Na Ahmed Ally Abdallah, Swahilivilla Tanzania
Hata hivyo, kijiji hichi kilizidi kupata faraja pale ambapo jengo la kufanyia semina lilipokamilika mnamo mwaka 2010, jengo ambalo dhamira kubwa ilikua ni kujenga shule ya msingi, lakini kwa bahati mbaya, serikali ya Tanzania ya awamu ya tano ikapitisha sera ya kuzuia kujenga skuli katika eneo lisilotimu heka nne, na hivyo, kutokana na Shina Inc kuiheshimu serikali na mifumo yake wakabadili matumizi ya jengo hilo na kulifanya kua jengo la kujikwamua kiuchumi kwa wanawake wa Bugandika, Jengo hili lilianza kujengwa mnamo mwaka 1992 na kukamilika mnamo mwaka 2010 na hivyo kuwa jengo la kwanza kutunukiwa jina la Itika women centre kwa kumuenzi mama yake bi Jessicaa aliyeitwa Kokuitika, kwa maana ya kua ukiitwa uitike, na ndivyo wanajamaii wa sehemu mbalimbali za Tanzania walivyokua wakiitika wito waliyoitwa na Shina Inc. kwa sasa jengo hili hukodishwa kama ukumbi, lina jumla ya viti 300 na limekua sababu moja wapo ya kuwaingizia wanawake wa bugandika kipato chao cha halali huku harakati zao nyengine za kujikwamua kiuchumi zikiendelea.
Sambamba na hayo, wanafunzi wa shule walijipatia zawadi kemukemu kutoka Shina Inc zikiwemo viatu, nguo za kujifunikia kutokana na baridi pamoja na kuzuwia mbu, na hata madaftari na kalamu, hii ni tabia endelevu kwa Shina Inc kutoa misaada ya namna hii kwa kila jamii wanayoenda. Hata hivyo, elimu kwa wanawake iliendelea kutolewa kiasi cha kusema kua, semina ya Jitambue Kama Kikundi ilifanyika kwa wanawake wa Bugandika.
Safari ya bi Jessica na rafiki zake wa Amerika haikuishia Tanzania bara pekee, lakini pia walidiriki kutembea juu ya maji kiasi cha kuwatoa Tanzania bara na kuwapeleka huko visiwani Unguja na Pemba, walianza kwa kuuvuka mkondo wa Nungwi na kisha wakaelekea moja kwa moja hadi katika eneo la Shengejuu na Ziwani, na huko ndipo kazi za shina Inc ziliposhamiri na kuwavutia sana wanajamii wa huko kisiwani Pemba. Awali kabla ya yote changamoto ya dini, uongozi pamoja na utamaduni ilimkumba bi Jessica kiasi cha kumfanya atoe semina kuhusiana na umuhimu wa wanawake katika jamii, ndipo hapo alipokitia moto kichaka na kufanya wanajamii hasa wanawake kutumia eneo fursa kama njia ya kutimiza ndoto zao.
Shina Inc kwa Pemba ilianza kufanya kazi na shirika la JUMAK na msaada wao zaidi ullilenga kwa mayatima, wanafunzi, watu wenye ulemavu na wanawake chini ya mratibu wao wa huko Pemba aitwae Dadi Hamad Dadi. Jumla ya mayatima 101 walipokea msaada kutoka kwa Shina Inc sambamba na wanafunzi wa shule ambao walisaidiwa sare, viatu na madaftari ili kukuza uzalishaji wa wasomi kisiwani humo, hata hivyo, kwa watoto wenye ulemavu walisaidiwa sana katika kupatiwa vigari vya kutembelea, magodoro, mashine za kupimia presha, na seti ya afya kila baada ya miezi mitatu na muda mwengine wakipatiwa pesa za kujikimu pale ambapo zinapopatikana, jumla ya walemavu 55 kutoka Shengejuu na Maziwani walipatiwa huduma hiyo, jambo hili liliwagusa sana Shina Inc kiasi cha kutaka kufungua kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu kwa siku kilichopewa jina la WBB Centre, wakanunua eneo, wakalitia uzio, barabara ikafika, umeme ukafika na maji yakapatikana, na hivyo mji mpya ukawa, lakini cha ajabu, harakati zao zilikwama mwishoni kutokana na changamoto za kiserikali zisioweza kuepukika, na hivyo Shina Inc ikaligeuza eneo hilo kuwa ni kituo cha kujikwamua kiuchumi kwa wanawake wa eneo hilo la maziwani na shengejuu, jumla ya vikundi 350 vyenye watu wasiosizidi 20 kwa kila kikundi viliunda, na hivyo wanawake wakapata fura ya kulima mbogamboga, wengine hupanda migomba, matunda na hata ufugaji wa kuku na mbuzi, na hivyo kujipatia riziki zao za halali.
