If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, December 27, 2013

Serikali ya Kenya yatoa onyo kwa vituo vya runinga vitakavyozima mitambo yao

Na RFI

Wakaazi wa jiji la Nairobi na viunga vyake nchini Kenya ambao hawana visimbuzi hawataweza tena kutazama Televisheni baada ya serikali kuhamia mfumo wa Digitali usiku wa kuamkia leo.

Uhuru Kenyatta, rais wa Kenya

Vituo vikuu vya televisheni nchini humo vilielekea Mahakamani mapema juma hili kutaka kuahirishwa kwa muda wa kuhamia mfumo huo wa Digitali bila mafanikio kwa kile wanachosema watapata hasara ikiwa hawatashirikishwa katika usambazaji wa mawimbi hayo, na baada ya kupoteza kesi walikataa rufaa ambayo itaamuliwa leo.

Waziri wa Habari na Mawasiliano nchini humo Fred Matiangi amesema kuwa hatua hiyo ya wamiliki wa vyombo hivyo vya habari kutaka kwenda kuahirishwa kwa zoezi hilo si kwa nia njema.

Serikali imeonya kuvichukulia hatua vituo hivyo ikiwa vitazima mitambo yake kama ilivyofanya siku mbili zilizopita.

Mpango wa kuhamia Digitali utakamilika nchini humo mwezi Juni mwaka ujao.

Awali vituo vitatu vikubwa vya televisheni nchini Kenya vilizima mitambo yao baada ya Mahakama Kuu nchini humo kutoa uamuzi kwamba vinapaswa kuingia katika mfumo wa utangazaji wa dijitali na kuachana na mfumo wa analojia.

Vituo hivyo vya Standard Group, Nation Media Group na Royal Media Services, awali vilikwenda mahakamani kuomba kuahirishwa muda wa kuhamia kwenye mfumo huo, hadi masuala kadhaa yatakapofafanuliwa.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako