If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, August 27, 2013

Tanzania yachukua hatua kali dhidi ya biashara ya magendo ya dawa za kulevya

Na Deodatus Balile, Dar es Salaam

Baada ya waimbaji wawili mashuhuri wa Tanzania kukamatwa Julai huko Afrika Kusini kuhusiana na biashara ya magendo ya madawa ya kulevya na tuhuma zinazohusiana dhidi ya wafanyakazi sita wa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, serikali ya Tanzania inachukua hatua kali dhidi ya usafirishaji wa madawa ya kulevya.

Mzigo huu mkubwa wa heroini ulikamatwa huko Nairobi tarehe 14 Februari, 2013. Madawa hayo yalinunuliwa kutoka Tanzania na yalikusudiwa kupelekwa Uingereza. [AFP Photo/Stringer]

"Tumeweka operesheni ya pamoja maalumu ambayo itahusisha polisi, upelelezi na kitengo chetu cha upelelezi cha jeshi kusimamisha wasafirishaji katika vituo vyote vya kuingizia," msemaji wa serikali na Mkurugenzi wa Shirika la Habari la Tanzania Assah Mwambene aliwaambia waandishi wa habari tarehe 21 Agosti.

Baadhi ya hatua mpya zinalenga kufunga mianya katika taratibu za usalama za kupokea mizigo na kuikagua, Waziri wa Usafirishaji Harrison Mwakyembe aliiambia Sabahi.

Chini ya sheria mpya, waajiriwa wote wa uwanja wa ndege watatakiwa kujisajili wakati wa kuanza zamu zao na muda wa kumaliza katika kitabu cha mahudhurio. Waajiriwa pia wanatakiwa kurekodi muda kwa ajili ya kwenda msalani, waziri alisema.

Ofisa polisi wa shirikisho la Australia akionyesha baadhi ya dawa nyingi za methamfetamini alizokamatwa ambazo haijawahi kutokea katika kemikali za kusafishia zilizosafirishwa kwa meli. Nchini Tanzania na Afrika Kusini, dawa hizo hujulikana kama "tik". [Australian Federal Police/AFP]

Zaidi ya hayo, waajiriwa watazuia kuingia maeneo ya kazi kama watafika kazini kwa kuchelewa, Mwakyembe alisema. Wasimamizi watawajibika kuhakikisha kwamba rekodi zinatunzwa kulingana na kanuni.


Sheria hizi zinazuia yeyote zaidi ya wafanyakazi walioidhinishwa -- kama vile wachukuzi na wakala wa forodha -- kukutana na mizigo ya abiria. Yeyote atakayepuuza sheria hii atachukuliwa hatua na anaweza kukabiliwa na athari za kisheria, alisema.

Kuchukuliwa kwa hatua kali za kinidhamu ni katika kutoa mwitikio wa kupasuka kwa dawa tarehe 5 Julai kulikohusisha waimbaji wa Tanzania Agnes Gerald Deal, anayejulikana kama Masogange, na Melisa Edward.

Wanawake hao wawili walikamatwa baada ya ndege yao iliyotoka Dar es Salaam kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo nje ya Johannesburg, wakituhumiwa kubeba kilogramu180 za madawa ya kulevya aina ya methamfetamini ya chembe katika masanduku tisa yanayofanana, Mwakyembe aliiambia Sabahi.

Viongozi sita katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam walituhumiwa kwa kuwasaidia wanawake hao wawili kukagua mizigo yao yenye madawa ya kulevya katika kaunta ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini. Kamera za usalama za uwanja wa ndege ziliwarekodi watuhumiwa waliohusika.

Viongozi hao walitambuliwa kama Jackson Manyonyi, Mohamed Kalungwana, Yusufu Daniel Issa, Juliana Thadei, Zahoro Mohamed Selemani na Corporal Ernest. Walituhumiwa kwa kupitisha masanduku kwa haraka ambayo yalikuwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 8.2 za kitanzania (Dola milioni 5.1 ), na wamefukuzwa kazi.

Waimbaji wawili waliokamatwa wamefikishwa katika mahakama ya Afrika Kusini na huenda wakakabiliwa na kifungo cha maisha, Mwakyembe alisema.

Tanzania kituo cha biashara ya madawa ya kulevya kimataifa
Kwa mujibu wa Msaidizi wa Kamishna wa Polisi Godfrey Nzowa, anayeongoza kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya Tanzania, karibia watu 2,000 walikamatwa katika miaka mitatu iliyopita kwa biashara au kutumia madawa ya kulevya. Kesi zilizo nyingi kati ya hizo zinahusisha mashamba ya bangi mkoani Mara.

