Msafara wa Mhe. Mwakilishi Mpya wa Jimbo la Kiembesamaki ukiingia katika viwanja Baraza la Wawakilishi kumshindikiza kwa ajili ya kuapishwa leo asubuhi.
Gari iliomchukuwa Mhe. Mahmoud Thabit Kombo likingia katika viwanja vya Baraza leo asubuhi kwa ajili kuhudhuria kuapishwa na kushiriki katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea kujadili Ripoti za Kamati za Baraza Zinazowakilishwa na Wenywviti wa Kamati hizo.
Mhe. Mwakilishi Mteule akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani tayari kwa kuapishwa Rasmin kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar,akishindikizwa na Mwakilishi wa Jimbola Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira na katikati Mwakilishi wa Bububu Mhe Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) wakimshindikiza katika ukumbi wa Mkutano kwa ajili kuapishwa
Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho akiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuaza kwa taratibu za shughuli za Kikao na kumapisha Mwakilishi Mpya wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. wakati wa Kikao cha asubuhi leo.
Mhe. Spika Pandu Ameir Kificho akisoma Dua kabla ya kuaza kwa Kikao cha Baraza cha Asubuhi leo.
Wanafamilia ya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakihudhuria sherehe za kuapishwa kwake leo asubuhi katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wanawake wakimshindikiza Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiingia katika ukumbi wa Mkutano tayari kwa kuapishwa kwake kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Waheshimiwa Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Mwakilishi wao wa Jimbo la Kiembesamaki wakati akiapishwa katika ukumbi wa Mkutanona Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho leo asubuhi.
Mhe Mhmoud Thaib Kombo, akiapishwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi kuwa Mwakilishi wa Jimbola Kiembesamaki, baada ya kushinda Jimbo hilo na kuwa Mwakilishi Mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia kuapishwa kwa Mhe. Mahmoud Thaib Kombo, baada ya kushinda uchaguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akitia saini baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Kiembesaki Zanzibar kwa kupata ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika wiki iliopita.
Mhe. Spika wa Baraza la Mapinduzi Pandu Ameir Kificho akimkabidhi Vitendea Kazi vya Baraza la Wawakilishi Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.



No comments:
Post a Comment