If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, February 20, 2014

Je, haki itatendeka katika kesi inayomkabili Kenyatta ya uhalifu dhidi ya ubinadamu..?

Na Julius Kithuure, Nairobi

Huku kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai imeahirishwa kwa muda usiojulikana, watu wa Kenya wanatoa maoni mbalimbali kuhusu mwelekeo na namna nzuri ya kuona haki ikitendeka.

Mwandanamaji wa Kenya akiangalia picha za vurugu za baada ya uchaguzi wakati wa maandamano huko Nairobi mwaka 2011. [Simon Maina/AFP]

Ingawa kuna maoni tofauti, karibia kila mmoja ana kitu cha kusema kuhusu hili. Baadhi wanaunga mkono uahirishaji huo wa kesi hiyo, wakati wengine wanasema waendeshaji kesi wa ICC wanapaswa kustahimili. Wengine bado wanatoa wito kwa njia mbadala wa Kenya badala ya mahakama ya kimataifa.

Kesi dhidi ya Kenyatta katika ICC imekuwa na vizuizi mbalimbali kutoka ilipoanza, huku mashahidi mbalimbali wakiondoa ushahidi wao na madai kuwa ushahidi umechafuliwa na pande zote za kesi. Katika mwezi wa Disemba, Mwendesha Mashtaka wa ICC Fatou Bensouda alikiri kwamba hakuwa na ushahidi wa kutosha kumshtaki Kenyatta kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 hadi 2008, na mnamo tarehe 23 Januari timu ya waendesha mashtaka iliomba kuahirisha kesi hiyo kwa muda usiojulikana.

Kenyatta ana masuala 'muhimu zaidi' ya kuzingatia

Wanaomuunga mkono Kenyatta wasema uendeshaji mashtaka unakosa ushahidi mzito na kuondolewa kwa ushahidi muhimu kumedhoofisha kabisa kesi hiyo.

Picha iliyochukuliwa tarehe 8 Aprili, 2011, ikionyesha Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Uhuru Kenyatta wa wakati huo (wa pili kushoto) kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai. [AFP]

"Ni wazi kwamba sasa kesi dhidi ya raisi huyu ni yenye kasoro na yenye kiasi kidogo cha uuaji," mbunge wa Juja Francis Munyua Waititu aliiambia Sabahi. "Basi ni kwa nini rais apoteze nguvu zake, muda na rasilimali kwa suala ambalo halina kichwa wala mkia?"


Waititu alisema Kenyatta ana masuala muhimu zaidi ya kuzingatia kama vile mapambano dhidi ya al-Shaabab, kuanzisha miradi ya maendeleo na kusimamia mpito kuelekea kwenye mfumo wa ugatuizi wa utawala.

"Kuburuza jina la rais aliyechaguliwa kidemokrasia wa nchi ya kidemokrasia inayoheshimika katika matope kwa tuhuma za uongo za kufanya uhalifu dhidi ya ubinadamu, hata hivyo, hakuna ushahidi halisi, ni kutukana mchakato mahakama," alisema mwanasheria mwenye makaazi Nairobi Aomo Kelly wa Odiwuor, Aomo Kelly & Associates Advocates.

"Ni matumaini yangu kwamba mwendesha mashataka akiri kuwa amerithi kesi dhaifu kutoka kwa mtangulizi wake", aliiambia Sabahi. "Lakini muda utafika wa kuhitimisha sarakasi hii na kuomba msamaha Wakenya na jumuiya ya kimataifa kwa kutupeleka kwenye njia isiyofaa."

Uahirishaji wa hivi karibuni unampa Bensouda miezi mitatu ya kukusanya taarifa za ziada, ikiwa ni pamoja na ripoti ya fedha ya Kenyatta, ambayo waendesha mashtaka wanakiri kwamba inaweza bado isitoe ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi hiyo.

"Kadri kesi hii itakavyoendelea muda mrefu katika hali ya kutokuwa na uhakika, ndivyo hivyo itaondoa sifa ya ICC na kudhoofisha hadhi yake kidunia," alisema Anthony Githendu, mkuu wa mauzo katika taasisi ya Kenya Institute of Management

"Jambo halisi la kufanya wakati mwendesha mashtaka anapokiri kwamba hana ushahidi usiopingika dhidi ya mshukiwa ni kutupilia mbali mashtaka na kuacha majaji kumtoa hatiani mshukiwa na siyo kutafuta muda wa ziada kukusanya ushahidi zaidi," aliiambia Sabahi.

Waathirika wanatafuta haki kwa njia zozote
Hata hivyo, wanaounga mkono kesi hii dhidi ya Kenyatta wasema haki lazima ipatikane licha ya nani anayeshtakiwa.

"Kama baba wa kijana wa kiume aliyeuawa na kikundi katika vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007 hadi 2008, nimesubiri haki isiyopatikana kwa urahisi kwa miaka zaidi ya mitano," alisema Joseph Otieno, mwenye umri wa miaka 61, muuzaji wa mkaa katika makazi duni ya Kibera huko Nairobi.

"Sasa, kwa kuwepo mazungumzo ya kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha, mashahidi walifundishwa, hatua za kuunganisha ushahidi zilidanganywa, pamoja na istilahi za kisheria, nina wasiwasi kuwa tumaini dogo nililonalo litafutika kama kesi ya Kenyatta itaachwa," aliiambia Sabahi.

Ingawa Otieno anasema bado haijathibitshwa iwapo Kenyatta ana hatia au hana hatia, kesi ya ICC inampa tumaini.

"Kuwaepo kwa kiongozi mkuu mahakamani kunanitia moyo kuwa kijana wangu atapata haki," alisema. "Inanipa pia matumaini kwamba mfumo wa haki bado vinafanya kazi, ingawa taratibu kidogo."

"Amani na usalama wa muda mrefu wa nchi unategemea hitimisho la kesi za ICC," alisema.

Suluhisho la Kikenya?
Bado wengine wametoa mbadala wa tatu: mfumo wa ndani ya nchi iliyo nje ya mamlaka ya kisheria ya ICC. "Sasa ICC haina uwezo wa kutatua kitendawili cha nani alisababisha vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi, basi turejee na kutafuta suluhisho litakalotolewa na Wakenya kuhusu tatizo hilo," alisema mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Onyonka.

"Basi tuendelee kutoka walipoachia ICC na kuanzisha mfumo wa haki wa ndani," aliiambia Sabahi. "Kimsingi, nina furaha kwa sababu mahakama ni mfumo wa haraka wa kufuatilia uanzishaji wa Kitengo cha Uhalifu cha Kimataifa, mahakama maalumu yenye mamlaka kama hayo ya ICC kushughulikia uhalifu dhidi ya ubinadamu."

Henry Muthee, mkulima mdogo mwenye umri wa miaka 56, huko Naivasha ambaye alimpoteza binamu yake katika vurugu hizo, alisema njia nzuri kuponya majeraha ya Wakenya "ni kwa serikali kuweka mahakama ya ndani ambayo itamhukumu kila mkosaji wa vurugu hizo ambaye kimsingi ni zaidi ya washukiwa watatu wa ICC".

"Na kwa sababu haki ya kutoa usalama kwa raia ni kazi ya serikali, hatimaye inapaswa kuwafidia waathirika wa vurugu bila masharti," Muthee aliiambia Sabahi.

Lakini Margaret Macharia, mwenye umri wa miaka 52, ambaye anaendesha duka dogo la vitabu ambaye alipata shida wakati wa vurugu huko Eldoret, mji ulioko kilometa 320 nje ya Nairobi, alionyesha wasiwasi kwamba suluhisho litakalotolewa na Wakenya halitakuwa la haki.

"Kama ICC pamoja na nguvu zake inazotumia haiwezi kuwakamata waliowajibika na vurugu hizo, kisha wanarejesha suala hilo katika mamlaka ya kisheria ya Mahakama ya Kenya wanafunga ukurasa huo kwa pamoja," alisema Macharia, ambaye anauza mitumba ya nguo katika soko la Gikomba huko Nairobi.

Aliihimiza mahakama kuwapuuza mashahidi waliodanganya na wale waliotoa ushahidi wa uongo kwa sababu kesi haitegemei shuhuda za dazeni za mashahidi walijiondoa lakini "mamia ya wengine waliotoa ushahidi".

"Majaji wa ICC waachwe ili waamue kama kuna ushahidi wa kutosha kumhukumu Kenyatta bila kupingwa na bila kuwa na msukumo unaozingatia hali yake ya juu maishani," alisema.

Samehe na sahau
Irungu wa Ndirangu, dereva teksi mwenye umri wa miaka 44, katika eneo la Zimmerman mjini Nairobi, alisema kwa kuwa Kenyatta alichaguliwa, kisha watu wakamuona hana hatia kupitia kupiga kura kwao.

"Tunapaswa tusameheane na kusahau yaliyopita," alisema Ndirangu, akiongeza kwamba kesi hii inapaswa kuahirishwa wakati Kenyatta akiwa madarakani. "Hakuna mkuu wa nchi anayepaswa kukabiliwa na mashtaka akiwa madarakani kwa sababu uamuzi wa hatia utaiyumbisha nchi."

Lakini Jerry Kenyansa, mwenyekiti wa taifa wa Counties Commuter Welfare Association (COCOWA), alisema kwamba ikiwa Kenyatta hana hatia, hapaswi kuwa na hofu kushirikiana na ICC.

"Rais Kenyatta hapaswi kuachiwa bado hadi atakaposhirikiana vya kutosha na waendesha mashtaka wa ICC," aliiambia Sabahi. "Kama Kenyatta hana la kuhofia au kuficha, anapaswa kuwaruhusu waendesha mashtaka wa ICC bila kuwazuia katika akaunti zake za benki kwa sababu wanatuhumu kwamba alitoa fedha nyingi kwa wafuasi waliokuwa wakiwalipa waliohusika na vurugu hizo."

Serikali ya Kenya inapaswa pia kuwajibika kwa ucheleweshaji wa kesi ya Kenyatta, alisema.

"[Serikali] inapaswa … kuisaidia ICC kwa ushahidi wa muhimu ilio nao dhidi ya Bw. Kenyatta, badala ya kujificha chini ya uhuru wa nchi," alisema Kenyansa.

Kusubiri kwa muda
Sheila Mugambi, aliyepo katika mafunzo ya daktari wa meno katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, alisema kuna uwezekano wa haki kutotendeka maadamu Kenyatta yupo madarakani.

"[Kenyatta] anasimamia jeshi la Kenya, anaidhibiti polisi, anausimamia upelelezi na ana utajiri mwingi," alisema. "Kutokana na historia hii, haiwezekani kwa mashahidi kutoa ushahidi kwa uhuru dhidi ya mshukiwa mwenye nguvu kubwa."

"Ni vizuri kusubiri hadi mshukiwa akiwa si mkuu wa nchi tena," aliiambia Sabahi. "Nitafurhaia pia ikiwa majaji wataagiza uchunguzi mpya kuamua iwapo Kenyatta na vyombo vya serikali waliwatishia mashahidi kwa siri ili waondoe au wabadili ushahidi au kuwahonga kubadilisha mawazo yao."

Kenyatta aliahidi wakati wa kuapa kama rais mwezi April 2013 kuwa atashirikiana na ICC ili kusafisha jina lake.

"Ninashangaa kilichompata na kumfanya abadili mawazo yake ghafla," alisema Mugambi. "Hili limenisababisha kukisia kwamba wenye hatia wakati wote wanaogopa."

No comments:

Post a Comment

Maoni yako