Na Rajab Ramah, Nairobi na Hamdi Salad, Mogadishu
Kukabiliana na ongezeko katika mashambulio yasiyozuiliwa na yaliyopangiliwa vizuri nchini Kenya, wanasiasa, wachambuzi sawa na raia wamechangia katika mjadala mkali kuhusu iwapo Vikosi vya Ulinzi vya Kenya (KDF) vijiondoe nchini Somalia.

Mwanachama wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya akiwa kwenye lindo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kismayu 2012. [AU-UN IST PHOTO / TOBIN JONES]
Wito wa hivi karibuni uliotolewa na wanasiasa wa Kenya kwa serikali kuwasilisha mpango wa kujitoa ni inalingana na maoni ya miongoni mwa watu wa Kenya waliochoswa juu ya gharama ya kibinadamu ya kupambana na al-Shabaab. Lakini wachambuzi kutoka Kenya na Somalia watahadharisha kwamba kuondoa vikosi vya Kenya kutoka kwenye Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) ni kutoona mbali na ushauri mbaya.
Kutolewa kwa wito wa kujitoa
"Katika jaribio letu la kumsaidia jirani tumepata shida sana -- gharama kuanzia kwenye kupoteza watu na upotevu wa fedha," alisema kiongozi wa wachache katika baraza la mawaziri Moses Wetangula. "Sasa umefika wakati wa kupanga kama nchi kuhitimisha uwepo wetu nchini Somalia na kuokoa nchi yetu kuondokana na mgogoro zaidi."

Askari kutoka kikosi cha Kenya cha Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) wakati wa kusonga mbele kuingia katika jiji la bandari la Kismayu la Somalia mwaka 2012. [AU-UN IST PHOTO / STUART PRICE]
"Sisi katika Muungano wa Mageuzi na Demokrasia [chama cha upinzani] tayari tumeiandikia serikali kuomba kwamba wanatutoa sisi na nchi pia pamoja na mpango wa kuondoa vikosi vya Kenya ndani ya nchi ya Somalia," aliiambia Sabahi.
Wetangula alisema mkakati wowote wa kuondoka unapaswa kujumuisha kutoa mafunzo kwa jeshi na polisi wa Somalia na kushirikiana na wabia wa maendeleo kusaidia Somalia kufikia siku njema sijazo .
Ronald Tonui, mwanachama wa chama cha Jubilee ambaye anawakilisha jimbo la Kati la Bomet katika Bunge la Taifa, alisema anapanga kuwasilisha hoja katika bunge baada ya tarehe 3 Juni, wakati wabunge watakaporeja kutoka mapumziko, kuondoa vikosi vya Kenya nchini Somalia.

Vikosi kutoka kikosi cha Wakenya cha Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) wakiwa wamekaa nyuma ya lori la jeshi kuelekea mji wa bandari wa Kismayu mwaka wa 2012. [AU-UN IST PHOTO / STUART PRICE]
Ronald Tonui, mwanachama wa chama cha Jubilee ambaye anawakilisha jimbo la Kati la Bomet katika Bunge la Taifa, alisema anapanga kuwasilisha hoja katika bunge baada ya tarehe 3 Juni, wakati wabunge watakaporeja kutoka mapumziko, kuondoa vikosi vya Kenya nchini Somalia.
"Haileti mantiki kwamba vikosi vyetu vinajaribu kudumisha amani nnchini Somalia kwa gharama ya usalama wa Wakenya," Tonui aliiambia Sabahi. "Tumebakia kwenye milipuko ya kigaidi kutoka tulipochukua jukumu nchini Somalia mwaka 2011. Ni wakati sasa wa kuhitimisha kwa ajili ya amani ya nchi yetu."
"Mfululizo wa mashambulio tuliyokumbana nayo kutoka kuanza kwa [operesheni] ya KDF nchini Somalia yamekuwa na madhara makubwa katika uchumi wetu, hivyo kurudidsha nyuma mpango wa maendeleo yetu kama nchi," alisema.
"Kwangu mimi, mapambano haya pekee hayana faida," alisema. "Afadhali [tungetajwa] kuwa waoga lakini [kuhakikisha] raia wetu wako salama kuliko kuonekana jasiri wakati taifa lote linatishwa na mashambulio yasiyokwisha."
Mary Okoth, mwenye miaka 40, muuza maua katika maeneo ya jirani ya Westlands Nairobi, alisema hakukuwa na mantiki kwa Kenya kuendelea kujihusisha nchini Somalia kutokana na kuongezeka kwa hali isiyo na uhakika ya usalama nyumbani.
"Msemo wa zamani unasema kwamba hisani huanzia nyumbani," aliiambia Sabahi. "Huwezi kukimbia na ndoo ya maji kuzima nyumba ya jirani wakati nyumba yako mwenyewe inaungua moto. Nafikiri nguvu inapaswa kuja nyumbani na kuondoa machafuko hapa kabla ya kufikiria kujihusisha kokote kimataifa."
'Serikali haitaruhusu magaidi kutulaghai'
Licha ya wito wa kujitoa na uungaji mkono unaoongezeka wa kurudisha vikosi nyumbani, serikali ya Kenya imesema kwa msimamo ulio wazi hilo sio chaguo.
"Serikali haitawaruhusu magaidi kutuamrisha au kutulaghai katika kubadili sera yetu ya ndani au ya kigeni," Makamu wa Rais William Ruto aliwaambia waandishi tarehe 5 Mei, siku chache baada ya mfululizo wa mashambulizi ya mauaji huko Nairobi na Mombasa ambayo yaliua watu sita na kujeruhi kadhaa.
"Hatutajitoa hadi Somalia itakapokuwa imara na usalama wa kutokuwa na ugaidi," alisema, akisema kuwarudisha nyumbani wanajeshi wa Kenya kutoka AMISOM kutaleta kimbilio salama kwa al-Shabaab, ambako kutaleta tishio kubwa la usalama kwa Kenya na kanda nzima.
"Ulinzi wetu wa pamoja ni jukumu la pamoja; kila mtu lazima atimize wajibu wake katika kudumisha uangalifu wa dhati," Ruto alisema. "Mamlaka zote za serikali lazima zitimize wajibu wake kikamilifu na kila raia lazima atimize wajibu wake wa uzalendo."
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa Elias Bare Shill alipuuza wito wa kujiondoa.
"Mapendekezo ya kujitoa kwa vikosi hayajulikani yalipo," aliiambia Sabahi. Ukweli, alisema kamati yake ya bunge "ingependa kuunga mkono juhudi yoyote ya kuongeza wanajeshi."
Bila ya kutoa idadi maalumu, Shill alisema mzigo wa fedha kwa Kenya kwa kuwa na wanajeshi wa KDF nchini Somalia ilikuwa tofauti na ilivyochukuliwa na wananchi kwa sababu asilimia kubwa inachukuliwa na AMISOM na kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.
"Pia inapaswa kuzingatiwa kwamba sababu kuu ambayo ilitupeleka Somalia ilikuwa kuepuka mashambulizi zaidi kwa kuwa kikundi kichafu cha wanamgambo kimeendelea kufanya mashambulizi na utekaji ndani ya eneo la Kenya," alisema.
Shill alisema Kenya inapaswa kukaa Somalia kumaliza walichokianza, kuwatokomeza al-Shabaab kabisa.
Kujitoa kwa KDF kutakuwa 'maafa'
Simiyu Werunga, kepteni mstaafu wa Kenya na mkurugenzi wa Kituo cha Usalama na Mafunzo ya Kimkakati Afrika huko Nairobi, alisema kujitoa hakutakuwa tu maafa kwa Wasomali lakini pia kwa kanda nzima.
"Kujitoa kunamaanisha tutakuwa tukiwapa magaidi muda wa kutangaza ushindi, kuunda upya kundi na kuanzisha uzinduzi wa mashambulio zaidi," aliiambia Sabahi. "Kwangu mimi, huu ni muda ambao operesheni inapaswa kuimarishwa kwa sababu [al-Shabaab] imedhoofishwa na kuzikimbia kambi zao."
Werunga alisema kuendelea kwa mashambulio nchini Kenya kulikuwa matokeo ya kushindwa kwa usalama wa ndani.
"Wanajeshi wetu wanapaswa [kubaki] nchini Somalia hadi watakapoondoa tishio la ugaidi, lakini hawapaswi kushirikishwa katika masuala ya siasa ya nchi ya Somalia," alisema Werunga, akiongeza kwamba serikali ya Kenya inapaswa kushughulikia rushwa nyumbani na kuimarisha kukusanya kiintelijensia ili kuzuia mashambulizi ya ugaidi.
Kwa upande wake, msemaji wa zamani wa rais wa Somalia na mshauri mwandamizi Abdirahman Omar Osman Yarisow alisema malumbano ya kujitoa kwa vikosi vya Kenya nchini Somalia hakuna sababu na hakuna busara.
"Kipaumbele ni kuwashughulikia al-Shabaab. Kujitoa kokote kwa vikosi vilivyopo chini ya utaratibu wa AMISOM kutamaanisha mbinu iliyodhoofishwa katika kuwashughulikia al-Shabaab," aliiambia Sabahi.
"Kujitoa kwa KDF kungesababisha matatizo katika mji wa bandari wa Kismayu ambako masalia ya al-Shabaab wanaweza kuungana na kuteka tena bandari ambayo ilikuwa ikifanya kazi kama kiungo chao cha utendaji," Yarisow alisema.
"Sisi, watu wa Somalia na serikali niliyokuwa nikiitumikia muda mfupi uliopita, tunaikubali na kuipongeza kazi ambayo vikosi vya Kenya vimefanya kwa Somalia," alisema. "Ni bahati mbaya kwamba wahalifu wameamua kushambulia Kenya kwa kile wanachodhani ni ulipizaji kisasi."
Eunice Oloo, wakili na ofisa wa sheria wa Rights Promotions and Protection Centre iliyopo Nairobi, alisema aliunga mkono uamuzi huo wa kuvibakiza vikosi vya Kenya nchini Somalia kwa sababu imesaidia kutuliza taifa na kupunguza migogoro ya kibinadamu kule.
"Mzigo ambao migogoro ya kibinadamu imekuwa ikisababisha kwa Kenya na wabia wengine wa maendeleo kwa kuwatunza wakimbizi ambao wamekuwa wakikimbia vita nchini Somalia umekuwa ni mkubwa," aliiambia Sabahi.
"[Kwa hiyo] kuendelea huko kwa vikosi hivyo kunatafsiriwa kuifanya Somalia kuwa na utulivu. Katika upande mwingine, kujitoa kutatafsiriwa kuwa […] watu wengi kukoseshwa makazi, watu wengi ambao wataishia kuwa wakimbizi nchini Kenya," alisema.
Athari ya kujiondoa kwa usalama wa ndani
KDF inachangia zaidi ya vikosi 3,600 katika AMISOM, hivyo kama Kenya itajitoa, litakuwa pigo kwa uthabiti wa misheni na operesheni za kijeshi, kwa mujibu wa Abdikarim Daud Nur, mwanajeshi wa zamani wa jeshi la Somalia ambaye anafundisha sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Mogadishu.
Hata hivyo, alisema kujitoa hakutawezekana na hakuna madhara katika usalama wa ndani wa Kenya, kwani wanamgambo wa al-Shabaab walikuwa wakilenga Kenya kabla hata haijapeleka vikosi vyake Somalia.
"Iliichukua Kenya muda mrefu kuwa sehemu ya AMISOM ili iweze kulinda mahitaji yake ya kimkakati," aliiambia Sabahi. "Kwa hiyo, sidhani kwamba itaiachia fursa hiyo kwa urahisi kutokana na milipuko michache na vitisho kutoka kwa al-Shabaab."
Kitu kilicho na athari juu ya usalama wa ndani ni ukamataji holela wa Kenya kwa watu wenye asili ya Kisomali na Waislamu kwa jumla, Nur alisema. "Hilo litaaanza kujenga chuki za kididni na itapelekea vijana wengi kujiunga na al-Shabaab na al-Qaeda."
Kanali Abdullahi Adamu Irro, mwanachama wa zamani wa jeshi na pollisi ya Somalia wakati wa Mohamed Siad Barre, walikubaliana kwamba kujitoa ndani ya Somalia hakutaboresha usalama wa ndani wa Kenya.
"Kinyume chake, kinachoweza kutokea ni kwamba [al-Shabaab] wanasema 'Kenya imedhoofika' na kuendelea mashambulizi yao kuilenga Kenya," aliiambia Sabahi.
Irro pia aliunga mkono wasiwasi juu ya atahri ya uondoaji ungekuwa kwa mashambulizi kijeshi ya jumla ya AMISOM na uwezo wa serikali ya Somalia kujenga juu ya mafanikio ya shughuli za kijeshi iliyonayo hadi sasa.
Kama askari wa Kenya wataondolewa, lazima uwepo mpango wa kuchukua nafasi yao mara moja, alisema. "Muda utolewe kwa ajili ya nafasi hizo kujazwa kabla ya Kenya kuondoka kwa sababu kama watajiondoa, itamaanisha kuwa al-Shabaab itachukua maeneo ambayo walitolewa."
Kwa mfano, alisema, wakati majeshi ya Ethiopia yalipojiondoa bila ya kutarajia kutoka Hudur mwaka 2012, al-Shabaab ilirejea na kuwaua raia wengi waliokuwa wakiunga mkono vikosi vya serikali na washirika.
Hata hivyo, Irro alisema ili Kenya kuendelea kushiriki katika AMISOM operesheni kwa uungaji mkono kutoka kwa Wasomali wote, ni lazima kuchukua hatua ya kutoa mafunzo kwa askari wake juu ya masuala ya haki za binadamu na utamaduni wa Somalia, na kuhakikisha nia yake ni wazi kwa watu wa Somalia.
Hatimaye, ni kwa maslahi ya nchi hizo mbili za Somalia na Kenya kuaminiana, kufanya kazi pamoja, kushirikiana kiintelijensia na kupambana na adui pamoja, alisema.
Swali: Unafikiri nini -- askari wa Kenya wanapaswa kuondoka kutoka Somalia? Vipi/Lini? Toa maoni yako katika sehemu ya maoni hapa chini.
Chanzo: sabahionline.com



No comments:
Post a Comment