If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Showing posts with label Jaji Warioba: Siendi Dodoma makabidhiano ya Katiba. Show all posts
Showing posts with label Jaji Warioba: Siendi Dodoma makabidhiano ya Katiba. Show all posts

Tuesday, October 7, 2014

Jaji Warioba: Siendi Dodoma makabidhiano ya Katiba

Na Fidelis Butahe na Habel Chidawali, Mwananchi

Dar/Dodoma. Wakati Katiba inayopendekezwa ikikabidhiwa kesho kwa Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hata akialikwa katika sherehe hizo hatahudhuria kutokana na majukumu aliyonayo kwa sasa.

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.PICHA|MAKTABA

Jaji Warioba alisema angependa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo pia itahudhuriwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wakuu wa mikoa, mabalozi na wageni mbalimbali, lakini kutokana na dharura aliyoipata haitawezekana.

Sherehe hiyo itafanyika mkoani Dodoma kesho na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta atakabidhi nakala ya Katiba inayopendekezwa kwa Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

Katika hafla hiyo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, wajumbe wa Bunge hilo walioshiriki mchakato huo kuanzia mwanzo mpaka mwisho watapewa vyeti.

Akizungumza na gazeti hili jana, Jaji Warioba alisema hadi jana hakuwa amepata mwaliko lakini hata kama akipewa hataweza kuhudhuria. “Siwezi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa siku mbili tatu hizi kwa sababu nina dharura. Kama wakinialika nitawaomba radhi kwamba sitaweza kuhudhuria,” alisema.

Alipoulizwa iwapo Jaji Warioba ni miongoni mwa waalikwa katika sherehe hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi alisema angetoa majibu leo kuhusu suala hilo lakini anaamini mkongwe huyo ni miongoni mwa viongozi wastaafu, hivyo kualikwa ni lazima.

Maoni yako