If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, July 9, 2013

Kumbukumbu za habari ya vijana zalenga ukosefu wa ajira, ukosefu wa usalama Garissa

Na Bosire Boniface, Garissa

Ili kusaidia kuzuia uhalifu na kuwatambua vijana kwa ajili ya matumaini ya ajira, Kaunti ya Garissa inakusanya habari za msingi juu ya vijana wa eneo hilo.

Vijana katika kaunti ya Garissa kaskazini mashariki ya Kenya wanakabiliwa na matumaini finyu ya ajira. Juu, watoto kutoka shule ya msingi ya Bour Argy wanasoma vitabu vilivyoazimwa kutoka maktaba ya "ngamia" ya Garissa. [Na Alexander Joe/AFP]

Habari hizo zitakwenda katika kumbukumbu za habari ya vijana, ambayo maafisa wa kaunti watazitumia kwa kutengeneza sera na huduma zinazoelekezwa kwa vijana, Gavana wa Kauntu, Nathif Jama Adam aliiambia Sabahi.

Katika mpango huo, ulioanza tarehe 24 Juni, vijana wote katika kaunti hiyo watatakiwa kutoa majina yao, tarehe ya kuzaliwa, wanapoishi pamoja na habari kuhusu viwango vya elimu zao, shughuli zao za sasa au hali ya ajira, Adam alisema.

"Ukosefu wa fursa za ajira umekuwa ukilaumiwa kwa vijana kujihusisha na shughuli za kihalifu, ikiwa ni pamoja na kujiunga na kikundi cha al-Shabaab," alisema. "Tunataka kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na kiusalama zinazoikabili kaunti hii."

"Jambo lililo la uhakika ni kuwa vijana ni kundi kubwa zaidi [la idadi ya watu] na pia ndio asilimia ya juu zaidi isiyo na ajira," alisema. "Habari hizi zitatusaidia kuzipanga katika mipango ya maendeleo."

Mpango wa kumbukumbu za habari za vijana ulianzishwa kufuatia taarifa kwamba vijana walihusika katika vurugu za hivi karibuni katika majimbo ya Garissa na Wajir, na ni sehemu ya mipango mipana ambayo itashughulikia matatizo ya kimfumo na kielimu ambayo yanalifanya kaunti iwe katika hatari ya kuathiriwa na al-Shabaab na makundi mengine ya watu wenye siasa kali.


Kama sehemu ya mpango huo, Kamishna wa zamani wa Kaunti ya Garissa Mohammed Maalim alianzisha kampeni ya "Mjue Jirani Yako" mwezi wa Februari, uliounda kumbukumbu za wamiliki majumba na wapangaji wao katika kaunti ya Garissa, na kufufua mpango wa polisi wa akiba wa mjini.

Kumbukumbu hizo za habari zitakuwa muhimu kwa kutambua matatizo yanayowakabili vijana pamoja na kuwasaidia kuwa na sifa za kupata programu zinazofadhiliwa na serikali, mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Vijana wa Kaunti ya Garissa Hussein Salat Gure aliiambia Sabahi.

Hata hivyo, serikali ya kaunti inapaswa kujiepusha dhidi ya kuchagua kulenga baadhi ya sehemu za vijana na kuwatenga wengine kwa fursa za ajira au kufadhili mipango Gure, alisema.

"Huko nyuma kumekuwepo na hatua za makusudi za viongozi kuwapendelea watu wa koo zao katika maendeleo," alisema. "Ili kushughulikia changamoto za usalama na uchumi zinazowakabili vijana wa kaunti, mipango inayojumuisha wote ni muhimu."

Kuna koo tatu kuu katika Kaunti ya Garissa na nyengine ndogo isiyopungua nne. Kuuacha upande ukoo wowote katika hizo nne kunaweza kuhujumu ajenda ya gavana ya maendeleo, Gure alisema.

Ili kuwakinga vijana wasijiingize katika uhalifu, serikali ya kaunti inapaswa kuwashirikisha katika shughuli za kiuchumi, alisema Mustapha Khalib, mwenye umri wa miaka 30 na karani wa tiketi anayefanya kazi katika kampuni ya huduma za usafiri ya Dekh Coach Travellers.

Ni rahisi kwa vijana wasiyo na kazi kuingia katika uhalifu, Khalib alisema, na kuongeza kwamba kwa kweli alitumikia miaka nane katika Gereza Kuu la Kamiti kwa sababu ya wizi na vurugu.

"Serikali ya jimbo inapaswa kuwaingiza wafungwa wa zamani katika mipango yao ya maendeleo na [kuwezesha] maingiliano katika jamii," alisema.

"Wakati mtu anapokuwa hana la kufanya, mambo kadhaa humpitia akilini mwake," aliiambia Sabahi. "Huku umri ukiwa unakwenda, mtu hugundua kuwa hana chochote na jamii na serikali inajali kidogo. Ili kufidia wakati uliopotea, hujiingiza katika uhalifu."

No comments:

Post a Comment

Maoni yako