Shina Inc imewapelekea mashine ya umwagiliaji na kuwasaidia katika kulipia bili ya maji ili mradi huu wa kilimo upate kuendelea, kikubwa zaidi, imewapelekea mashine kubwa ya uzindikaji wa mbogamboga na matunda kiasi cha kuyahifadhi na kuyauza katika sehemu mbalimbali, hata hivyo bado wamekosa nembo zenye ubora ambapo hupelekea kuangusha kiasi fulani soko lao la je ya nchi, kitu kikubwa walichovutiwa Shina Inc kwa watu hawa ni namna wanavyojitolea, wanavoungana na kujua thamani ya shukurani kwa yule anaewafadhili na kuwatendea wema, jambo ambalo Shina Inc linawavutia na kutamani kuwekeza katika jamii hizi mara kwa mara.
Safari ya bi Jessica na rafiki zake kutoka huko Amerika ilitia nanga huko Makunduchi kisiwani Unguja, Shina Inc chini ya mratibu wao wa Makunduchi Unguja Hija amir, yatima wameweza kuotesha shina la kuwasaidia wanafunzi na watu wenye ulemavu na mayatima, mwaka 2007 walipokea mayatima 81 mpaka mwaka huu wa 2018 walemavu 13 na mayatima 15 tu ndio waliyosalia katika kupokea huduma hiyo, wote walisomeshwa, wakatunzwa na kushughulikiwa vizuri kiasi cha wao wenyewe kuridhika na kuhisi kuwa ni watu wenye haki ya kuishi kama walivyo viumbe wengine. Wanafunzi nao hawakuachwa mbali kwenye shina la makunduchi, kila mmoja alipatiwa kile alichokiagiza katika shirika hili la Shina Inc, daftari, kalamu, viatu, sare za shule wote walipatiwa, na hivyo Shina Inc likatoa faraja kwa watoto hawa waliyopenda kujiendeleza kimasomo.
Kina mama nao hawakuwa mbali, elimu ya kujikomboa ikawafikiana hivyo miradi ya kilimo hasahasa mbogamboga ikaanzishwa, aliyekuwa waziri wa maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na watoto Muheshimiwa Abuu nae hakuwa nyuma katika kuwashika mkono wanawawake na watoto, nae akajitolea kuwa mlezi wa Shina Inc huko Makunduchi, na hivyo baada ya miaka mitatu kufanikiwa kuvisajili vikundi 3 vya kina mama, hii ikawa faraja pekee kwa kina mama wa Makunduchi.
Waratibu wa shina Inc nchini Tanzania wamefarijika sana kuweza kufanya kazi na shirika hili, kwani limewajengea uwezo wa kujitambua, kujikwamua kimaisha na kujenga imani iliyokubwa ya kuzisaidia jamii zao, wameelewa kuwa kiengereza kina umuhimu wake lakini pia sio kigezo cha kumfanya mtu adharaulike, kwani kila lugha inanafasi yake katika ulimwengu na jamii zilizotuzunguka, Shina Inc imewapatia fursa ya kujifunza nje ya Tanzania kwa waratibu wake wote hasahasa katika kongamano la umoja wa vijana Afrika linalojulikana kwa lugha ya kiengereza kama Youth African Conference, lililofanyika huko nchini Ghana, kabigiza fortunatues mratibu kutoka Bukoba, Betson Shengoma mratibu kutoka ilemela, na Dadi Hamad Dadi mratibu kutoka Pemba wote walipata fursa ya kuhudhuria katika kongamano hili.
Zaidi ya hayo, Shina Inc haitoi mikopo, Shina Inc haina riba, si kama wanafanya yote kwa sababu wanapesa za kutosha, bali wanawatu wenye kujitolea kwa lengo la kusaidia jamii masikini na zenye mahitaji kama hizi, wao wamejitolea, wamejenga uaminifu na Shina Inc na kuwatayari kuwanyanyua pale wanapojikwaa na kuanguka.
Ni maneno yasiyopingika kuwa mchuma janga hula na wa kwao na kinyue chake ni mchuma chema hula na wa kwao, nasi hatuna budi kuyatia maanani maneno haya ya muandishi maana ya tija kubwa kwa yule mwenye kuyazingatia akilini, tuliyopata fursa ya kuhama nchini tunawajibu wakuchuma chema na kukileta nyumbani, kidogo unachokitoa ni kikubwa kwa yule unayempatia, ndio maana wahenga wakanena “haba na hapa, hujaza kibaba” kinyume chake ni kwamba “mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba”.
Wakati umefika kuweza kuwasaidia na kuwanyanyua wananchi na ndugu zetu wa nyumbani huko barani Afrika hasahasa kundi la wanawake, watoto na wazee, ni muda wetu sasa kulipa fadhila za yule aliyetuzaa, akatupokea, akatukuza, akatusomesha, akatufunza maadili, akatupa tonge ya ugali, wali, dagaa, samaki au hata mboga, tukajengewa mapenzi, tukapata ,marafiki, tukaunda vikunda, tukaunda jamii, tukawa kitu kimoja na mwisho kupata fursa ya kuihama miji yetu kwa lengo la kwenda kutafuta, mkumbuke kuwa “mkataa kwao Mtumwa” sisi tulikuwa kama wao na wao wanatamani kuwa kama sisi.
Mwisho.
Mwisho.













No comments:
Post a Comment