Hata hivyo, heroini, inaletwa kuuzwa nchini Tanzania kutoka katika meli za mizigo za nje za Pakistani, alisema.

"Kwa kawaida meli husimama Baharini ya Hindi usiku na kushusha madawa ya kulevya katika mashua ziendazo kasi ambazo huyapeleka pwani ya Bagamoyo," Nzowa aliiambia Sabahi. "Kutoka Bagamoyo, madawa ya kulevya hupakiwa kwenye magari ya gharama na kupelekwa Dar es Salaam kwa ajili ya kufungishwa tena na kusafirishwa kwa ndege kwenda Afrika Kusini, China na sehemu nyingine duniani."

Wasafirishaji wa heroini Pakistani wanafanya usafirishaji haramu kwenda China kupitia Tanzania kwa sababu ya ukaguzi mkali wa usalama wa China katika vitu vinavyoagizwa kutoka Pakistani, Nzowa alisema.

Uongozi wa Tanzania umeendelea kupata mafanikio katika kugundua madawa ya kulevya, tunashukuru kwa taarifa zilizopatikana kutokana na uchunguzi unaoendelea na vifaa vipya vilivyotolewa na washirika wa kimataifa, alisema.

"Tumepokea teknolojia mpya kutoka Marekani ambapo tunachoma sindano kwa kemikali maalumu kwa ajili ya kugundua madawa ya kulevya katika mizigo inayoshukiwa na wakati unapoichomoa, kama sanduku lina madawa haramu, sindano itatoa majivu katika sekunde tano," alisema.

Tanzania pia inashirikiana na mashirika ya ulinzi ya kimataifa kupambana na biashara ya madawa ya kulevya kimataifa, kwa mujibu wa Christopher Shekiondo, mkuu wa Tume ya Kudhibiti madawa ya kulevya.

'Kutovumilia rushwa'
Hata hivyo, usafirishaji wa madawa ya kulevya bado ni tatizo nchini Tanzania kwa sababu ya viongozi kula njama, alisema Kamanda wa Huduma ya Utoaji wa Vibali vya Uhamiaji na vibali vya kupita Dawson Mongi.

"Huwezi kupamabana na madawa ya kulevya bila kukabiliana na rushwa nchini," Mongi aliiambia Sabahi. "Madawa ya kulevya yanaharibu picha yetu kama nchi. Tunatakiwa kutatua kama nchi ili kutovumilia rushwa."

Akitoa maoni yake kwamba serikali haishughulikii vya kutosha suala hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi alisema idadi kubwa ya ukamatwaji unaohusiana na madawa ya kulevya unaonyesha jinsi serikali ilivyo makini katika kushughulikia tatizo hilo.

"Serikali imetoa maelekezo maalum kumkamata yeyote atakayehusika na biashara hii haramu, bila kujali cheo, uhusiano wa kisiasa na kikabila," aliiambia Sabahi.

Wakati huohuo, sheria mpya ya kukabiliana na usafirishaji wa madawa ya kulevya imeandaliwa, alisema William Lukuvi, waziri wa serikali katika ofisi ya waziri mkuu kwa sera, uratibu na bunge la taifa.

"Tumegundua kwamba sheria zetu zina uzembe kidogo kuhusu usafirishaji wa madawa ya kulevya. Wasafirishaji wanatozwa faini ya shilingi 500,000 (Dola 309) kwa anayekamatwa akiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 10 (Dola milioni 6.1). Hii sio kitu," alisema Lukuvi.

"Baraza la mawaziri sasa linaijadili sheria, na litakuja na adhabu kadhaa ambazo zitawazuia watu kujihusisha na biashara hii," aliiambia Sabahi.

Miongoni mwa mawazo mapya yaliyojadiliwa katika uanzishaji wa mahakama maalumu kwa ajilii ya kuharakisha kesi za madawa ya kulevya.

"Kwa sasa, inachukua hadi miaka saba kusikiliza kesi dhidi ya wasafirishaji wa dawa za kulevya. Hadi wakati wa kusikiliza kesi unapofika, ushahidi wakati mwingine unakuwa umeharibika kutokana na viwango hafifu vya utunzaji wa ushahidi," alisema Lukuvi. "Kwa hiyo,mahakama inaishia kuwaachia huru wauzaji wa madawa ya kulevya kutokana na masuala ya kiufundi."

Serikali inashughulikia kuboresha huduma ambapo ushahidi wa uhalifu utatunzwa, alisema.

"Mwaka huu wa fedha tumetenga shilingi milioni 300 (Dola 185,000) chini ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya kujenga bohari ambalo litatumika kutunza ushahidi mara wakosaji watakapokamatwa," alisema.

Chanzo - sabahionline.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako