If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, August 16, 2013

Wasiwasi waibuka kuhusu maandalizi ya vikosi vya usalama vya Somalia

Na Abdi Moalim, Mogadishu

Kuongezeka kwa mashambulio ya hivi karibuni huko Mogadishu na mashambulio ya al-Shabaab wakati wa Ramadan kumeibua wasiwasi miongoni mwa Wasomali wengi kuhusu uwezo wa serikali kukabiliana na vurugu.

Askari wa Somalia walipigwa picha baada ya wanamgambo wa al-Shabaab kushambulia eneo la Umoja wa Mataifa huko Mogadishu tarehe 19 Juni, 2013. [Mohamed Abdiwahab/AFP]

Aliyekuwa mkuu wa Shirika la Upelelezi na Usalama la Taifa la Somalia (NISA) Ahmed Moalim Fiqi alisema serikali ya shirikisho hairithishi uwezo wa jeshi kitaifa wa kuhakikisha usalama, na inakabiliwa na matatizo mengi ambapo inahitaji msaada.

Fiqi alisema serikali inahitaji kuja na mpango bayana wa kupambana na al-Shabaab, kushughulikia migogoro ya kikabila na kupanga kwa ufanisi na kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia ili kupata msaada huo.

"Tawala za mkoa, uma, maulamaa, wasanii, vijana, wazee wa kimila, wote wana jukumu katika mapambano hayo [kwa ajili ya amani] -- kisha tunaweza kuita dunia," alisema.

Mlinzi wa usalama wa Uturuki, ambaye alijeruhiwa katika bomu la al-Shabaab la kujitoa muhanga katika ubalozi wa Uturuki huko Mogadishu, alibebwa katika gari ya wagonjwa kupelekwa uwanja wa ndege wa Ankara tarehe 28 Julai. [Stringer/AFP]

Mpango unaofaa kutoka kwenye utawala ungevutia na kutoa mwitikio kwenye mahitaji ya maeneo mbalimbali ya jamii ya Wasomali, na kufanikiwa kungehitaji pia kila upande kusaidia serikali katika kutekeleza hilo, Fiqi alisema.

Kitu kilicho muhimu sana, alisema, ni kujenga hisia kali za utaifa miongoni mwa askari wa serikali. "Askari wetu wanapaswa kuamini katika mapambano kama kanuni [kwa sababu] bado wanaonekana kama kupitia adui hawajulikani."

Fiqi alishauri vikosi vya usalama kutumia mbinu za kisasa kukabili ugaidi, ikiwa ni pamoja na simu, uchunguzi kupitia simu na kieletroniki. "Uzuiaji ni muhimu kwa upelelezi. [Al-Shabaab] hutumia simu za ndani hivyo mazungumzo yao kupitia simu yanapaswa kusikilizwa."

Vitisho na mashambulio ya Al-Shabaab
Msemaji wa al-Shabaab Abdiasis Abu Musab alitangaza tarehe 5 Agosti kwamba kikundi hicho cha wanamgambo kilifanya mashambulio 26 siku ya 27 ya Ramadhani -- kikichukulia siku hiyo kuwa ya kitakatifu katika mwezi huu -- katika mikoa ya Benadir, Bay na Shabelle ya chini ya Somalia.

Tangazo lake limekuja siku moja kabla ya mashambulio mengi kama 20 ya maguruneti kadri ya al-Shabaab jijini Mogadishu kote kujeruhi watu wapatao 15. Haya yalifuataia wimbi la hivi karibuni la mapambano na ulipuaji mabomu yaliyofanywa na wanamgambo hao ambayo yalilenga vituo vya serikali na vituo vya nje vya kidiplomasia na vya misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na mashambulio kwenye Ubalozi wa Uturuki na maeneo ya Umoja wa Mataifa huko Mogadishu.

Mashambulio na vitisho hivyo ambavyo vinatarajiwa kuongezeka vinawatisha raia ambao wanaishi katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali, kwa mujibu wa Muungano wa Amani, ambavyo vinajumuisha pande za kisiasa, vikundi shawishi na asasi za kiraia huko Mogadishu. Kikundi hicho kilisema serikali inapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kulinda watu dhidi ya kitisho cha al-Shabaab.

Raia wa Somalia wamelazimika kusikiliza agizo la al-Shabaab ya kuwa mbali na majengo ya serikali na asasi za kimataifa zinazotoa misaada ya kibinadamu, ambapo inaathiri uwezo wao wa kupata misaada, Mwenyekiti wa Muungano wa Amani Abdullahi Sheikh Hassan alisema.

"Ukimya wa serikali umehamasisha al-Shabaab kutishia watu kutokwenda kuishi maeneo fulani," aliiambia Sabahi.

Kuibuka kwa vikwazo na kufungwa kwa barabara za umma hakutafanya kitu katika kuboresha usalama, Hassan alisema, akiongezea kwamba serikali inapaswa kuja na mpango madhubuti ambao ungejumuisha askari waliopata mafunzo ya kiwango cha juu na waliowezeshwa kisilaha.

"Maofisa elfu mbili [waliopaza mafunzo kikamilifu] wangetosha kuweka usalama Mogadishu," alisema.

Serikali yasema asilimia 90 ya mashambulizi ya al-Shabaab yameshindwa
Kinyume chake, Msemaji wa Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon, Ridwan Haji Abdiwali alitetea rekodi ya serikali ya shirikisho katika kuzuia mashambulizi ya al-Shabaab.

"Asilimia tisini ya njama za al-Shabaab [zilizodhamiriwa] zimeshindwa, na hakuna ukweli kwa propaganda na sifa mbaya iliyoonyeshwa kuhusu usalama," Abdiwali aliiambia Sabahi.

Serikali pia imeachilia mbali shutuma kwamba haikuwa tayari kufanyia kazi masuala ya usalama.

Kwa mujibu wa Abdiwali, serikali kwa mara ya kwanza imefanikiwa kulipa mishahara ya mara kwa mara kwa wanajeshi. Kila mwanajeshi anapokea Dola 160 kama ujira wa mwezi, ambayo ni zaidi ya kile walichokuwa wakipata awali kwa vipindi, alisema Abdiwali.

Aidha, alisema Jeshi la Somalia hivi karibuni litaongeza wanajeshi wengine 1,800 lakini alikataa kutoa maelezo zaidi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanali mstaafu wa Jeshi la Taifa la Somalia Abdikarim Daud, serikali imekabiliwa na udhaifu katika usalama na kuachwa nyuma katika ujenzi wa vifaa vinavyoaminika vya usalama kwa sababu jeshi la taifa linaendelea kutojipanga kikamilifu na kutopewa fedha. Baadhi ya wajumbe wa jeshi la usalama bado hawalipwi kila mara, alisema Daud, ambaye alitumikia chini ya utawala wa Mohamed Siad Barre.

"Maskini, mwenye njaa hawezi kuhakikisha usalama, [...] jeshi zuri linapaswa kujengwa ambalo ustawi wake unatolewa na ambalo linawajibika," alisema.

Serikali pia bado haijafanya usuluhishi wa taifa, alisema Daud.

"Usalama umehatarishwa kila wakati umoja wa nchi unavunjwa," alisema, akiongeza kwamba pamoja na al-Shabaab, "makabila yenye kinyongo" yanaweza kuwa yanachochea kero kwa baadhi ya maeneo.

Chanzo - sabahionline.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako