Mjadala Shehemu ya kwanza na ya ya pili kuhusu mustakabali wa Jumuiya mbalimbali za waTanzania katika DIASPORA baada ya kufunguliwa kwa matawi ya vyama mbalimbali vya siasa katika nchi husika.
Pichani ni washiriki katika Mjadala huu Bwn. RAYMOND ABRAHAM Makamu Rais. Jumuiya ya waTanzania DMV (Picha ya kwanza Kushoto) akifuatiwa na Bwn. LIBERATUS MWANG'OMBE Katibu Mstaafu wa Tawi CHADEMA DMV, Bwn. GEORGE SEBO Mwenyekiti Mpya wa (Tawi) CCM DMV, Bwn. YACOB KINYEMI Katibu wa Tawi CCM. DMV, Bwn. IDDI SANDALY Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV, akifuatiwa na Bwn. KESSY JANABI Rais Mstaafu wa Jumuiya DMV, Bwn. YUSUPH M. YUSUPH Mwenyekiti wa Jumiya ya kiIslamu, TAMCO, pamoja na Mch FERDNAND SHIDEKO The Way of The Cross Gospel Ministry na wa mwisho kabisa ni Muongozaji wa Mjadala Mubelwa Bandio
Katika mjadala huu uliohusisha wakazi wa Washington DC na vitongoji vyake (DMV), washiriki wanajaribu kujadili namna tulivyofika hapa na pia namna ya kuweza kujinasua toka katika hii dhana ama hali halisi ya TATIZO la mgawanyiko unaoanza kujitokeza kutokana na ITIKADI miongoni mwa waTanzania.
Karibu uungane nasi



No comments:
Post a Comment