If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, March 28, 2014

Serikali ya Somalia, ASWJ walumbana juu ya ujumuishwaji wa wanamgambo kwenye SNA

Na Hamdi Salad, Mogadishu

Serikali ya Somalia inakabiliwa na upinzani kutoka Ahlu Suna wal Jamaa (ASWJ) baada ya pande hizo mbili kutokufikia makubaliano juu ya kuviunganisha vikosi vyao kwenye kampeni ya kijeshi inayoendelea sasa dhidi ya al-Shabaab mkoani Galgadud.

Wanajeshi wa Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) wakiwa wamekaa kwenye lori mjini Qoryooley baada ya operesheni iliyofanikiwa kwenye Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia kuukomboa mji huo kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabaab siku ya tarehe 22 Machi 2014. [PICHA YA AFP / AU UN IST / TOBIN JONES]

Uhusiano kati ya serikali na wanamgambo hao wanaoshirikiana na serikali yalianza kuzorota mwishoni mwa mwaka jana juu ya ahadi ambazo hazikutekelezwa, naibu mwenyekiti wa kamati tendaji ya ASWJ, Sheikh Ahmed Abdullahi Ilkaase, aliiambia Sabahi.

Wakati operesheni ya jeshi la serikali ilipokaribia kwenye maeneo yanayodhibitiwa na ASWJ, serikali ilituma ujumbe mjini Dhusamareb, mji mkuu wa mkoa wa Galgadud, mnamo tarehe 19 Machi kuwaomba ASWJ kupigana chini ya Jeshi la Taifa la Somalia sambamba na Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini humo (AMISOM).

Lakini ujumbe huo, akiwemo Waziri wa Ulinzi Mohamed Sheikh Hassan Hamud, Wazri wa Usalama wa Taifa Abdikarim Hussein Guled, Waziri wa Habari Mustafa Ali Duhulow, na Waziri wa Mambo ya Ndani na Masuala ya Shirikisho Abdullahi Godar Barre ulikumbana na upinzani kutoka upande wa ASWJ, ambao unahisi ulikosewa kwenye makubaliano ya usalama yaliyopita.

"[Mawaziri hao] walitwambia tuachane na jina na uongozi wetu na wapiganaji wetu wapigane chini ya serikali ingawa bado hawajatekeleza makubaliano ya awali yaliyofikiwa Abudwaq kati yetu na serikali," Ilkaase alisema. "Kwa hivyo, tuliyakataa."


Kutoka kushoto kwenda kulia: Waziri wa Ulinzi Mohamed Sheikh Hassan Hamud, Waziri wa Usalama wa Taifa Abdikarim Hussein Guled, Waziri wa Habari Mustafa Ali Duhulow, na Waziri wa Mambo ya Ndani na Masuala ya Shirikisho Abdullahi Godar Barre wakiwasili kwenye Divisheni ya 21 ya SNA wilayani Dhusamareb tarehe 19 Machi 2014. [Hamdi Salad/Sabahi]

Hata kwenye mapigano ya karibuni kabisa ya AMISOM kuukomboa mji wa El Bur, ASWJ ilikataa kushiriki, alisema Ilkaase.

"Hatukuweza kufikia makubaliano na serikali juu ya namna wanajeshi (wetu) watakavyoweza kushiriki," alisema. "Serikali inatazamia wanajeshi wa ASWJ [kushiriki] chini ya jina lake ingawa wanajeshi hawapati mafao yoyote kutoka serikali hiyo, ambapo sisi tunataka kushiriki kwenye vita tukitumia jina letu wenyewe.

Ahadi zisizotekelezwa
Chini ya makubaliano yaliyofikiwa mwezi Machi 2013, pande hizo mbili zilikuwa zimekubaliana kushirikiana kwenye masuala ya usalama na utoaji wa huduma.

"Wakati huo, tulitimiza makubaliano yetu na serikali na kukabidhi udhibiti wa wanajeshi 700 ambao sasa wamewekwa kwenye Divisheni ya 21 ya SNA [mjini Dhusamareb]," alisema, akiongeza kwamba makabidhiano hayo ilikuwa sehemu ya mpango mkubwa wa hatimaye kuwahamishia wanamgambo wote wa ASWJ serikalini.

Lakini Ilkaase aliishutumu serikali kwa kutokutimiza sehemu yake ya makubaliano na kushindwa kuwalipa mishahara wanajeshi hao. "Serikali ya shirikisho imekuwa ikilipia chakula tu cha wanajeshi, na hawajapata mshahara wowote," alisema juu ya wanajeshi wa ASWJ ambao tayari wamejumuishwa jeshini.

AWSJ pia ilitarajiwa kupata msaada wa kulipa madeni ya wanajeshi wake waliokuwa wakipigana na al-Shabaab, ambayo yalifikia dola milioni 5 tangu mwaka 2009, alisema. Vile vile, serikali ilikuwa imeahidi kutoa huduma kwa mayatima na waliopata ulemavu katika mapambano ya muda mrefu ya ASWJ kuikomboa mikoa ya kati ya Somalia kutoka kundi hilo la wanamgambo, alisema.

Ikiwa makubaliano ya awali hayakutimizwa na serikali, Ilkaase alisema wapiganaji 1,800 waliobakia kuhudumu chini ya ASWJ hawatajumuishwa kwenye jeshi la taifa lakini wataendelea kufanya kazi peke yao kwa msaada kutoka kwa jamii.

"Tuna uwezo wa kufanya kazi na kuwatoa askari hao shukrani kwa fedha zilizokuzwa na umma, wafanya biashara na watu wanaoishi nje," alisema. "Baada ya sisi kupokea [fedha] tunazisambaza kwa askari, na muda uliobakia [wanaendelea kutumikia kwa sababu] wao ni wazalendo."

Hata hivyo, Kamanda wa Divisheni ya 21 Kanali Sulub Ahmed Dirie na Waziri wa Ulinzi Sheikh Hassan Mohamed Hamoud wanakanusha madai ya Ilkaase, kwa kusema kwamba askari wote katika kambi ya kijeshi ya Dhusamareb walipokea mishahara yao.

Serikali imekuwa ikiwapa askari wa ASWJ mishahara yao kutoka siku waliyowekwa kambini, Hamoud aliiambia Sabahi.

"Tulipendekeza kwa ASWJ kuwa vikosi vyao na vile kutoka kwa serikali vingefanyakazi chini ya bendera ya serikali, na kujiunga na vita pamoja na serikali na AMISOM," Hamoud alisema, akikataa kutoa maoni shutuma zaidi kuhusu shutuma za ASWJ.

Sabahi pia iliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Ndani na Shirikisho kujibu shutuma kutoka ASWJ, lakini wao walikataa kutoa maoni.

Serikali, ASWJ wanahitaji kuelewana
Mazungumzo kati ya ASWJ na serikali hayana ukweli na hakuna upande wowote unazingatia ukweli uliopo sasa, alisema Kanali Abdullahi Adamu Irro, askari wa zamani wa polisi na vikosi vya kijeshi vya Somalia chini ya serikali ya Mohamed Siad Barre.

"Serikali ingepaswa kuteua kamati ya ufundi ya kushughulikia suala hilo na kusafisha njia kwa ajili ya majadiliano ya mafanikio, badala ya Mawaziri kwenda kwa Ahlu Sunna na kuharakisha, kuwauliza ASWJ kufanya kazi chini ya jina la serikali," aliiambia Sabahi.

"Serikali ingepaswa kuheshimu makubaliano iliyofikia awali pamoja na ASWJ," alisema. "Sio sahihi kwao kushinikiza [ASWJ] kupambana chini ya serikali bila kutimiza sehemu yao ya mpango huo."

Kwa upande mwingine, ASWJ ingeahirisha kwa serikali katika masuala ya utawala na masuala ya kijeshi, Irro alisema.

"ASWJ walikubaliana kuwa na kambi ya 21 ufunguliwa upya kwa askari wake kuwekwa huko na pia walikubalika uteuzi wa utawala wa [Dhusamareb] na serikali," alisema. "Kwa hiyo, ASWJ hawana msingi wa kudai kwamba askari wa kikanda lazima wafanyekazi chini ya jina lake."

Alisema ni muhimu kwa pande zote mbili kufikiria hali zilizopo ili Mazungumzo yaweze kufanikiwa.

"ASWJ inapaswa kuzingatia hali ngumu iliyonayo serikali, na serikali inapaswa kufikiria jukumu la ASWJ lililotekeleza katika vita kupambana na al-Shabaab," alisema.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako