If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Showing posts with label Ikulu: Rais hataidhinisha mamilioni ya wabunge. Show all posts
Showing posts with label Ikulu: Rais hataidhinisha mamilioni ya wabunge. Show all posts

Tuesday, February 4, 2014

Ikulu: Rais hataidhinisha mamilioni ya wabunge

Dar es Salaam. Ikulu imesema Rais Jakaya Kikwete hatakubali kuidhinisha kama akipelekewa ombi la kuongeza kiinua mgongo cha wabunge kutoka Sh43 milioni hadi Sh160 milioni.

Wabunge wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwahutubia kwenye Ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma, Novemba 7 mwaka jana. Picha ya Maktaba

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana kuwa Rais Kikwete hajapokea maombi hayo huku akipinga maelezo kuwa Serikali ilishayakubali.

Gazeti dada la The Citizen wiki iliyopita, lilimkariri Waziri wa Fedha, Saada Mkuya akisema Serikali ilikuwa imepitisha kupandishwa kwa kiwango cha kiinua mgongo kutoka Sh43 milioni hadi Sh160 milioni baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitano.

Waziri huyo alikaririwa akisema kuwa kiwango hicho kilipitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na tayari wabunge walishaanza kuchukua fedha hiyo licha ya ukweli kuwa Bunge hili halijamaliza muda wake.

Hata hivyo, Rweyemamu alisema nao wamelisoma suala hilo kwenye magazeti na kwamba halijafika Ofisi ya Rais... “Suala hili halijafika Ofisi ya Rais hata kama litaletwa, `I really doubt if the President will endorse such matter’ (Nina shaka kama Rais ataidhinisha suala hili).”

Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi tayari imekanusha vikali taarifa za kupandishwa kiwango hicho cha malipo kwa wabunge.

Maoni yako