Fuad Ahmed alichangia ripoti hii kutoka Mogadishu
Makamanda wa kijeshi wa Somalia siku ya Jumatatu (tarehe 6 Oktoba) walishangilia kuichukuwa ngome ya mwisho iliyokuwa ikishikiliwa na wanamgambo wa al-Shabaab, huku wanajeshi wa serikali na vikosi vya washirika vikichukua udhibiti wa mji wa bandari wa Barawe kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miongo miwili.

Wanajeshi wa Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia wakiwaangalia maadui kupitia kioo cha bunduki ya kutungulia kwenye mlima unaotazamana na Barawe katika mkoa wa Shabelle ya Chini nchini Somalia siku ya tarehe 5 Oktoba. (Picha ya AMISOM/Tobin Jones)
"Al-Shabaab hawapo tena Barawe," Naibu Mkuu wa Jeshi la Taifa la Somalia, Jenerali Abdirisak Khalif Elmi, aliwaambia mamia ya wakaazi wa huko, akiwatolea wito wa kuiunga mkono serikali.
Vifaru na magari yaliyobeba silaha yalifanya doria kwenye mji huo siku ya Jumatatu baada ya wapiganaji wa al-Shabaab kukimbia kabla ya kuingia kwao mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wanajeshi wa Somalia na wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini humo (AMISOM) waliingia Barawe siku ya Jumapili "bila ya upinzani mkali", kwa mujibu wa kikosi cha Umoja wa Afrika, lakini operesheni za kuhakikisha usalama zinaendelea.
Kaimu Mkuu wa AMISOM, Lydia Wanyoto, aliwapongeza wanajeshi wa Somalia na AMISOM kwa ushujaa na unyumbukaji wao katika kuuchukua mji wa Barawe na kwa Operesheni nzima ya Bahari ya Hindi.
Alisema Barawe ulikuwa ni mshipa mkuu wa fahamu kwa al-Shabaab na kwamba kushindwa kwao kunaweza kuwa pigo kubwa zaidi kwa kundi hilo tangu wafukuzwe kutoka miji ya Mogadishu na Kismayu.
"Kukamatwa kwa Barawe ni ushindi mkubwa sana kwa Somalia kwani magaidi hao waliitumia bandari ya huko kuingizia silaha na pia kupokelea wapiganaji wa kigeni," ilisema taarifa ya AMISOM: 2 Kundi hili pia liliitumia Barawe kusafirisha mkaa kwenda Mashariki ya Kati, biashara ambayo ikiingiza mabilioni ya dola na ambayo ilikuwa kama chanzo chao kikuu cha fedha."
Wanyoto alisema wanajeshi hawakukabiliwa na upinzani wowote mjini Barawe, lakini wanamgambo wa al-Shabaab waliokimbia walijaribu kufanya uvamizi kwenye viunga vya mji huo.
"Uvamizi wa al-Shabaab ulizimwa haraka sana na wanajeshi wetu waliingia Barawe bila kizuizi, huku kukiwa na furaha kubwa kutoka kwa wenyeji, wengi wao wakiwa wamejipanga mitaani kuvikaribisha vikosi vya washirika," alisema.
Mustakabali mzuri
Kuanguka kwa Barawe ni pigo kubwa kwa waasi, na kunakuja siku chache baada ya kuanguka kwa mji wa Adale katika mkoa wa Shabelle ya Kati na mwezi mmoja baada ya kifo cha kiongozi wa al-Shabaab, Ahmed Abdi Godane, kwenye mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani.
Hata hivyo, al-Shabaab imeapa kulipiza kisasi kifo cha kiongozi wao huyo na kuendelea na mapigano yao ya kuing'oa serikali ya Somalia.
Siku ya Jumamosi, kamanda wa ngazi za juu wa al-Shabaab, Mohamed Abu Abdallah, alisema kundi hilo la wanamgambo lingeliendelea kufanya mashambulizi.
"Mapigano yataendelea na tutaugeuza mji huo kuwa makaburi ya adui," alisema, kwa mujibu wa mtandao unaoiunga mkono al-Shabaab.
Ambapo wanajeshi wengine walifanya msako wa nyumba kwa nyumba, sehemu kubwa ya wanajeshi walikuwa wameweka vizuo vyao nje ya mji huo, alisema Gavana wa Shabelle ya Chini, Abdukadir Mohamed Nur, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
"Operesheni za kuhakikisha usalama zinaendelea," alisema.
"Somalia inaamkia katika hatima inayong'are," Mwakili Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Somalia Nicholas Kay alisema katika ujumbe wa pongezi kwa vikosi vya serikali na AMISOM.
"Hatimaye...amani na uhuru kamili"
Wakazi waliripoti kwamba Barawe ilikuwa shwari na tulivu, na isipokuwa risasi za kusherehekea zinazolengwa hewani.
"Hali ni shwari na hakuna mapigano -- isipokuwa risasi nzito hewani zinazopigwa na wanajeshi wa Somalia na AMISOM wakati walipokuwa wanaingia mjini," mkaazi wa Barawe Isak Mohamed aliiambia AFP.
Baada ya miaka zaidi ya sita ya vitisho katika mikono ya al-Shabaab, wananchi wa Barawe walipumua upumzi wa ahuweni siku ya Jumapili baada ya kikundi hicho kusafishwa kutoka mjini, mzee wa jadi Abdalla Ahmed, mwenye umri wa miaka 53, aliiambia Sabahi.
"Hatimaye tunapata hisia ya amani na uhuru kamili. Hiki ni kitu ambacho tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu," alisema. "Tutajaribu kufikiri jinsi ya kuchukua faida ya maana hii mpya ya matumaini ambayo yamekuja na mwanga na tunamuomba Mungu alisaidi Jeshi la Taifa la Somalia na ndugu zetu wa AMISOM kwa ushindi."
Ahmed, ambaye amekuwa katika mji kwa kipindi cha miaka 20, alisema watu wa Barawe aliishi katika dhiki na chini ya hali ngumu sana kwa kipindi cha miaka sita, zaidi kuliko maeneo mengine yaliyokuwa yanadhibitiwa na al-Shabaab.
"Mji wa Barawe ndio ambapo al-Shabaab walikuwa wanaendesha mauaji mengi yasiyokuwa halali," alisema. "Mwezi uliopita tu walimpiga mawe hadi kufa mwanamake kutoka Barawe baada ya kumtia hatiani kwa kuolewa na wanaume wanne bila ya kuwa na ushahidi wowote. Mpaka sasa hatujawaona wanaume wanaodai walimuao."
Zainab Ma'ow, mama mwenye umri wa miaka 38 na watoto wanane, alisema kuwa alikuwa anakaribisha kwa moyo wote kuondoshwa kwa al-Shabaab, lakini alivionya vikosi vya usalama na wananchi kuwa macho ili kuhakikisha mafanikio ya kudumu.
"Kwanza ushindi ni katika ukweli kwamba tumekuwa huru kutoka al-Shabaab, ambayo ilitunyima uhuru wetu kwa muda mrefu," aliiambia Sabahi. "Hata hivyo, bado tuna hofu kwamba huenda kuna mabaki ya al-Shabaab katika Barawe ambayo kuna uwezekano wa kujificha kati ya umma, hivyo napenda kuwaomba vikosi vya usalama vya Somalia kwa kufanya upekuzi wa kina ili kuhakikisha usalama kwa vile mji hivi sasa uko chini ya udhibiti [yao]. "
Ma'ow alitoa wito kwa wananchi wenzake kufanya kazi na vikosi vya usalama ili kuwakamata wanachama wote al-Shabaab na wafuasi wao ambao wanaweza kuwa wameachwa nyuma.
Vile vile akiwa na wasiwasi kuhusu jinsi ya muda mrefu amani inaweza kudumu katika Barawe, Marian Ibrahim, mwenye umri wa miaka 35 na mama wa watoto sita, alisema kuwa tayari majira ya asubuhi siku ya Jumatatu wananchi waliamshwa na sauti ya milio mizito ya risasi nzito na milipuko kutoka nje kidogo ya mji.
"Baada ya siku chache za furaha, wananchi wanaogopa mara nyingine tena kwamba al-Shabaab wataushambulia mji," aliiambia Sabahi. "Tunawaomba AMISOM kwa kutoa misaada mingi [kwa vikosi vya Somalia] ili kuharibu uwezo wa al-Shabaab kwa sababu walikimbia mji na silaha nyingi na wapiganaji na inawezekana wana mipango ya kuanzisha mashambulizi msituni ya kila siku katika Barawe. "
Chanzo: sabahionline.com



No comments:
Post a Comment