If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, July 10, 2013

Chama cha Muslim Brotherhood nchini Misri chakataa kupatiwa nafasi za uwaziri ndani ya Serikali ya mpito

Waziri Mkuu mpya nchini Misri, Hazem el-Beblawi
Waziri Mkuu mpya nchini Misri, Hazem el-Beblawi
AFP/GERARD JULIEN
Na Lizzy Anneth Masinga

Chama cha Muslim Brotherhood chakataa kupatiwa nafasi yeyote ndani ya Serikali ya mpito nchini Misri, badala yake kimesisitiza kurejeshwa madarkani kwa aliyekuwa Kiongozi wa taifa hilo,Mohamed Morsi.

Saa kadhaa baada ya kuteuliwa kwa Waziri Mkuu Maafisa nchini humo walitangaza kuwa Chama cha Muslim Brotherhood na chama cha kiislamu cha Nour vitapatiwa nafasi za uwaziri katika Serikali ya Mpito ya nchini Misri.

Hazem el-Beblawi, Mchumi na Waziri wa zamani wa Fedha ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Msemaji wa Ofisi ya Rais Ahmed al Muslimani ameeleza.

Mshindi wa Tuzo la amani la Nobel na Kiongozi wa Upinzani nchini Misri, Mohamed ElBaradei aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais katika wizara ya Maswala ya mambo ya nje.

Uteuzi huo ulifuatiwa na Tangazo kuwa nafasi za uwaziri katika Serikali mpya zitaachwa kwa Chama cha Freedom and Justice,Muslim Brotherhood na Nour.

Hatua ya uundwaji wa Serikali ya mpito imekuja takriban juma moja baada ya Jeshi kumuangusha aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed Morsi na kumteua Adly Mansour kuwa Rais wa nchi hiyo.

ElBaradei awali ilisemekana kuwa aliteuliwa kuongoza Baraza la Mawaziri lakini uteuzi wake haukuungwa mkono na Chama cha Nour.

Waziri Mkuu mpya anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuliunganisha Taifa lililogawanyika na kuunusuru Uchumi wa nchi hiyo.

Via kiswahili.rfi.fr

No comments:

Post a Comment

Maoni yako