If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, September 7, 2013

Wakenya wagawanyika kuhusu kura ya wabunge ya kujiondoa kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai

Julius Kithuure alichangia katika ripoti hii kutoka Nairobi

Wakenya wametoa sauti ya kuwa na maoni tofauti kufuatia kura iliyopigwa na watunga sheria Alhamisi (tarehe 5 Septemba) kurejesha mada ya kujiondoa kutoka kwa Mahakama ya Kimataiifa ya Makosa ya Jinai (ICC).

Msimamizi wa mgahawa jijini Nairobi akiangalia matangazo ya habari za moja kwa moja tarehe 5 Septemba za majadiliano kuhusu kujiondoa kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai. [Simon Maina/AFP]

Kura hiyo ya ishara tu haitakuwa na athari kwenye majaribio yanayokuja ya Makamu wa Rais William Ruto na Rais Uhuru Kenyatta, na bunge lazima lipige kura baadaye kuhusu mswada huu ndani ya siku 30 kuweka hatua rasmi kwa ajili ya kujitoa.

Mada ya majadiliano "kusimamisha muungano wowote, ushirikiano na msaada" kwa mahakama kuliidhinidhwa kwa kishindo na Bunge la Taifa kupitia kura ya maoni.

Hadi leo, nchi 122 ni sehemu ya Sheria ya Roma ambayo ilianzisha ICC, na kama Kenya itajitoa ICC itakuwa ni mwanachama wa kwanza wa mahakama hiyo kufanya hivyo.

Wakenya wakitembea nyuma ya jengo la bunge jijini Nairobi tarehe 5 Septemba, tarehe ambayo wabunge walikuwa na mjadala wa kujitoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai [Simon Maina/AFP]

Wabunge wazungumza katika mjadala uliokuwa moto

Katika mjadala uliokuwa moto ambapo wabunge mara kwa mara waliomba kuwepo kwa taratibu wakati walipokuwa wakichangia mada na wakishangiliwa na wenzao, kiongozi wa wengi katika bunge Aden Duale alisema kujitoa kutoka ICC kungelinda katiba ya nchi na kuhifadhi taswira ya Kenya".


"Itaweka hatua kwa ajili ya kufikia mwisho kwa utamaduni wa kutoadhibiwa nyumbani na nje ya nchi kwa pamoja," Duale alisema.

Lakini mbunge wa upinzani Jakoyo Midiwo alisema ilikuwa "siku mbaya kwa Kenya" na kwamba nchi "itakabiliwa na madhara kwa kujitoa".

"Ni ujumbe gani tunaotuma kwa ICC?" kiongozi wa upinzani Francis Nyenze alisema. "Siyo vizuri kwa nchi kuonekana kuwa adui wa mahakama hiyo."

Muungano wa Jubilee wa Kenyatta na Ruto unatawala Bunge la Taifa la Kenya na Seneti, lililo bunge la juu, litajadili mada hiyo wiki ya ijayo.

Kujitoa hasa kutoka ICC kunahitaji uwasilishaji wa maombi rasmi kwa Umoja wa Mataifa, mchakato ambao unaweza kuchukua mwaka mmoja. Hata hivyo, kujitoa kungetoa utangulizi kwa ICC kutofanya uchunguzi na kuendesha mashtaka kwa uhalifu wowote wa baadaye.

"Kujitoa hakutaathiri kwa namna yoyote kesi na mashauri yanayoendelea ," msemaji wa ICC Fadi El Abdallah alisema katika taarifa. "Kura ya maoni au uamuzi wa serikali hautabadilisha jukumu la Kenya chini ya sheria ya kimataifa... ili kushirikiana kikamilifu na ICC katika kesi zinazohusika."

Kisha kesi zinaweza tu kuletwa mahakamani kama serikali inaamua kukubali utawala wa sheria wa ICC au Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupeleka kesi hiyo.

Shirika la Kimataifa la haki za binadamu Amnesty International, lililaani hatua hiyo, likionya kwamba itawanyima Wakenya "moja ya ulinzi muhimu wa haki za binadamu".

"Hatua hii ni mpya kabisa katika mlolongo wa kueneza jitihada za kudhoofisha kazi ya ICC nchini Kenya na barani kote," alisema Netsanet Belay, mkurugenzi wa programu ya Afrika ya Shirika la Haki za Binadamu.

Shirika hilo la haki za binadamu lilitoa wito kwa wabunge "kutetea dhidi ya uhuru wa kutoweza kuadhibiwa na kukataa pendekezo hilo."

"Tunachokiona sasa ni serikali kuahidi kutoa ushirikiano kwa kesi za ICC kwa upande mmoja na kuchukua kila fursa kuishambulia kisiasa ICC na kuidhoofisha kwa upande mwingine," Belay alisema.

Wakenya wajibu
"Ninafikiri maslahi binafsi yameyazidi maslahi ya taifa na Wakenya wataadhibiwa kwa kiasi kikubwa kwa hatua hizo za wabunge zisizo na msingi," alisema mwanasheria wa katiba Suyianka Lempaa. "Kujiondoa katika muungano wa mataifa yaliyoendelea kunaonyesha kwamba unajitayarisha kufanya namna zote za ukatili dhidi ya ubinadamu bila ya kuwajibishwa kwa mtu yeyote yule."

Lempaa alisema Muungano wa Marekebisho na Demokrasia (CORD) wabunge hawakupaswa kutoka nje ya Bunge la Taifa wakati wa mjadala mkali.

"Ni kweli kwamba Wabunge wa Jubilee wana idadi kubwa na walitarajiwa kuidhinisha kwa ushindi hoja lakini wabunge wa CORD wangepaswa kubakia bungeni na kucahngia katika mjadala huo," aliiambia Sabahi.

"Uanachama wa ICC umeridhiwa na nchi 121 zikijumuisha 34 katika Afrika," Lempaa alisema. "Kwa nini Kenya ifanye kazi nje ya mwavuli wa mataifa yaliyoendelea isipokuwa kama inahofia kitu fulani? Nina hisia kwamba hoja hii itaifanya Kenya kuonekana kama nchi iliyotengwa."

Mbunge Stephen Manoti, anayewakilisha jimbo la Bobasi, alieleza sababu yake ya kuunga mkono kujitoa kwa Kenya katika ICC.

"ICC ni mahakama ya ubaguzi wa rangi na inawabagua Waafrika," aliiambia Sabahi. "Tuna mahakama iliyorekebishwa na mahiri ambayo ina uwezo wa kuendesha bila ya shida kesi zote ICC inazodai kutatua."

"Tunajua kujitoa huko hakuna matokeo ya hapo hapo kuhusiana na kesi za sasa zinazowakabili Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake wa Rais William Ruto, lakini kwa faida ya matukio ya baadaye, tunahitaji kuiondoa Kenya kutoka katika ICC ili kulinda uhuru wa Kenya na uadilifu wa viongozi waliochaguliwa," Manoti alisema.

"Nafikiri huko ni kujikinga kutoadhibiwa dhidi ya utawala wa sheria kunakofanywa na wabunge," Gitahi Ngunyi, mwandishi wa kisiasa wa gazeti la The People la Kenya, aliiambia Sabahi.

"Kama Rais Uhuru na makamu wake hawana makosa na weupe kama pamba, kwa nini wabunge watumie usiku kucha kujadili jinsi Kenya itakavyoishinda sheria?" alisema, akiongeza kwamba kujitoa ICC kunatoa ishara mbaya kwamba Kenya ina kitu inachoficha na kinachohofia.

"ICC haiwafuati watu kama hakuna makosa yaliyotendwa," alisema.

Chanzo  - sabahionline.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako