If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, October 7, 2014

S. Kusini: Kujiunga na AL kutategemea kura ya maoni

Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kuwa, kujiunga nchi hiyo na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kunahitajia maoni ya wananchi na kuitishwa kura ya maoni. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin ameeleza kuwa, suala la Sudan Kusini kuwa mwanachama wa jumuiya ya Arab League litaamuliwa na wananchi wa nchi hiyo. 

Ameongeza kuwa, uhusiano wa serikali ya Juba na nchi zote za Kiarabu ni madhubuti na mzuri.

Katika upande mwingine, mazungumzo kati ya pande hasimu za Sudan Kusini yaliyoanza karibu miezi 10 iliyopita yamesimama. 

Michael Makuei mkuu wa timu ya mazungumzo ya serikali ya Sudan Kusini amesema mazungumzo hayo yamesimama lakini yataanza tena Oktoba 16. 

Ameongeza kuwa, uamuzi huo umechukuliwa ili kila upande upate fursa ya kujadili masuala muhimu kuhusiana na mazungumzo hayo, hasa nafasi ya waziri mkuu na iwapo rais atakuwa mkuu wa nchi pamoja na serikali au la.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako