If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Sunday, September 1, 2013

Obama kuomba idhini ya bunge kabla ya kuivamia kijeshi nchi ya Syria

Na Flora Martin Mwano

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajia kuomba idhini ya bunge la nchi hiyo ili aweze kufanikisha mkakati wa kuivamia kijeshi nchi ya Syria inayotuhumiwa kwa matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya raia wake.

In deciding to seek congressional approval first, President Obama has effectively delayed a possible military strike against Syria until after Congress reconvenes Sept. 9.
Rais wa Marekani, Barack Obama /MICHAEL REYNOLD/EPA

Kwa mujibu wa katiba ya nchi yake, Rais Obama anayo haki ya kuliagiza jeshi lake kuvamia Syria bila kuomba idhini ya bunge lakini jeshi hilo halitatakiwa kukaa vitani kwa zaidi ya siku 60 ikiwa bunge halikuidhinisha uvamizi.

Bunge la Congress linatarajiwa kupigia kura pendekezo hilo kabla ya tarehe 9 mwezi huu na Rais Obama sasa anasema kuna umuhimu wa kuwa na majadiliano kabla ya hatua za kijeshi kuchukuliwa.

Katika taarifa fupi iliyotolewa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa juma hili kwenye ikulu ya White House, Obama amesema jeshi la Marekani lipo tayari kwa uvamizi ili kumuadabisha Bashar al-Assad kutokana na majeshi yake kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia wa Syria.

Marekani inasema ina uthibitisho kuwa majeshi ya serikali ya Damascus yalitumia silaha hizo katika shambulizi la Agosti 21 pembezoni mwa mji wa Damascus ambapo watu zaidi ya 1,000 walidaiwa kufa.

Serikali ya Syria imekuwa ikikanusha tuhuma zinazoelekezwa kwake na kuwataja waasi kuwa ndio waliotumia silaha za kemikali.


Naye mshirika wa karibu wa serikali ya Damascus, Rais wa Urusi Vladmir Putin ameisisitiza Marekani kuweka hadharani ushahidi wake unaoonyesha kuwa silaha za kemikali zilitumiwa na majeshi ya Assad.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande anaunga mkono pendekezo la uvamizi wa kijeshi na bunge la nchi hiyo linatarajia kupigia kura iwapo wanataka kujiunga na Marekani kwenye oparesheni hiyo.

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa UN waliokuwa nchini humo kuchunguza iwapo silaha za kemikali zilitumika wameondoka mjini Damascus siku ya jumamosi wakiwa na sampuli walizochukua toka eneo la tukio tayari kwa kuzipeleka maabara ili kupata majibu sahihi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako