BODI ya kusajili mashirika yasiyo ya kiserikali imekosolewa kwa kutangaza nia ya kufutilia mbali usajili wa mashirika zaidi ya 900.

Bw Kalonzo Musyoka akihutubu awali. Picha/MAKTABA
Akiongea wakati wa kuzindua rasmi ubalozi wa Cyprus nchini Kenya Ijumaa, aliyekuwa makamu wa rais Bw Kalonzo Musyoka aliiambia bodi hiyo haiwezi kudai kufutilia mbali usajili wa mashirika hayo kwa sababu ni sehemu ya jamii.
Akiongea wakati wa kuzindua rasmi ubalozi wa Cyprus nchini Kenya Ijumaa, aliyekuwa makamu wa rais Bw Kalonzo Musyoka aliiambia bodi hiyo haiwezi kudai kufutilia mbali usajili wa mashirika hayo kwa sababu ni sehemu ya jamii.
Bw Musyoka ambaye pia ni kinara wa muungano wa Cord aliwashauri wananchi kupuuza habari kwamba Wakfu wa Kalonzo Musyoka utapokonywa usajili na bodi hiyo kwa kusema wakfu huo umekuwepo kwa miaka mingi.
KMF ilikuwa miongoni mwa mashirika 957 yaliyoorodheshwa na bodi hiyo ambayo hayakuwa yametimiza mahitaji ya bodi hiyo.
“Ningependa kuwashauri wananchi kupuuza habari zozote zinazosema KMF imehasi kwa sababu wakfu huu umekuweko kutoka zamani,” alisema.
Alisema wakfu huo umesomesha zaidi ya watu 2,000 kutoka nchini na umekuwa ukitoa ufadhili kwa wanafunzi kusomea mataifa mengine.
“Ningependa kuifahamisha bodi hiyo kwamba haiwezi kurudisha taifa hili lilikokuwa miaka iliyopita. Mashirika ya kijamii ni sehemu ya jamii ya Kenya na huu sio wakati wa kutatiza ufanyikazi wake,” alisema.
Baadhi ya mashirika maarufu yaliyokuwa katika orodha hiyo ni lile la kutetea haki za kibinadamu la Kenya Human Rights Commission (KHRC), African Population and Health Research Centre, African Development Solutions, Airtel Foundation na Ahadi Trust Kenya.
Bw Musyoka alisema kufunguliwa kwa Ubalozi wa Cyprus nchini ungeimarisha maendeleo na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.
Bw Musyoka alisema, “Ninawatakiwa raia wa Cyprus kila lema,” na kushauri nchi majirani wa Cyprus kuingilia na kusuluhisha mzozo unaoshuhudiwa nchini humo.
Ulizinduliwa rasmi baada ya kuwepo nchini kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Ahadi
Katika hafla ya kufana, Cyprus iliahidi kushirikiana na Kenya kibiashara na masuala ya kiuchumi lakini ikaitaka serikali kuimarisha uhusiano zaidi kwa kuidhinisha mikataba kati ya mataifa hayo mawili.
Balozi wa Cyprus nchini Kenya Charalambos Kapsos alisema, “Cyprus inapendekeza kuidhinishwa kwa mkataba wa uhusiano kati ya mataifa yote mawili kwa sababu ni kigezo muhimu cha uhusiano wa kibiashara.”
Alisema Cyprus ilitazamia uhusiano ulioimarika zaidi na Kenya kwa manufaa ya raia wa mataifa yote mawili.
Uhusiano kati ya Kenya na Cyprus umekuwepo kutoka zamani, na umenawiri mwaka baada ya mwaka mwingine tangu enzi za rais mwanzilishi Jomo Kenyatta, alisema Bw Musyoka aliteuliwa katika wadhifa wa kuiwakilisha Cyprus nchini Kenya mwaka jana.
Alisifia maendeleo ya nchini humo hasa katika sekta ya utalii na juhudi zake za kuisaidia Kenya katika masuala ya elimu.
Akiongea wakati wa hafla hiyo Balozi Josephine Owuor aliyewakilisha Wizara ya Mashauri ya Kigeni alisema uhusiano ulioimarika zaidi kati ya Kenya na Cyprus unatarajiwa punde baada ya mataifa hayo mawili kutia sahihi mkataba.
“Uhusiano wa kibiashara kati ya Kenya na Cyprus umeimarika ingawa kuna baadhi ya masuala tunayohitaji kujikakamu zaidi,” alisema na kuongeza kuwa mikataba kati ya Kenya na Cyprus itatiwa sahihi hivi karibuni.
Balozi huyo aliisifia Cyprus kwa kuisaidia Kenya katika kufanikisha masuala kadhaa ikiwemo ni pamoja na ujenzi wa mahospitali, shule na utoaji wa huduma za bure za matibabu.
Source: swahilihub.com



No comments:
Post a Comment