If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, October 16, 2013

Kongo: Daktari Mkongo atunukiwa tuzo ya ushujaa ya 2013

Denis Mukwege, tabibu wa magonjwa ya wanawake raia wa Kongo ametunukiwa tuzo ya ushujaa ya kiraia ya mwaka 2013 kuenzi huduma za kibinadamu anazozitoa katika eneo lililoathiriwa na vita la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Dakta Mukwege alikuwa miongoni mwa wagombea waliopendekezwa kuwania tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2013. 

Tabibu huyo wa magonjwa ya wanawake raia wa Kongo alipokea tuzo hiyo jana kutokana na huduma zake anazotoa katika hospitali ya Panzi, ambayo huwahudumia raia walioathiriwa na vitendo vya ubakaji huko mashariki mwa Kongo.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa jeshi la Kongo na baadhi ya makundi yenye silaha ikiwemo harakati ya waasi ya M23 yamekuwa yakijihusisha na vitendo vya kuwabaka raia huko mashariki mwa Kongo. 


Dakta Denis Mukwege amesema kuwa kitendo cha kuwahudumia wanawake hao wa mashariki mwa Kongo waliobakwa kimebadili maisha yake.

 Amesema kazi yake ya udaktari imemfanya awe shuhuda wa moja kwa moja wa jinai kubwa ambayo ni vigumu kuielewa kikamilifu. 

Amesema hii ni kwa sababu na hapa ninamnukuu" vitendo hivyo vya ubakaji vinawalenga watu adhimu kama mama zetu, wake zetu na watoto wetu." Mwisho wa kumnukuu.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako