If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, August 28, 2013

Kenya kuongeza tahadhari kwa ajili ya njama za ugaidi wa al-Shabaab

Na Bosire Boniface, Garissa

Al-Shabaab wanaweza kuwa wanapanga njama za mashambulio ya kigaidi huko Kenya katika kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kutokea kwa mauaji ya sababu za kisiasa ya ulama mwenye msimamo mkali Aboud Rogo Mohammed, maofisa usalama watahadharisha.

Polisi wa Kenya wa kutuliza ghasia wakipiga doria nje ya msikiti wa Masjid huko Mombasa, tarehe 31 Agosti, 2012. Ghasia ziliibuka katika mji wa bandari baada ya kuuawa kwa ulama mwenye msimamo mkali Aboud Rogo Mohammed. [Simon Maina/AFP]

Maofisa usalama wa Kenya wiki iliyopita waliwatahadharisha raia, wakisema kikundi cha wanamgambo cha Somalia kinaweza kulenga Mombasa, jiji la pwani mahali ambapo ulama alikuwa akitoa mawaidha na mahali ambapo aliuawa akiwa anaendesha gari kwa kupigwa risasi tarehe 27 Agosti, 2012.

Mamlaka zimeimarisha usalama baada ya kupokea ripoti za upelelezi kwamba wapiganaji wa al-Shabaab wapatao watano wameingia Kenya wakitokea Somalia, Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Pwani Aggrey Adoli aliiambia Sabahi.

"[Watu binafsi] waliingia Mombasa kati ya tarehe 18 Agosti na walitarajiwa kuungana na wenzao huko Mombasa kufanya mashambulio," alisema. "Wakati Wakenya wakiendelea na shughuli zao, wanapaswa kuwa na tahadhari kuhusu lengo baya la kikundi hicho."

Wafanya ghasia huko Mombasa walichoma gari hili wakati wa wimbi la vurugu lililosababisha uharibifu na vifo ambazo zilifuatia kuuawa kwa ulama mwenye msimamo mkali Aboud Rogo Mohammed tarehe 27 Agosti, 2012. [AFP]

"Tunajua shabaha maalamu ambayo wanamgambo hao wanachunga sana, ikiwa ni pamoja na hoteli, makanisa, vituo vya polisi na ofisi za usalama. Hatutataja maeneo hayo lakini tumesambaza maofisa usalama kwenye maeneo lengwa na kuongeza usalama kukabiliana na mipango hiyo," Adoli alisema.


Angalau maulama wawili wako chini ya uangalizi wa polisi, kama ripoto za usalama zinavyoonyesha kwamba kuna uwezekano kuwa wanaratibu mashambulio yaliyopangwa, alisema.

Ingawaje ripoti hizo zinaonyesha kwamba al-Shabaab walilenga Mombasa, raia wa Kenya katika majiji mengine wanapaswa kuwa waangalifu kwa ishara za njama za kigaidi, mkuu wa polisi alisema.

Maadhimisho ya mwaka mmoja baada mauaji ya Rogo
Viongozi wametoa tahadhari kwa Mombasa siku za kabla ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha Rogo.

Rogo alikuwa katika orodha ya vikwazo vya Baraza la Umoja wa Mataifa kwa sababu ya kujihusisha kinyume cha sheria na al-Shabaab na kikundi cha al-Hijra cha Kenya -- pia kinachojulikana kama Kituo cha Vijana wa Kiislamu (MYC). Kuuawa kwake kulisababisha maandamano makali huko Mombasa ambayo yalisababisha uharibifu wa biashara na kuchomwa kwa makanisa.

Baada ya maandamano, serikali ya Kenya iliunda kikosi kazi kilichoongozwa na Kaimu Mwendesha Mashtaka wa Serikali Jacob Ondari kuchunguza mauaji ya Rogo. Ondari alitangaza Jumatatu (tarehe 26 Agosti) kwamba kikosi kazi hakikuweza kuwatambua wale waliofanya mauaji ya Rogo.

Muda wa tukio la hivi karibuni ulipangwa kukutana na maadhimisho, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Mombasa Robert Kitur aliiambia Sabahi.

"Tunajua kwamba al-Shabaab wanalenga sherehe za nchi na za kimataifa ambazo zitakuwa na idadi kubwa ya watu," alisema, akitoa wito kwa jamii kushirikiana na polisi kusaidia kuzuia vitisho.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kushiriki uzinduzi wa bandari ya Mombasa Jumatano na kuongoza Onyesho la Kimataifa la Mombasa, maonyesho ya kilimo yanafanyika tarehe 28 Agosti hadi tarehe 1 Septemba.

Kamishna wa Kata ya Mombasa Nelson Marwa alisema serikali haitaruhusu wanamgambo kuvuruga amani ambayo wananchi wenyeji wamekua wakiipata kwa muda mrefu.

"Hatukuwa na mashambulizi kwa miezi mitatu iliyopita. Katika kipindi hicho tumefanikiwa kuzuia mipango kadhaa ya mashambulizi ya magaidi na kuwakamata washukiwa kadhaa kwa sehemu kwa sababu ya ushirikiano wa jamii," alisema, akiongeza kwamba mamlaka zitaendelea kuwashughulikia wale wanaosababisha mapinduzi.

Wakati huo huo, hoteli zimekuwa zikifuata hatua za kuwakagua wageni, alisema Bernard Akama, mlinzi binafsi mwenye umri wa miaka 25, huko Mombasa.

"Tumepanga eneo la ukaguzi kuwa mbali na lango la kuingilia," aliiambia Sabahi. "Tunasaidiwa na angalau ofisa usalama mmoja mwenye silaha. Alama ya silaha katika maeneo ya hoteli sio picha nzuri, lakini kwa ajili ya usalama wa wote ni muhimu."

Abdullahi Mohammed Jamaa, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 25 huko Mombasa, aliiambia Sabahi kwamba amegundua ongezeko la ulinzi katika siku za hivi karibuni.

"Kuwepo kwao mitaani kunatupatia dhana ya usalama," alisema. "Ni marafiki pia kwa sababu wanazungumza nasi na kutuuliza iwapo kuna tatizo lolote la usalama."

No comments:

Post a Comment

Maoni yako