If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, February 18, 2014

Polisi wapongeza kupunguza ufalifu

Na Kija Elias, Moshi.

SERIKALI imelipongeza jeshi la polisi kwa kupunguza uhalifu wa kimataifa kufikia asilimia 1.1 tofauti na ilivyokuwa mwaka 2012.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, alitoa pongezi hizo wakati akifungua mkutano mkuu maafisa wandamizi wa jeshi la polisi, uliofanyika ukumbi wa chuo cha polisi Moshi.

Alisema pamoja na Tanzania kutajwa kuongoza katika utekelezaji wa maazimio ya mikakati ya kukabiliana na uhalifu wa kimataifa kati ya nchi wanachama wa INTERPOL, kuongezeka kwa matukio ya uhalifu wa mitandao na uhalifu wa kimataifa, ni moja ya changamoto zilizokuwa zikichafua sura ya taifa kimataifa.

Alisema ushirikiano huo umesaidia kuongeza imani kwa wananchi na vyombo vya dola, imani ambayo haitokani na matumizi ya nguvu dhidi ya wahalifu, bali limewezeshwa kwa kiasi kikubwa kwa utekelezaji wa sheria ya ugaidi ya mwaka 2002 na sheria ya fedha chafu ya mwaka 2006.

Hata hivyo, alisema kuna viashiria mbalimbali vinavyoonesha kuongezeka kwa aina hizo za uhalifu na kutolea mfano wa ongezeko la fedha chafu zinazopatikana na hutumika kutanua mitandao ya kihalifu kitaifa na kimataifa.


Aidha aliongeza kuwa jeshi la polisi linapaswa kuongeza ushirikiano ili kurudisha imani kwa wananchi na vyombo vya dola.

Kwa upande wake Mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP Ernest Mangu,alisema jeshi lake limejiandaa ipasavyo kukabiliana na vurugu ambazo zinazojitokeza hususani nyakati za uchaguzi.


Alisema wakati nchi ikijiandaa na mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya suala la amani, usalama na utulivu ni moaj ya vipaumbele ambavyo jeshi lake imejipanga kulishughulikia.

Chanzo: ZanziNews

No comments:

Post a Comment

Maoni yako