If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, February 4, 2014

Tuzungumze Toleo la nne “Majungu na Maendeleo”



By Jessica Kamala-Mushala & Bernadeta Kaiza

Tunapenda kuwakaribisha ndugu wasomaji kwenye toleo la nne“TUZUNGUMZE”. Katika toleo letu la tatu tulihitimisha ya kwa swali :” Je sisi tunajitambulishaje kama watanzania waishio ughaibuni?”.

Tulitoa hamasisho la utafiti binafsi wa kuchambua na kutambua ni vigezo gani vinavyotufanya sisi tuwe tofouti na mataifa mengine. (What makes us unique and stand out as Tanzanians)

Tuzungumze nini Leo? Leo tunagusia Majungu katika jamii and its impact on social relations and community development. Je majungu ni nini?

Mchangiaji #1 Majungu ni mazungumzo ya mtu au watu yenye nia ya kuharibu sifa au maendeleo ya mtu, watu au kikundi. Mara nyingi hutokana na kumwonea mtu wivu hasa yule mwenye, uzoefu, maendeleo au nafasi katika jamii. Majungu hutokea mara nyingi kwenye vikundi na makazini.

Mchangiaji #2” Hatuwezi kuongelea Maendeleo which is a product of fikra safi isiyo na hiyana” bila kukubaliana majungu ni nini katika mjadala huu.

Mchangiaji #3 Naona Maendeleo ni matunda yanayotokana na fikra sahihi na yenye elimu na uboreshaji wa jamii.

Matunda ya uboreshaji yaweza kuwa mali halisi (tangible assets) kama barabara, huduma bora za afya, elimu n.k. Lakini katika jamii inaweza ikawa Ushirikiano au upendo wa kuinuana. Maendeleo ni kukua kwa fikra au uchumi wa mtu au jamii.

Mchangiaji #1: Basi tukubaliane Majungu ni fikra potofu zenye kurudisha maendeleo nyuma. Na kama ni hivyo kwa nini yameendelea kuwepo?

Mchangiaji #3: Jamani palipo na watu zaidi ya mmoja hasa kwenye vikundi, mazungumzo yaweza kuwa chanzo cha kupika majungu dhidi ya mtu hasa ikiwa wana mahusiano, fikra potofu au mawazo mgando juu ya anayezungumziwa. Swali linakuja Je majungu yaweza kuwa ukweli? Mhh!!

Mchangiaji #2: Majungu ni ukweli wa mbali unaokuzwa kupita kiasi ili kujiridhisha na kuchafua hali ya hewa kwa wengine akisimamisha mawazo yake kwenye jamii.

Ukimuhuliza ushahidi atasema “we niamini, kama hauamini shauri yako jaribu ukome” Planting a negative seed enough to turn peoples opinion and preferences.

Asiye mkosaji ni nani? Ili kusonga mbele kimaendeleo yabidi patokee mtu mwenye kujadili, kuelimisha na kubadili mwelekeo wa majungu kuwa wa kujenga jamii yenye maendeleo.

Mfano wa majungu:Ahh Huyu namfahamu hanauwezo wa kuanzisha biashara Marekani** Majadiliano yaendelea…… Kwani hela katoa wapi, kwanza hana kazi, pili hana uzoefu…… n.k

Mchangiaji #4: Ndio maana watu wengine kwa makusudi kabisa ya kuogopa majungu, wanapendelea kijikalia kivyao badala ya kujichanganya na Watanzania ughaibuni-USA. Je Watanzania wenzangu hiyo ni dawa ya majungu? Au ni woga?

Tujiulize Je sisi ni chanzo, mwendelezo wa majungu, wapendaji au wasukumaji gurudumu la maendeleo? Tuendelee kuelimishana wandugu!


No comments:

Post a Comment

Maoni yako