If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, October 12, 2013

Maalim Seif : Viongozi wanaowakimbia wapiga kura hawawatendeia haki wananchi

Na Hassan Hamad OMKR

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, amesema viongozi wa majimbo wanaowakimbia wapiga kura wao hawawatendei haki wananchi waliowachagua.

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na wagombea Ubunge wa jimbo la Chambani kupitia CUF, katika uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 26/06/2013

Amesema ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya wabunge na wawakilishi wakiyakimbia majimbo yao baada ya kuchaguliwa, jambo ambalo linaleta sura mbaya na kutowathamini wananchi.

Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametoa changamoto hiyo katika Skuli ya Ukutini jimbo la Chambani, kwenye hafla maalum ya kuwapongeza mawakala wa CUF walioshiriki katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo mwezi Juni, 2013.

Katika hafla hiyo Maalim Seif alimpongeza Mbunge mpya wa Jimbo hilo Yussuf Salim Hussein (CUF), kwa kuanssza kuwapa matumaini wananchi wa jimbo hilo, na kumtaka kuendelea na moyo huo wa kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wowote.

Tangu kuingia madarakani kwa Mbunge huyo miezi mitatu iliyopita, tayari ameshajenga Afisi ya Mbunge pamoja na kuanza matengenezo makubwa ya barabara ndani ya jimbo hilo la Chambani, hali inayowapa matumaini wananchi wa jimbo hilo.


Maalim Seif ametoa wito kwa viongozi wengine wa majimbo kubadilika na kuiga mfano wa Mbunge huyo, ili waweze kutekeleza ahadi za kimaendeleo walizozihidi wakati wa kampeni.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chambani, Yussuf Salim Hussein, ameipongeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kusimamia vyema zoezi la uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.

Amebainisha kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia vyema masuala ya uchaguzi ikiwa itaamua kufanya hivyo, na kuwepo uwezekano wa kufanyika kwa chaguzi huru na za haki katika visiwa vya Zanzibar.

Mbunge huyo pia amelipongeza jeshi la polisi kwa kuonyesha mfano wa kufanya kazi kidiplomasia, na kwamba utaratibu huo utasaidia kuliweka taifa katika hali ya amani na usalama.

Kabla ya hafla hiyo Maalim Seif aliifungua rasmi Afisi ya Mbunge wa Jimbo la Chambani ambayo itakuwa ikifanya kazi wakati wote kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo

Chanzo - ZanziNews 

No comments:

Post a Comment

Maoni yako