribu kumvamia wakati anaelekea kwenye hoteli ya nchini kukutana na ujumbe wa shirikisho uliyoongozwa na Waziri Fiqi na baadaye nyumbani kwake.
Msemaji wa Ras Kamboni Abdinasir Serar, badala yake, aliilaumu serikali ya shirikisho kwa kuingilia na kuwaunga mkono waliokuwa majemadari wa vita katika mkoa.
"Tunatoa wito kwa serikali huko Mogadishu kuachana na kuvuruga hali tete katika Jubbaland na kuchochea migogoro ya ndani baina ya makabila katika mkoa," aliiambia Sabahi.
"Pia tunatoa wito kwa serikali kuzidisha jitihada zake katika mapambano dhidi ya kikundi cha ugaidi cha al-Shabaab nchini Somalia, badala ya kupoteza muda na rasilimali katika kuchochea moto wa mgogoro wa ndani miongoni mwa makabila huko Kismayo katika jaribio la kutothamini mafanikio ya jamii za Jubbaland".
Njia ya amani ya kudumu
"Somalia imeshapata uzoefu wa kutosha [kwa vita vya kikabila]," alisema Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon wakati akitoa hotuba katika sherehe zilizofanyika huko Mogadishu Jumapili kutangaza rasmi huduma ya msaada wa mamilioni ya dola kutoka Saudi Arabia.
Akidokezea vita vya kikabila ambavyo viliihuzunisha nchi kufuatia kuanguka kwa utawala wa Mohamed Siad Barre, waziri alisema Wasomali wanajua kwa hakika kwamba mapigano ya kikabila sio suluhisho linalowezekana kwa amani ya kudumu.
"Vurugu ambazo zimekuwa zikiendelea huko Kismayo hazitatatua tatizo," alisema. "Ningeviomba vyama vilivyohusishwa katika msukosuko kusamehe vurugu hizo na kuwa na imani katika serikali yao na mchakato [iliyoweka]".
Rais Sheikh Mohamud pia aliita mapigano hayo ni bahati mbaya na kusema alishangazwa na matukio yanayoendelea. "Vurugu haziwezi kutumika kama njia ya kufanikisha malengo ya kisiasa," alisema katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumamosi.
"Muda wa vita umekwisha," alisema rais. "Tunatakiwa kuungana na kufanyia kazi kusuluhisha migogoro yetu kwa njia za amani. Tunapaswa kuungana pia kuwapiga al-Shabaab".
Uongozi uliokomaa unahitajika kuendelea
Mwakilishi maalumu wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (SRCC) kwa niaba ya Balozi wa Somalia Mahamat Saleh Annadif alitoa wito kwa viongozi wa Somalia wa ngazi zote kuonyesha ukomavu na uaminifu katika kusuluhisha migogoro.
"Watu wa Somalia na viongozi wanapaswa kutumia nguvu za kiusalama zinazofanywa na Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), jeshi la usalama la Somalia na wanaofungamana nao, kuendeleza amani na mafanikio. Wanapaswa kutumia kipindi hiki muafaka kumaliza migogoro ya kisiasa ambayo inasababisha ugumu katika mchakato wa kuiimarisha Somalia".
Ismail Mohamed, mchambuzi wa masuala ya siasa anayeishi Kismayo, alisema migogoro inayojitokeza wakati wa uanzishaji wa Jubbaland kuwa ni migumu na dhaifu na itafanya kipimo muhimu kwa serikali ya shirikisho.
"Kimsingi, mazungumzo ya kina na mjadala wa amani ni njia pekee ya kumaliza mgogoro huko Jubbaland," alisema.
Serikali ya shirikisho inatarajiwa kufanya mkutano wa usuluhishi kuhusu Kismayo hivi karibuni.
Mji wa bandari uliokombolewa na al-Shabaab mwezi Septemba 2012, kukata shina la mapato yaliyotegemewa na ufikiaji wa kimkakati wa kundi hilo.
Source - sabahionline.com



No comments:
Post a Comment