Na Bosire Boniface, Garissa
Ukweli kuhusu kiasi cha uwepo wa al-Shabaab na ushawishi katika kaunti ya Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya, ambayo ilionyeshwa katika ripoti iliyovuja ya Shirika la Upelelezi la Taifa (NIS), imewaacha viongozi na wakaazi wa kaunti katika matatizo.

Mwanamke aliyekaa kando ya mtoto aliyejeruhiwa kwenye Hospitali Kuu ya Jimbo la Garissa tarehe 4 Novemba, 2012 baada ya shambulio la guruneti katika kanisa ambalo lilisababisha kifo cha askari polisi mmoja na watu wengine 14 kujeruhiwa. [Stringer/AFP]
"Idadi kubwa ya mashambulio ya kigaidi ambayo Garissa imekumbana nayo ikilinganishwa na kaunti nyingine katika nchi ni uthibitisho kwamba al-Shabaab ni miongoni mwao," Seneta wa Garissa Yusuf Haji aliiambia Sabahi.
"Wakati wa hatua za awali na kwenye kilele cha shambulio, Garissa ilichukuliwa kama makao makuu ya kikundi hiki," alisema, akiongezea kwamba al-Shabaab walihamisha operesheni zao kwenda Kenya baada ya Somalia na vikosi shirika kudhibiti kikundi hicho cha wanamgambo katika ardhi yao ya nyumbani nchini Somalia.
Ripoti ya hali katika kurasa 32 zilizo ndani ya waraka wa NIS, ambayo iliandikwa tarehe 26 Aprili, 2013 lakini ilivuja kwa wananchi baada ya shambulio la al-Shabaab kwenye kituo cha biashara cha Westgate mwezi uliopita, inaelezea ukweli unaosumbua.
Wafanyakazi wa Amniyat, sehemu ya kitengo cha upelelezi cha wasomi cha al-Shabaab, kimechagua Garissa kama "ngome inayopendelewa kwa ajili ya operesheni zao ambapo waliweka miundombinu kuwezesha shughuli zao", kwa mujibu wa ripoti.
"Al-Shabaab wanadhibiti theluthi mbili ya kaunti ya Garissa, hali ambayo inaweza kupanuka kuingia Nairobi," ripoti hiyo ilisema.
Kwa mujibu wa ripoti, wafanyakazi wa Amniyat wameendelea kuingia kwa wingi nchini Kenya -- hususani katika mkoa wa kaskazini mashariki -- na kuwezesha "shughuli za kigaidi kwa kiasi cha kujihusisha na kudhibiti shughuli za kiuchumi, ambapo baadhi yake ni kinyume cha sheria".
"Operesheni za al-Shabaab na 'Amniyat katika mkoa wa kaskazini mashariki zimekuwa uti wa mgongo wa mtandao ambao unasambaza kifaa chenye kulipuka cha kienyeji (IED)/maguruneti na silaha nyingine zinazotumiwa na wafanya ugaidi huko Nairobi na mkoa wa Pwani," ripoti hiyo ilisema, ikiongezea kwamba al-Shabaab pia walitumia upinzani baina ya koo, siasa na nyinginezo katika mkoa kama uficho wa shuguhuli zao za kigaidi.
Historia ya al-Shabaab huko Garissa
Kamishna wa Kaunti ya Garissa Harun Rashid Khator alisema al-Shabaab wamekuwepo huko Garissa kwa muda mrefu, kabla Kenya haijapeleka vikosi kwenda Somalia mwezi Oktoba 2011.
"Walianza kuwepo wakati wa uandikishaji wa mkusanyiko wa vijana kutoka mkoa wa kaskazini mashariki, pamoja na wengine wengi kutoka katika Kaunti ya Garissa," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba vijana wengi wanaoajiriwa wanarejeshwa Kenya baada ya hatua dhidi ya al-Shabaab zilizochukuliwa na vikosi vya Somalia na Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Kutokana na utafiti unaoendelea, mamlaka za kaunti zimekuwa na taarifa kwamba wanachama wa al-Shabaab wanamiliki mali katika kaunti, alisema Khator.
Kati ya 2007 na 2009, kulikuwa na ustawi wa mali na utafutaji wa ardhi, hususan katika mjii wa Garissa, alisema. Wakati serikali ilikuwa ikifanya uchunguzi wa madai kwamba fedha za uharamia zilikuwa zikichochea ustawi huo, kipindi hicho kinaweza kuwa ndio wakati al-Shabaab walipopata ardhi.
