If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, September 7, 2016

KENYA: KOIGI WA WAMWERE AJIUNGA NA JUBILEE PARTY

Na MWANGI MUIRURI

KINARA wa Chama Cha Mwananchi (CCM) Bw Koigi wa Wamwere Jumatano amekivunja chama hicho na kutangaza kujiunga na kile kipya cha Jubilee Party (JP).

Bw Koigi wa Wamwere akihutubu wakati wa kikao maalum kilichoandaliwa na Ubalozi wa Venezuela, Nairobi, Junanne. Picha/WANDERI KAMAU

"Huu sio wakati wa kukwamilia vyama vya mfukoni ilihali kuna mwamko mpya wa kujiunga na chama cha kitaifa kinachowaleta Wakenya wote pamoja bile kuwagawa katika vyama vya mtu binafsi, eneo fulani au katika ubaguzi wa aina moja au nyingine," amesema Koigi wa Wamwere.

Taarifa ya habari aliyotuma kwa vyombo vya habari inasema: "Mimi nikitafakari na na nikizingatia tajriba yangu ya kisiasa nimeona manufaa makubwa yamo njiani katika uwiano wa kitaifa ndani ya chama cha Jubilee Party, vita ambavyo nimekuwa nikipambana kuafikia ndani ya chama changu kidogo cha nyumbani cha CCM.”

"Sasa natangaza rasmi kuasi umiliki wa CCM na kuanzia sasa hivi natambulika kama jenerali wa chama cha JP na nitashiriki kikamilifu mikakati yake ya kuzinduliwa rasmi na Rais Uhurtu Kenyatta na Naibu wake Bw William Ruto na kisha nishirikiane nao katika kutafuta kura za kutosha za kuirejesha serikali ya Jubilee mamlakani kwa awamu ya pili."
Kujihisi nyumbani


Aliwataka wafuasi wake wamfuate ndani ya JP na wajihisi nyumbani “kwa kuwa kile chochote ambacho kinaweza kutuleta pamoja kama Wakenya na kutema uhasama wa jadi wa kisiasa ni cha kukumbatiwa kwa dhati.”

Akasema: “Ikiwa unajua kwa kweli kuwa kujisajili kwako ndani ya CCM kulikuwa kwa manufaa ya kusaka umoja wa Wakenya na kuendeleza mikakati halali ya kusaka utawala bora, basi mimi kama Bw Wa Wamwere nakushauri ujitoe kwa chama kidogo na tuingie nyumba kubwa ya Jubilee ili tufunge safari ya pamoja tukiwa wengi ya kutuelekeza kwa manufaa halisi kwa taifa hili na watu wake.”

Chama hicho cha JP kimepangiwa kuzinduliwa rasmi kuanzia Alhamisi na harakati hizo ziendelezwe kwa siku tatu mfululizo huku Rais na Naibu wake wakijitokeza hadharani Jumamosi kukipamba kama chombo chao cha kuwania uchaguzi mkuu wa 2017.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako