If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, September 6, 2012

Kituo cha Wajir chatambuliwa kama kiongozi katika usuluhishi wa migogoro

Miaka miwili baada ya kuanzishwa, Kituo cha Amani na Utafiti Mahususi cha Kenya (CEPAR) katika Jimbo la Wajir kinapata kutambuliwa ndani ya nchi na kimataifa kama kiongozi katika utatuzi wa migogoro.

Mamia ya Wakenya wamefunga barabara inayounganisha Nairobi na mkoa wa magharibi kuandamana kupinga kushindwa kwa serikali kuzuia mapigano ya kikabila kati ya Wamaasai na Wakikuyu kuhusiana na maji na ardhi katikati ya Bonde la Ufa mwaka 2005. [AFP]

Kituo kimeonesha miaka 30 ya utendaji mzuri katika kutatua migogoro kulikofanywa na jamii za Wajir, wakiwashirikisha kusaidia kufikia amani ya kudumu katika Jimbo la Kaskazini Mashariki na kuwaonyesha kama mfano kwa jamii nyingine katika kuiga, kwa mujibu wa mkurugenzi wa CEPAR Hussein Adan Mohamud.

"Hadi mapema mwaka huu, kituo kilikuwa hakijulikani nje ya Wajir katika jimbo la Kaskazini Mashariki," Mohamud aliiambia Sabahi. "Lakini katika miezi mitano iliyopita, kimekuwa kikiwavutia watu kutoka sehemu nyingine za nchi na dunia inapenda kutafiti na kujifunza taratibu za utatuzi wa migogoro zilizotumiwa na wakaazi wa Wajir kumaliza mgogoro wa kikabila uliyodumu kwa miaka zaidi ya 20".

Licha ya kuwavutia raia na viongozi wa serikali kutoka majimbo ya Bonde la Ufa na mashariki ambayo yanakabiliwa na migogoro ya kikabila, kituo pia kimewavutia wajumbe wa serikali za kigeni na raia kutoka Ethiopia, Somalia, Kambodia, Rwanda, Afrika Kusini, Uganda na Marekani, Mohamud alisema.

"Mwanzoni mwa mwaka, kituo kilipokea wageni wachache wasiofika watano kwa mwezi, lakini tangu Machi, idadi imeongezeka hadi wastani wa watu 30 kila mwezi," alisema.

Wageni wanajifunza kwa kuchanganyika kupitia semina na kujihusisha na jamii za wenyeji. "Tunahisi maarifa na jitihada zilizobuniwa na jamii za Wajir katika kutatua migogoro ziendelezwe na kufuatwa na wengine," Mohamud alisema. "Sasa tunawavutia watu wanaotaka kujifunza kutoka kwetu."

Kituo kilianzishwa na waasisi kutoka Wakala wa Amani na Maendeleo wa Wajir (WPDA), ambao walitumika kumaliza migogoro ya kikabila ambayo iliikumba Wajir miaka ya 1980. WPDA ilianzisha kamati za amani zenye wazee, vijana, wanawake, viongozi wa dini na mamlaka za serikali katika kila kijiji kwa ajili ya kufuatilia migogoro na kuishughulikia haraka ili kuzuia migongano mikubwa.

WPDA pia ilijihusisha katika shughuli za kielimu kuzuia ukereketwa wa kupingukia, kama vile ujenzi wa chuo kikuu cha kwanza katika jimbo la Kaskazini Mashariki na kuwaelimisha wazazi kuhusu dalili za tahadhari ambazo watoto wao wanaweza kwa kuangukia katika mikusanyiko mibaya..

CEPAR imeungana na Kituo cha Mafunzo ya Amani na Migogoro huko Cambodia, Akademia ya Amani na Maendeleo huko Hargeisa, Chuo Kikuu cha Hargeisa na Chuo Kikuu cha Eastern Mennonite huko Marekani, alisema Mohamud. Taasisi ya utafiti inapanga kuanza kutunza kumbukumbu za jinsi migogoro inavyomalizwa katika maeneo mengine duniani pia, alisema.

Wageni katika kituo hicho waliiambia Sabahi walifurahishwa na jitihada hizo za amani na wanakusudia kuiga mafunzo hayo watakaporudi katika maeneo na nchi zao.

Samuel Toroitich Abus, mjumbe wa Kamati ya Amani ya Wilaya ya Kusini ya Keiyo katika Jimbo la Rift Valley, aliiambia Sabahi kwamba kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha utulivu katika makabila tofauti tofauti. "Hata vijana na wanawake wana majukumu muhimu sana katika jitihada za amani," alisema.

Joseph Rotuk, mjumbe wa Kamati ya Amani ya Wilaya ya Kericho katika Jimbo la Rift Valley, aliiambia Sabahi amejifunza somo la msingi sana katika CEPAR. Alisema Kamati za Bonde la Ufa zimeanzishwa baada ya kamati za huko Wajir, zikiwa na kundi tofauti lililoshiriki katika jitihada za amani.

"Nimejifunza kwamba amani inahusisha mazungumzo na makubaliano," alisema. "Haijalishi jinsi gani mtu alivyodhulumiwa, mmoja wapo anapaswa kurudi nyuma kwa ajili ya amani ya kuishi kwa pamoja. Ni mchakato wa elimu."

No comments:

Post a Comment

Maoni yako