"Tumebainisha mali zinazomilikiwa na kikundi hicho. Kutokana na uchunguzi, walipata mali kabla Vikosi vya Ulinzi vya Kenya havijaenda Somalia. Tunachunguza pia mali nyingine kadhaa ambazo kikundi hicho kinadai kumiliki kupitia wakala," alisema.
Aidha, wafanyakazi wa al-Shabaab wamejihusisha katika biashara pamoja na wafanyabiashara wenyeji.
"Al-Shabaab wanamiliki kama wafanyabiashara na wanawasambazia wafanyabishara wa Kenya bidhaa kutoka Somalia," alisema. "Baadhi ya wafanyabiashara wana taarifa ya nani wanaofanya nao kazi lakini wafanyabiashara wengine hawawajui washirika wao."
Kwa sababu Garissa inapakana na Somalia na iko karibu na kambi kubwa ya wakimbizi ya Dabaab, inapaswa kutoshangaa kwamba al-Shabaab wanaiona kaunti hiyo kama msingi, alisema Seneta Haji.
Polisi, viongozi washirikiana
Vikosi vya usalama vya wenyeji vinashirikiana na serikali ya nchi kuwaelimisha wananchi wa Garissa kuhusu hatari ya kuwahifadhi wafanyakazi wa al-Shabaab, alisema.
"Wakaazi wa Garissa wana ushirikiano mkubwa na ni watu wanaopenda amani," alisema Haji. "Hata hivyo, kuna wachache wanaoweza kuwaingiza wafanyakazi wa al-Shabaab. Hawa ndio tunaowatafuta katika mikutano yetu mjini na katika mikusanyiko ya umma kutoa taarifa kwa sababu al-Shabaab hawana rafiki wa kudumu."
Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa dini walisema walikuwa wakiisaidia serikali kwa kuhubiri dhidi ya msimamo mkali.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Kenya huko Garissa Sheikh Abdullahi Salat alisema walikuwa wakijaribu kulipiza kisasi "kuondoa kasumba kwamba wanaweza kuwa wamefanya kwa baadhi ya vijana [kuwafanya waamini] wanapigania sababu za kidini".
"Ni mchakato wa taratibu kubadili imani, lakini tunashukuru serikali ina uvumilivu na maendeleo," alisema.
Alisema kuwa ushirikiano wa jamii na viongozi umepunguza sana idadi ya mashubulizi huko Garissa mwaka uliopita.
Usalama ulioimarishwa
Mkuu wa Kitengo cha Ofisa Polisi Garissa Benjamin Ongo'mbe aliiambia Sabahi kwamba kupitia ripoti za NIS, polisi wamefanikiwa kuzuia mashambulizi mengi ya kigaidi katika mji wa Garissa.
"Tulipata taarifa za mashambulizi kwa kuwasambaza maofisa usalama wengi katika maeneo lengwa au kwa kuwaagiza baadhi ya waendeshaji wa biashara kufunga biashara mapema kwa siku tulizoambiwa," alisema. "Kati ya Juni na hivi karibuni tuliwakamata watu wasiopungua 15 kuhusiana na baadhi ya matukio."
Baadhi ya kesi zimewekwa kando katika Mahakama ya Kaunti ya Garissa, alisema Ongo'mbe, na polisi wameomba kwa mahakama muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wakiwa wamewashikilia washukiwa.
Zaidi ya hayo, polisi wamepata amri ya mahakama kutumia nguvu inapolazimu wakati wa ukaguzi wao ambao angalau dazeni ya maskani wanaminika ama kuwakaribisha magaidi au kutumiwa kama bohari ya silaha.
Hata hivyo baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wamewekwa chini ya uangalizi wa polisi kutokana na ripoti kwamba wanasaidia al-Shabaab, Ongo'mbe alisema.
"Ni kitendo kinachowiyanishwa kwa uangalifu wakati tunaposhughulika na viongozi wa jamii, ambapo baadhi yao wana vyeo vya juu" alisema. "Wanaweza kufanya siasa vita kamili ya ugaidi na kushawishi raia [kuamini] kuwa wanalengwa kwa sababu ya imani yao. Hii ndiyo sababu tunakusanya ushahidi wa kushtakiwa dhidi ya viongozi hao ili tunapopeleka mashtaka tunakuwa na ushahidi."
Source - sabahionline.com



No comments:
Post a Comment